Aliyepigana Vita vya Kagera, Afariki Dunia kwa kung'atwa na nyuki

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Dodoma. Shujaa wa vita vya Kagera, Abinael Chikataa (71) amefariki dunia kwa kung'atwa na nyuki akiwa katika sherehe ya kuogesha wajukuu wake waliokuwa wamefanyiwa tohara.

Tukio hilo lilitokea Julai 15, mwaka huu katika Mtaa wa Kikuyu Kusini, jijini hapa na nyuki hao walikuwa kwenye mti, lakini walichokozwa na watoto kwa kupigwa mawe.

Chikataa alishiriki vita ya Kagera mwaka 1978, amewahi kufanya kazi ya ulinzi Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na mwaka 2012 alistaafu kazi hiyo na kuendelea na shughuli zake binafsi akiwa mjumbe wa Serikali ya mtaa.

Akisimulia tukio hilo, Elbeneza Simkoko alisema baada ya watoto kuwarushia mawe nyuki hao, walianza kumshambulia Chikataa aliyekuwa jirani na mti huo. Sikomkoko ambaye ni jirani alisema Chikataa alikuwa nje
ya nyumba yake akiwaogesha wajukuu zake baada ya kufanyiwa tohara na nyuki hao hawakuwa na muda mrefu eneo hilo kwa kuwa walipita na kutua kwenye mti.

Alisema baada ya kuumwa na nyuki zilifanyika jitihada za kuokoa maisha yake na wakati anafikishwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, ilibainika ameshapoteza maisha.

Mtaalamu wa tiba za binadamu wa Hospitali ya Matovolwa, Dk Ernest Ishengoma alisema kung'atwa na nyuki kunaweza kukahitaji huduma ya kwanza kwa haraka kama mgonjwa hatakuwa na shida yoyote hasa sumu ya nyuki.

"Utamjuaje kama ana aleji na nyuki? Ni pale utakapomuona aliyeng'atwa na nyuki akivimba mwili kwa haraka na anaweza pia kupoteza fahamu.

"Lakini hali hizi zinategemea ni kiasi gani cha nyuki wamemng'ata mtu, wakiwa wengi ni hatari na mhusika anatakiwa kukimbizwa hospitalini au kituo cha afya kilicho jirani," alisema Dk Ishengoma.

Daktari wa tiba kwa kutumia nyuki na mazao yake kutoka kampuni ya Tanzania International Bee Ltd, Dk Musiba Paul alisema licha ya nyuki kusababisha kifo, sumu yake ni zao linalotumika kutibu magonjwa mengi yanayosababishwa na bakteria, fangasi, virusi pamoja na kuondoa maumivu ya mwili.

"Tafiti nyingi duniani zimeonyesha matibabu kupitia mazao haya ya nyuki yameleta matokeo mazuri katika kutibu saratani na kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi, tafiti bado zinaendelea," alisema Dk Musiba." Akimzungumzia marehemu, Chifu wa Mkoa wa Dodoma, Henry Mazengo II alisema marehemu alikuwa mwadilifu na alisimama kidete kutetea maovu ndani na hakuwahi kusikia kama alikuwa na shida nyingine.​
 
Dunia ina mambo
main-qimg-e60f11f9282b702389c1700bddc6c337-lq.jpg
 
Itakua kilichowaokoa wajukuu wa kamanda,ni vimo vyao na mbio.
 
Mazali kama haya yakuvamiwa na kung'atwa na nyuki natamani sana yanitokee. Yani nitatembeza mkono balaa.
 
Back
Top Bottom