All about Edward Hosea, Mwanyika

All about Edward Hosea, Mwanyika

Wamiliki/Wakurugenzi watajwa - Moh'd Ent. + RA - ni waheshimiwa wabunge ndani ya Bunge tukufu la Jamhuri ya Mwungano!!
 
Jamani 2007 kuna nini? FMES fanya utaratibu tusikilize na upande wa pili
 
mmh hizi habari nyengine kuamini bila ya ushahidi ni ngumu, lakini inawezekana pia.
 
suala nalolijua ni kweli familia ya hosea inaishi marekani,na muda mrefu sasa..na kila mwezi bwana hosea huwa antia timu marekani kuwausalimia wanafamilia wake..sijui anatumia fungu lipi?
 
Wana JF,

Tuipe hii habari benefit of doubt. Familia kuishi Marekani tumeambiwa na Mkombozi hapo juu ni kweli. Kwa Mishahara ya Bongo sio rahisi kwenda Marakani kila mwezi. Mtu aliyepo PCCB aje amwage data, kama vipi tuzitafute.

Mimi kwa mtazamo wangu, hizi habari ni nusunusu, tusitumie kutolea HUKUMU. Tufanye kazi zaidi ili kuthibitisha hayo yaliyomo.

Inawezekana YALIYOMO HAYAMO.
 
haba na haba ujaza kibaba,kwa kuunganisha taarifa tunaweza kupata mbuvu na mbichi.
 
FD
Ni kweli kabisa

Ninacho kifahamu juu ya huyu bwana Hosea ni kuwa familia yake ilikuwepo Uingereza baada ya Mkewe kwenda kusomea huko nadhani ni PhD...............well.....ndio maana nikawa shocked kusikia hizi news za huyu Bwana za kuhusu US. Na yeye mwenyewe Hosea nadhani karibu anamaliza PhD yake..........

NB: sifanyi kazi PCCB.................
 
Vita vya panzi furaha kwa kunguru
haya mambo yatajulikana tu na bado

Mungu yu mwema siku zote
utajificha lakini utafichuka tu
 
Wabunge wamfunga mdomo Hosea

na Happiness Katabazi
Tanzania daima

UAMUZI wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuamua kwa kauli moja, kuunda kamati teule ya Bunge kuchunguza utata katika mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura wa Kampuni ya Richmond umemfunga mdomo Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Edward Hosea.

Ukweli kuhusu hali hiyo ulidhihirika jana, wakati gazeti hili lilipofanya juhudi za makusudi kupata kauli ya mkurugenzi huyo ambaye Mei mwaka huu, alilitangazia taifa kuwa, taaasisi anayoiongza ilikuwa imebaini kutokuwapo kwa dalili zozote za rushwa katika mkataba huo wa Richmond.

“I have no comment,” alisema Hosea na kukata simu mara tu mwandishi wa gazeti hili alipomuuliza maoni yake kuhusu uamuzi wa Bunge kuunda kamati teule ikiwa ni miezi sita tangu taasisi yake iisafishe Richmond, uamuzi ambao ulizusha manung’uniko mengi kutoka kwa wananchi mbalimbali.

Wakati Hosea akikataa kutoa maoni yake kuhusu suala hilo, baadhi ya wasomi, viongozi wa vyama vya upinzani na wananchi wa kawaida wamepokea kwa hisia tofauti uamuzi huo wa Bunge kuunda kamati ya kuchunguza mkataba wa Richmond.

Mwenyekiti wa taifa wa TLP, Augustine Mrema, alisema Takukuru ni chombo kinacholinda wakubwa, kwa sababu wakati wapinzani na wananchi wakilalamika kuhusu mkataba huo, wao waliwaona wazushi.

Muhadhiri Mwandamizi kutoka Kitivo cha Sayansi ya Jamii na Siasa cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu, alisema, uamuzi wa kuunda kamati ya kuchunguza mkataba wa Richmond umechelewa na kwamba umeonyesha wazi udhaifu wa serikali kutokana na ukinzani unaoonyeshwa na taasisi zake.

Profesa Baregu alisema mapema mwaka huu Takukuru ilitoa ripoti yake ya uchunguzi ambayo ilisema mkataba huo haukuwa na chembe wala harufu ya rushwa, hatua ambayo ilipingwa na Watanzania wengi.

Naye Muhadhiri Mwandamizi katika Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, alihoji ni kwanini Bunge halikuchunguza mkataba wa Richmond wakati kashfa ya mkataba huo ilipoibuliwa mapema mwaka jana.

