Kasheshe
JF-Expert Member
- Jun 29, 2007
- 4,694
- 787
Mkuu Mkandara,Guys, I think the man is right!
Mwanakijiji kumbukeni sana nilipiga sana makelele kuhusu matumizi ya neno RUSHWA na tukalitungia sheria bila kufahamu maana na mapana ya neno hilo. Muswada ulisukumwa haraka haraka ukapitishwa ukiwa umeacha mabo mengi sana muhimu. Nakumbuka hata wewe ktk mada mojawapo uliwahi kusema kuwa sii lazima tunapozungumzia Rushwa basi iwe, lazima mtu kachukua/katoa hongo hali tumesahau kuwa CCM waliukubali muswada huu kwa sababu haukuwagusa wao kama viongozi wanao Hujumu uchumi wakitumia wadhifa wao na Azimio la Zanzibar linalowaruhusu kufanya Biashara.
Sasa wataweza vipi kufanya biashara hizo ikiwa hawana ruksa ya kutumia nafasi zao kupata connection?...How will it work halikutazamwa hili..
As a fact hata Rostam Aziz hana makosa ikiwa Richmond ni kampuni yake na hatuwezi mshtaki kwa sababu anakuwa protected na Azimio la Arusha pili, Richmond ni incorporated yaani entity inayojiendesha kama kampuni na tatu hakupokea wala kutoa rushwa kupata Tender hiyo..
Mkorogo wote wa sheria tumefungashiwa sisi na ndio maana Taasisi hiyo ya Dr. Hosea imeitwa - Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Kwa ufinyu wake haiweki hujuma za uchumi wa taifa letu..Deal la Richmond halina ushahidi wowote wa Rushwa lutumika.
Kutumia madaraka yako kupata Tender ya serikali sio kosa wala Rushwa hata kidogo na sheria za Azimio zinawa protect zaidi...
Ni mawazo yangu mnaweza nielemisha zaidi kama nimekosea.
Message yako sawa, lakini umei-twist... naomba usome post yangu hapo juu ndio utaelewa vizuri zaidi