Godbless J Lema
Arusha MP
- Sep 28, 2013
- 92
- 2,205
Mh Lissu amekamatwa leo na yuko njiani analetwa Dar es salaam . Hatupaswi kuogopa , kwani aliyetupa masikio asiweze kusikia kilio na maombi yetu na dua kweli ? Aliyetupa macho mnafikiri haoni ? Aliyetupa akili na fikra asiweze kuwaza juu ya mambo haya ? Tunawakati mgumu katika kazi zetu za siasa kwa sasa , lakini ni wakati muhimu kuliko wakati wowote katika historia ya mfumo wa vyama vingi , ni tabu ya kutembea kwa miguu ndiyo iliyosababisha ugunduzi wa gari , ni giza ndio kilikuwa chanzo cha ugunduzi wa umeme duniani , na tabu ya kuvaa magome ya miti ndiyo iliyoleta mapinduzi ya nguo tunazovaa Duniani leo .
Tunahitaji wakati kama huu katika mahitaji yetu ya mabadiliko , wala msiingie hofu , kwa wale wakristo mnaelewa shetani asingempleka Yesu msalabani mpango wa Mungu kwenu usingetimia , tunapita katika mateso na huzuni kwa maana kubwa katika ustawi na historia ya Nchi yetu ,kila mmoja wetu anapaswa kuona kinachoendelea na kuchukua hatua ya kulaani na kulaumu na kuomba , hata hivyo baada ya giza nene asubuhi utokea.
Msiogope Mungu amekusudia mema kwetu na kwenu .
Aluta continua , Uchaguzi mkuu wa Nchi utakuaje kama leo uchaguzi wa TLS huna vikwazo hivi ? Sio Lissu aliyekamatwa na kuanza kuletwa Dar , bali ni haki , utu ndio vimekamatwa , na wewe na mimi ni ndugu wa haki na utu wa karibu , ni sote tumekamatwa . Amkeni , dhambi mbaya na kubwa kuliko zote Duniani ni Uoga.
Mungu awabariki .
Godbless J Lema ( MB)