“Binafsi uamuzi wa kuunda kamati ya kuchunguza mkataba huo, umetoa nafasi kwa wahusika wakuu wa kashfa hiyo kupika makabrasha ya kujitetea na sasa serikali imeona makabrasha hayo yametimia, ndiyo maana juzi wakaamua kuunda kamati ya kuchunguza…hii ni danganya toto,” alisema Dk. Mvungi.

Dk. Mvungi alisema ripoti ya Takukuru haikuaminika kwa raia, ndiyo maana serikali na Bunge vimeamua kuunda kamati ya Bunge ili waweze kujisafisha vizuri.

“Mimi ninahoji, kipindi chote hiki cha mwaka mmoja sasa kimepita, Bunge lilikuwa wapi? Na kama lilikuwa na nia njema na taifa hili, kwanini halikuunda kamati tangu mwaka jana? Ningependa jambo linapotokea lichunguzwe kwa wakati ule ule na si kutoa nafasi kwa wahusika kupika makabrasha ambayo yakija kuchunguzwa na kamati hizo tunaambiwa hakukuwa na rushwa,” alisema Dk. Mvungi.

Mei mwaka huu Takukuru ilitoa taarifa ikionyesha kuwapo kwa uzembe katika kuingia kwa mkataba kati ya Kampuni ya Richmond kwa upande mmoja na Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco) kwa upande mwingine.

Hata baada ya kukiri kwamba, kulikuwa na kile ilichokielezea kuwa uzembe katika kuipa mkataba kampuni hiyo, Takukuru wakati huo ikijulikana kama Takuru ilieleza bayana kwamba, kampuni hiyo haikuwa na uwezo wa kukidhi matakwa ya mkataba huo.

Ripoti hiyo ya Takukuru kwa upande mwingine ilibainisha kwamba, Richmond ilikwama katika mchakato wa kwanza wa kutafuta kampuni ya kuipa mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura baada ya kuonekana kutokuwa na sifa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baada ya kuona hivyo, Richmond ilitangaza kushirikiana na kampuni maarufu ya utengenezaji wa vifaa ya umeme ya Pratt & Whitney, ushirikiano ambao unadaiwa kuwa ndiyo uliowafanya wajumbe wa kamati maalumu iliyoundwa na Waziri Mkuu, Edward Lowassa, waipe mkataba kabla ya kubaini kuwa maamuzi hayo yalikuwa na makosa pia.

Pamoja na kukiri kuwapo kwa kile kilichoitwa uzembe na Takuru, ripoti hiyo ya maandishi ya kurasa 12 iliyosomwa na Hosea mwenyewe mbele ya wanahabari, iliwasafisha viongozi wa serikali kuwa hawakuhusika katika vitendo vya rushwa wakati wa mchakato mzima wa kutafuta kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura.

Hata hivyo pamoja na ripoti hiyo kukiri kuwa Waziri Mkuu Lowassa ndiye aliyeamua kubatilisha uamuzi wa kutafuta kampuni kwa njia ya kutangaza zabuni kimataifa, bado ilishindwa kutoa tathmini iwapo uamuzi huo ulikuwa wa manufaa kwa taifa au la.

Uzembe pekee uliotajwa katika ripoti hiyo ni madai kwamba, serikali haikufanya juhudi za kutosha kuchunguza uwezo wa kampuni hiyo ambayo ilishindwa kukidhi matakwa ya kuzalisha umeme kwa wakati, kabla ya kuuza mkataba wake kwa Kampuni nyingine ya Dowans.

Hata hivyo, katika mazingira ambayo hakuweka wazi, aliutetea uzembe huo na kusema kuwa hauwezi kuhesabika kuwa ni kosa, kwa sababu haukusababisha hasara.
 
Just imagine that head of FBI, MI5, Surete or KGB going public stating that we have design a device that will capture all sexual activities that are a result of bribery, what would world think of this head honcho?

It is amazing that our PCCB head man Hosea, would map out the geniousness of his administration during formal anouncement of National Anti-corruption Strategy and Action Plan (NACSAP II). The meat and potatoes of this second round of kubana rushwa ni rushwa za ngono!

I would have expected that he would have stated that they are investing on scientific and human intelligence to fight corruption and not sex videos!

Hivi sexual bribery ndio zinazotuangamiza kama Taifa au ni mikataba na mikopo bomu?

What a waste of time and mind! No wonder Waziri Mkuu wa Canada na Waziri Mdogo wa UK wanatushangaa tulivyo na sheria mbovu!

May be I am short sighted and to critical for Serikali and people may call me insensitive to issues that affect and degrade women!


RRRK

Device to keep sexual bribery in check ready

2007-11-28 09:07:10
By Jane Mkonya


The Prevention and Combating of Corruption Bureau has said it has come up with a device to help nab people soliciting sexual favours from women as a bribe.

