Aliyetupa Macho asiweze kuona?

Aliyetupa Macho asiweze kuona?

Lema...Wakati mwingne mkiwa mnaandika UZI humu muwe mnafikiria mara mbili mbili kabla ya KUANDIKA especially kwa nyie ambao ni VIONGOZI....Mnatakiwa wakati mwingne muwe wa KWELI hili la LISSU kukamtwa leo KAJITENGENEZEA mwenyewe makusudi kuelekea huu UCHAGUZI wa TLS ili ionekane hili la yeye kukamtwa leo lina uhusiano na TLS......hamtaki kabsa kuangalia upande wa pili wa yeye kuvunja SHERIA.....

Mkuu, is this too good to be true???? Yaani mpaka unasema "Lissu kajitengenezea mwenyewe", kwa maana hata wewe huamini kama mtu anaweza kukamatwa siku moja au mbili kabla ya uchaguzi wa TLS? ni kweli unaamini hicho unachokisema au unajitoa ufahamu tu? Sijakuelewa vizuri..
 
Mh Lissu amekamatwa leo na yuko njiani analetwa Dar es salaam . Hatupaswi kuogopa , kwani aliyetupa masikio asiweze kusikia kilio na maombi yetu na dua kweli ? Aliyetupa macho mnafikiri haoni ? Aliyetupa akili na fikra asiweze kuwaza juu ya mambo haya ? Tunawakati mgumu katika kazi zetu za siasa kwa sasa , lakini ni wakati muhimu kuliko wakati wowote katika historia ya mfumo wa vyama vingi , ni tabu ya kutembea kwa miguu ndiyo iliyosababisha ugunduzi wa gari , ni giza ndio kilikuwa chanzo cha ugunduzi wa umeme duniani , na tabu ya kuvaa magome ya miti ndiyo iliyoleta mapinduzi ya nguo tunazovaa Duniani leo .

Tunahitaji wakati kama huu katika mahitaji yetu ya mabadiliko , wala msiingie hofu , kwa wale wakristo mnaelewa shetani asingempleka Yesu msalabani mpango wa Mungu kwenu usingetimia , tunapita katika mateso na huzuni kwa maana kubwa katika ustawi na historia ya Nchi yetu ,kila mmoja wetu anapaswa kuona kinachoendelea na kuchukua hatua ya kulaani na kulaumu na kuomba , hata hivyo baada ya giza nene asubuhi utokea.
Msiogope Mungu amekusudia mema kwetu na kwenu .

Aluta continua , Uchaguzi mkuu wa Nchi utakuaje kama leo uchaguzi wa TLS huna vikwazo hivi ? Sio Lissu aliyekamatwa na kuanza kuletwa Dar , bali ni haki , utu ndio vimekamatwa , na wewe na mimi ni ndugu wa haki na utu wa karibu , ni sote tumekamatwa . Amkeni , dhambi mbaya na kubwa kuliko zote Duniani ni Uoga.

Mungu awabariki .

Godbless J Lema ( MB)
Karibu sana jukwaani kamanda .
 
Napata shida sana kujua m uwezo wa kujenga hoja kwa wapinzan wa TZ. Nkisema CCM itaendelea kuwa chama pendwa kwa WaTZ walio wengi ntakuwa sijakosea kabisa.
Kwa kulazimisha sawa. Haya yote yanafanyika kukilinda.
Mh naomba kutoa maoni yangu...Wakati campaigns za mitandaoni ziliendelea,nilikuwa nashauri watu wajikite vijijini kupiga campaigns,kama issue ni pesa,wananchi tuko tayari kuchangia,ili mradi tu kampeni zifanikiwe (ikiwezekana nyumba kwa nyumba)tukiamsha ari ya watu kukichukia chama tawala,tunaweza kufanikiwa kuleta mabadiliko mbeleni,

Japo kwa muono wangu,2020 Lowassa agombee tena coz mkifanya kosa mkamuweka mtu mwingine tofauti na Lowassa,huyo mtu hata kama ana nguvu kiasi gani akiukosa urais hiyo 2020 atakuwa amekufa kisiasa...nashauri mkae mezani na ZZK muwe kitu kimoja then by 2025 tumtumie kama hazina kwenye uchaguzi mkuu...

