Mh Lissu amekamatwa leo na yuko njiani analetwa Dar es salaam . Hatupaswi kuogopa , kwani aliyetupa masikio asiweze kusikia kilio na maombi yetu na dua kweli ? Aliyetupa macho mnafikiri haoni ? Aliyetupa akili na fikra asiweze kuwaza juu ya mambo haya ? Tunawakati mgumu katika kazi zetu za siasa kwa sasa , lakini ni wakati muhimu kuliko wakati wowote katika historia ya mfumo wa vyama vingi , ni tabu ya kutembea kwa miguu ndiyo iliyosababisha ugunduzi wa gari , ni giza ndio kilikuwa chanzo cha ugunduzi wa umeme duniani , na tabu ya kuvaa magome ya miti ndiyo iliyoleta mapinduzi ya nguo tunazovaa Duniani leo .
Tunahitaji wakati kama huu katika mahitaji yetu ya mabadiliko , wala msiingie hofu , kwa wale wakristo mnaelewa shetani asingempleka Yesu msalabani mpango wa Mungu kwenu usingetimia , tunapita katika mateso na huzuni kwa maana kubwa katika ustawi na historia ya Nchi yetu ,kila mmoja wetu anapaswa kuona kinachoendelea na kuchukua hatua ya kulaani na kulaumu na kuomba , hata hivyo baada ya giza nene asubuhi utokea.
Msiogope Mungu amekusudia mema kwetu na kwenu .
Aluta continua , Uchaguzi mkuu wa Nchi utakuaje kama leo uchaguzi wa TLS huna vikwazo hivi ? Sio Lissu aliyekamatwa na kuanza kuletwa Dar , bali ni haki , utu ndio vimekamatwa , na wewe na mimi ni ndugu wa haki na utu wa karibu , ni sote tumekamatwa . Amkeni , dhambi mbaya na kubwa kuliko zote Duniani ni Uoga.
Mungu awabariki .
Godbless J Lema ( MB)
Mhe. Godbless Lema, kwanza nikupe pole sana kwa kifungo cha miezi 4 bila hatia wala mashtaka. Pole sana.
Hii ndiyo Tanzania ya Magufuli, ni vurugu, ni unyama, ni udikteta, ni uhuni na ubabe uliopitiliza. Haya matukio ni mageni sana masikioni mwa watu wa Tanzania. Sielewi huyu Rais wa CCM A5 anataka Watanzania wafanye nini kwa haya mambo ya ajabu ajabu anayowafanyia Watanzania wenzake kana kwamba ni Makaburu!!
Nelson Mandela(RIP) pamoja na kufungwa na MAKABURU miaka 27 gerezani bado alikuja kuwa Rais wa SA na AKAWASAMEHE MAKABURU WOTE!!. Bado Nelson Mandela alipoanza kutawala nchi ya Afrika Kusini ALIWEZA KUWAACHIA IKULU CHAMA CHA UPINZANI KUKAIMU AKIWA ZIARANI NCHI ZA NJE!!! Je, Magufuli anaweza kufika hata 0.00001% ya UTU na UUNGWANA aliokuwa nao Marehemu Mandela???
Tanzania inapitia kipindi kigumu sana katika Historia tangu kuundwa kwake. Bahati ni kwamba Watz hawakupitia misukosuko ya vita vya kupigania Uhuru ndiyo maana hawana fujo za kijinga kutaka kujibu mapigo. Lakini Rais Magufuli lazima ajue kuwa ameshaanza kubadilisha mwelekeo na upepo kwa Watanzania. Asifikiri Watanzania ni Malaika walioshushwa kutoka Mbinguni. Watz nao ni wanadamu kama wanadamu wengine kama wa nchi za Rwanda, Burundi, Algeria, Misri, Libya, Yugoslavia n.k.
Kuna kitu Rais Magufuli anachokitafuta kwa Watanzania na iko siku inakuja atakipata. Naomba JPM ayakumbuke maneno ya Baba wa Taifa aliyoyatumia wakti wa kumng'oa mkolone bila kutumia bunduki yanayosema,''
TUMEONEWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMEPUUZWA KIASI CHA KUTOSHA,TUMENYONYWA KIASI CHA KUTOSHA. UNYONGE WETU NDIO ULIOTUFANYA TUONEWE, TUNYONYWE NA TUPUUZWE, SASA TUNASEMA BASI ''
Magufuli ameamua kuchezea HAKI, UTU na HESHIMA za Watanzania kwa kuamua KUWAONEA, KUWAPUUZA, KUWANYONYA na KUWANYANYASA kisa tu eti wapinzani. Kwanini Magufuli ameamua kuwafanya WATANZANIA WAISHI KAMA WAKIMBIZI NDANI YA NCHI YAO????Hii ni akili ya ajabu sana kuwahi kufanywa na mtu anayejiita Rais wa JMT. Sijajua kwa akili ya Magufuli kama Wapinzani ni maadui,wahaini au magaidi wanaotaka kupindua nchi!! Nchi hii ni ya Watanzania wote bila kujali wako chama gani, wana itikadi gani, wana dini gani, wana Elimu gani au wanatoka kabila gani. Lakini kwa Utawala huu rangi zote za Ubaguzi na Ukabila zimeanza kuonekana waziwazi. Ubaguzi wa kiitikadi/kichama uko wazi(rejea speech zake kwenye Mkutano Mkuu wa CCM juzi na alipoongea na Wabunge wa CCM.Ukija kwenye Ukabila usiseme, kwa sasa kila akitumbua mtu anayemteua ni Msukuma mwenzie. Angalia swala la RC Makonda, pamoja na USHAHIDI WA WATU WA MUNGU KUWA HUYU ALIGHUSHI VYETI MAGUFULI YUKO KIMYA anajifanya kama vile haoni au hayupo. This is double standard. Inasikitisha sana. Nimalize kwa kusema tu kwamba haya yote anayotufanyia Watanzania wawe Wapinzani, wawe Wanachuo waliokosa mikopo, Wafanyakazi ambao hawajapata madai yao kama WAALIMU na MADAKTARI, Watani zangu WAHAYA na TETEMEKO LA ARDHI, Mungu wa Mbinguni anaona huu UTAWALA MWOVU NA IKO SIKU ATAUPATILIZA KATIKA JINA LA YESU KRISTO.
Mwisho ni kuwa Wana CCM tunashauri mwambieni Mwenyekiti wenu na Rais wenu kuwa VISASI HAVIJENGI VIWANDA wala UMOJA WA KITAIFA. Anachofanya kwa sasa ni KUBOMOA NCHI NA KUSAMBARATISHA UMOJA,AMANI, MSHIKAMANO NA UPENDO TULIACHIWA NA WAASISI WA TAIFA HILI. Shame on him!!!