PCCB Director General Edward Hoseah made the revelation to journalists at an occasion to unveil the enhanced National Anti-corruption Strategy and Action Plan (NACSAP II) in Dar es Salaam yesterday.

`The device will record voices as well as take pictures of people demanding sexual favours. We therefore call upon women to cooperate with the authorities concerned in efforts to curb sexual corruption at workplaces and elsewhere,` he said.

Hoseah explained that some victims have not been reporting their cases to the bureau, thus making the incidence of the vice appear low while the media are inundated with reports of such incidents.

`We will monitor corruption in Government ministries, departments and agencies and in the private sector and we will take appropriate action against all those suspected to be behind them,` he stated, adding that President Jakaya Kikwete has already blessed the strategy.

The PCCB chief reiterated his earlier stand that they will seek to tame not only cases of petty corruption but also those involving prominent people and institutions in both the public and private sectors.

He said the bureau would provide women willing to cooperate in the campaign with special gadgets capable of secretly recording voices and taking pictures of the suspects.

`The women will be required to carry the gadgets along with them wherever they go but in extreme secrecy to ensure maximum safety, confidentiality and efficiency,` he pointed out.

He said that, under NACSAP II, it is expected that corrupt tendencies and practices in the central and local government authorities would be effectively monitored and reported for appropriate action.

`We are sure that fighting corruption, particularly in the rich areas like natural resources which generate vast amounts of revenue, will enhance domestic resource mobilisation for national development and reduce donor dependence,` noted Hoseah.

Philip Marmo, Minister in the President`s Office (Good Governance), said in remarks at the occasion that the establishment of national strategy was in partial implementation of recommendations by the mid-1990s Presidential Commission on Corruption chaired by former Prime Minister Joseph Warioba.

`It is a continuation of the anti-corruption efforts made by the Government during the implementation of the strategy`s first phase - NACSAP I.

It is the Government`s expectation that NACSAP II will be the main vehicle for carrying out the spirit and intent of the national anti-corruption policy,` added the minister.
  • SOURCE: Guardian
 
Ama kweli Tanzania tuna watu wanaotudhania sisi "hamnazo". Sasa kama hicho kifaa kipo (kinaitwa recorder au kamera) kwanini kisitumike kuwawekea mtego wanaotaka rushwa ya aina yoyote ile? Kwanini wachague ya "ngono" au wanataka kuona visivyoonwa hadharani na kusikia visivyonong'onezwa mbele za watu?
 
ndio maana kuna watu wanaamini tumelogwa, nafikiri tumejiloga wenyewe.
 
Ama kweli tuna viongozi mwaka huu. Hata kama kulikuwa na ulazima huo basi, kwa nini watangaze kama wanataka kunasa watu ki-intelijensia?
 
Ama kweli tuna viongozi mwaka huu. Hata kama kulikuwa na ulazima huo basi, kwa nini watangaze kama wanataka kunasa watu ki-intelijensia?

....exactly!! Nurujamii........i mean...........this is very low from Hosea and his team
 
Kali nini tena...hiyo mbinu yao mpya ama...?

Halafu sio wote wakulima humu....wengine ndo tumeamka....na sasa ndo tunajiandaa na thedi shifti....si unajua boksi liabebeka vizuri usiku
 
....exactly!! Nurujamii........i mean...........this is very low from Hosea and his team

Hey say Dr. Hosea...

In reality PCCB is not capable of fighting the monster, corruption. Have you ever tried to reach them and try to give info that will lead to disclosing corruptive practices of any of the big fishes? Just try and see; you will be interrogeted with hostility as if you are a suicide bomber!
Believe me or not, they are there to serve the interests of big "fisadis". Do you remember how they cleared the Richmond scandal?
wanatuchezea kwa kutueleza mikakati ya kipuuzi juu kushgughulikia rushwa...rushwa ya ngono! hata hivyo hiyo effect yake kwenye uchumi ni negligible

Lakini wanafanya maigizo haya huku wakitafuna kodi yetu..oohooo..kudadadeki.
 
I will side with Hosea. Kama nimeshindwa kuwakamata wala rushwa wanaolitia umaskini taifa, labda nitaonekana wa maana nikifanya comedy ya kukamata wanaoomba rushwa ya ngono, lakini pia ni lazima apambane na wanaotoa rushwa ya ngono. Lazima afanye hivyo, kwa sababu ameprove failure, hata wewe uki-prove failure utafanya hivyo.
 
Amepata Ph.D juzi; mpeni nafasi aitumie, itaweza kumponya kutokana na upuuzi wa aina hii
 
Back
Top Bottom