My point here ni kuhakikisha angalau mwaka 2020 idadi ya wabunge wa CCM na Upinzani either inakuwa sawa au Upinzani wanakuwa wengi,hii itasaidia kurudisha hadhi ya bunge kwa kulifanya kuwa muhimili wa dola unaojitegemea tofauti na hali ilivyo sasa
 
Î
Godbless unaandika mengi unaishia kujichanganya, naamini unafahamu unajichanganya ila kwa vile unawajua wajinga unaowaandikia ambao watakipenda na kukishangilia ulichoandika umeamua uandike hivyo hivyo kwani unawadharau. Kama unasema hiyo hali iliyopo ni mpango wa Mungu kama ilivyokuwa kusulubiwa kwake Yesu kwa nini tena utake watu walaani? Unataka watu walaani mipango ya Mungu? Kama uliandika pasipo kufahamu basi ujinga huo haumithiliki

Lema anawaandikia wasiojielewa. Kwani umeshamwona mtu anapeleka mwanga kwenye mwanga? unless huyo mtu ni mbumbumbu sana. Watch out! usije kuwa unajaribu kujificha kwenye kona ile ile...
 
Utajifariji bila mafanikio, dhambi na haki ni vitu mbalimbali. Huwezi kumtabilia Rais kifo ukasamehewa kirahisi rahisi tu.
 
Mh naomba kutoa maoni yangu...Wakati campaigns za mitandaoni ziliendelea,nilikuwa nashauri watu wajikite vijijini kupiga campaigns,kama issue ni pesa,wananchi tuko tayari kuchangia,ili mradi tu kampeni zifanikiwe (ikiwezekana nyumba kwa nyumba)tukiamsha ari ya watu kukichukia chama tawala,tunaweza kufanikiwa kuleta mabadiliko mbeleni,

Japo kwa muono wangu,2020 Lowassa agombee tena coz mkifanya kosa mkamuweka mtu mwingine tofauti na Lowassa,huyo mtu hata kama ana nguvu kiasi gani akiukosa urais hiyo 2020 atakuwa amekufa kisiasa...nashauri mkae mezani na ZZK muwe kitu kimoja then by 2025 tumtumie kama hazina kwenye uchaguzi mkuu...

My point here ni kuhakikisha angalau mwaka 2020 idadi ya wabunge wa CCM na Upinzani either inakuwa sawa au Upinzani wanakuwa wengi,hii itasaidia kurudisha hadhi ya bunge kwa kulifanya kuwa muhimili wa dola unaojitegemea tofauti na hali ilivyo sasa
Jinga lingine, wananchi wapi unawasemea yaani hamchangishi pesa watoto wa maskini waliokosa mikopo wasome mnataka tuchangie pesa Lema na Lissu akapalilie kitambi mbumbumbuuuu
 
Lema...Wakati mwingne mkiwa mnaandika UZI humu muwe mnafikiria mara mbili mbili kabla ya KUANDIKA especially kwa nyie ambao ni VIONGOZI....Mnatakiwa wakati mwingne muwe wa KWELI hili la LISSU kukamtwa leo KAJITENGENEZEA mwenyewe makusudi kuelekea huu UCHAGUZI wa TLS ili ionekane hili la yeye kukamtwa leo lina uhusiano na TLS......hamtaki kabsa kuangalia upande wa pili wa yeye kuvunja SHERIA.....

Mtafute Lemutuz ndio mna akili sawa sawa
 
Lema anawaandikia wasiojielewa. Kwani umeshamwona mtu anapeleka mwanga kwenye mwanga? unless huyo mtu ni mbumbumbu sana. Watch out! usije kuwa unajaribu kujificha kwenye kona ile ile...

Kama amekuandikia wewe hongera yenu, amewafundisha neno bora kabisa, kukilaani kilicholetwa na Mungu, kuilaani mipango ya Mungu. Kweli mwenye giza amepeleka mwanga wa kiza kwa walio kwenye kiza totoro ! Mradi mnaelewana hakuna shida
 
Mh naomba kutoa maoni yangu...Wakati campaigns za mitandaoni ziliendelea,nilikuwa nashauri watu wajikite vijijini kupiga campaigns,kama issue ni pesa,wananchi tuko tayari kuchangia,ili mradi tu kampeni zifanikiwe (ikiwezekana nyumba kwa nyumba)tukiamsha ari ya tawalwatu kukichukia chama tawala,tunaweza kufanikiwa kuleta mabadiliko mbeleni,

Japo kwa muono wangu,2020 Lowassa agombee tena coz mkifanya kosa mkamuweka mtu mwingine tofauti na Lowassa,huyo mtu hata kama ana nguvu kiasi gani akiukosa urais hiyo 2020 atakuwa amekufa kisiasa...nashauri mkae mezani na ZZK muwe kitu kimoja then by 2025 tumtumie kama hazina kwenye uchaguzi mkuu...

My point here ni kuhakikisha angalau mwaka 2020 idadi ya wabunge wa CCM na Upinzani either inakuwa sawa au Upinzani wanakuwa wengi,hii itasaidia kurudisha hadhi ya bunge kwa kulifanya kuwa muhimili wa dola unaojitegemea tofauti na hali ilivyo sasa

Viongozi wa vyama vya upinzani muda umefika sasa wa kupanga mikakati na kuimarisha upinzani.
Chama tawala kinawaaribia mikakati kidiplomasia .
msipostuka mtakuta uchaguzi huo na nyie hamjajipanga.
Nafikiria sasa ni wakati muafaka wakuanza kupanga mikakati ya chaguzi zijazo.
Mfano mzuri wa chaguzi zilizopita chama tawala wameshinda vizuri kwasababu ya vyama vya upinzani kujikita kwenye kushughulikia matatizo.
Wananchi wanaopiga kura sio wote wanaweza kuona mnayolalamikia yana impact gani kwa sasa au kwa baadae.
Rudini kimkakati zaidi mrudishe imani zenu kwa wananchi kwa makosa yanayotokea sasa kwenye serikali.
Wawepo wa kuangaika na kesi pia mikakati ya kidplomasia iwepo ili walau msihue upinzani.
Wengine hatuna vyama lakini tunapenda kuona Demokrasia ya kweli inatawala Tz.
Mnyika,Zitto,Lema na wengineo tunakosa mengi mazuri kutoka kwenu badilikeni kutokana na mazingira muokoe jahazi la upinzani.
Mmefanya mengi kipindi cha Comredi Slaa njooni na mikakati ya kidplomasia wakati ndio huu.
 
Kama amekuandikia wewe hongera yenu, amewafundisha neno bora kabisa, kukilaani kilicholetwa na Mungu, kuilaani mipango ya Mungu. Kweli mwenye giza amepeleka mwanga wa kiza kwa walio kwenye kiza totoro ! Mradi mnaelewana hakuna shida

I wouldn't argue more...Ni kweli unachosema, unaonekana uko smart sana tu. Mnaopenda kusifiwa kwa kila kitu dawa yenu ni kuwasifia tu.
 
siku hizi Lema anajifungia chumbani kwake na kutuma post huku Jf....kiherehere cha maandamano na vurugu chote kwisha

c_x2z6pVP_I-640x350.jpg
 
Mkuu, is this too good to be true???? Yaani mpaka unasema "Lissu kajitengenezea mwenyewe", kwa maana hata wewe huamini kama mtu anaweza kukamatwa siku moja au mbili kabla ya uchaguzi wa TLS? ni kweli unaamini hicho unachokisema au unajitoa ufahamu tu? Sijakuelewa vizuri..

Huwezi kuelewa kwani unategemea mpaka uelezwe, udanganywe ndipo unapojidai kuelewa. Unachangia masikini bila hata kutaka kujua kwa nini Lisu kakamatwa. Wewe akikamatwa Lisu hata kama akikutwa anabaka wewe umekaririshwa tu Lisu anaonewa
 
Neno la Mungu lasema "Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia"
 
Back
Top Bottom