Aliyemshauri Rais Samia kuingia katika soka la Bongo kwa kununua magoli ana akili nzuri sana!

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,651
5,126
Mchezo wa soka (mpira wa miguu) ni mchezo unaopendwa na watu wengi sana Duniani. Kwa hapa Bongo ni kama ndo epicenter ya soka! Soka linapendwa hapa Bongo balaa!

Kuna wakati niliwahi kumwambia rafiki yangu mmoja kwamba kwa "uwazimu" huu wa upenzi wa soka hapa Tanzania hasa katika mechi za Simba na Yanga kuna siku nyumba zao na wake zao watavamiwa kama kwenye ile movie ya Acalipto ya Jaguar iliyotengenezwa na Bingwa wa filamu za Hollywood Mel Gibson.

Maana wakati wa hizo mechi wanaume wanaobaki ndani ni wa kuhesabu.

Sasa Rais Dr. Samia kuingia kwa kununua magoli katika mechi zinazochezwa na timu zetu kimataifa ni motisha kubwa sana kwa wachezaji na wapenzi wa soka.

Kwa taarifa tu ni kwamba promotion anayopata Rais Dr. Samia kwa kujitolea kununua hayo magoli ni kubwa na yenye thamani kubwa mno.

Hongera sana Mama kwa ubunifu huo.
 
download.jpeg
 
Labda kama safari hii kutakuwa na matokeo mazuri maana katika wanasiasa walojitokeza kujishughulisha na michezo hata JPM alijaribu kuihamasisha simu yetu na ikaishia wote twafahamu.

Mzee Mwinyi nae akawa ajitahidi kwenda uwanjani na kuna siku akasema timu yetu isiwe "kichwa cha mwendawazimu ambacho kila mtu ajifunzia kunyoa."

Soka wenzetu waanzia chini kwenye vitalu kisha kufika juu.

Tujifunze kutoka Morocco walitumia mbinu gani hadi timu imefika robo fainali za kombe la dunia.
 
Katika suala hili ama hakika Mama amekuja na kitu kipya chenye kuchochea hamasa na motisha kwa wachezaji katika mashindano ya kimataifa. Kongole nyingi sana ziende kwake.
 
samia hajaingia kwa kununua magoli tu,kafanya haya pia:
1. Anajenga viwanja vta michezo
2. Anamlipa kocha
3. Kawapa viwanja wachezaji soka wanawake
4. Kasaidia sana soka la walemavu
 
Dr Samia, sina la kujazia amefit katika kila sekta, uchumi 100%, Maendeleo 100% Michezo 100%, hapo kitambo ungekuta timu zimesha kalishwa au kutolewa kitambo mno.
HONGERA RAIS WETU KILA SEKTA SAFI.
N. B-Yapo makundi watakaokuwa wanaumia kweli kwa mafanikio haya ya kila sekta.
 
Unanunua magoli huku shule hazina waalimu hospitali hazina vifaa Tiba Wala madaktari na wauguzi wa kutosha.

Wanafunzi hawana mikopo Wala vijana hawana ajira.

Hakuna maji Wala umeme wa uhakika.

Miradi ya kimkakati inasuasua.

Kweli ni akili kubwa hiyo.
 
no hard feelings lakini ni moja ya mchezo ambao nauchukia sana

vijana na wazee wamekua wa ovyo sana kwa ulevi wa betting
mchezo huu una hasara nyingi kuliko faida

pesa badala ya kupelekwa kwenye miradi yenye tija na maendeleo, zinaenda teketezwa kwenye ujinga ujinga na upumbavu
 
Unanunua magoli huku shule hazina waalimu hospitali hazina vifaa Tiba Wala madaktari na wauguzi wa kutosha.

Wanafunzi hawana mikopo Wala vijana hawana ajira.

Hakuna maji Wala umeme wa uhakika.

Miradi ya kimkakati inasuasua.

Kweli ni akili kubwa hiyo.
Sukuma Gang wewe twakufahamu, hujawahi mponda Mwendazake na kila siku ulimtetea na kutukana wapinzani lakini inapokuja kwa mama DrSamia ambaye pia ni ccm unamponda.
 
Sukuma Gang wewe twakufahamu, hujawahi mponda Mwendazake na kila siku ulimtetea na kutukana wapinzani lakini inapokuja kwa mama DrSamia ambaye pia ni ccm unamponda.
Kwani nilichokiandika hapo hakina ukweli??
 
Unanunua magoli huku shule hazina waalimu hospitali hazina vifaa Tiba Wala madaktari na wauguzi wa kutosha.

Wanafunzi hawana mikopo Wala vijana hawana ajira.

Hakuna maji Wala umeme wa uhakika.

Miradi ya kimkakati inasuasua.

Kweli ni akili kubwa hiyo.
Acha kuwa na mawazo finyu kila sekta inahitaji maendeleo ikiwamo soka, ulishawaza hii nchi ikiwa na vijana hata 50 wanaocheza soka la kulipwa kwenye ligi kubwa duniani na kulipwa mapesa mengi, huoni watawekeza nyumbani kwa kuzalisha ajira nyingi na hata kujenga mahospitali kama alivyofanya Sadio Mane kule Senegal?

Mmekalia roho mbaya na chuki dhidi ya Mama kiasi mnakosa kuona mema na kusema uongo.
 
Kwenye mikopo muache
 
Sasa unafikiri kununua magoli ndio njia ya kupeleka watu ulaya kuchezea soka ya kulipwa.

Tatizo kila mtu akishika tu smart phone naye anajiona smart.
 
Hana akili zozote we umesikia nchi gani rais anatangaza madau. Ni bora hata yule aliyewapa wachezaji viwanja kama motisha.

Kinachowafanya wafocus na mpira ni kwa sababu wameshindwa kuongoza nchi na wameona watu wengi macho na masikio ni kwenye soka.

Watu wengi wanafocusa kwenye soka kama njia ya kujisahaulisha na machungu ya maisha. Ukiangalia mashabiki wengi wanatokea maeneo ya mbagala, mbande, tandale, manzese na maeneo au mikoa mingine ambayo ina changamoto zaidi kimaisha.

Kwa maana nyingine serikali ya samia imeamua kufanya soka kama siasa, ni kichaka cha kufichia kelele za wananchi. Bahati mbaya watanzania hawajagundua hili.
 
Nje ya mada, hivi raisi wa urusi Vladimir Putin akiamua kuitembelea Tanzania hivi karibuni SI tutaanza kuharisha jamani?! Maana tutalazimika kutekeleza wajibu wetu Kwa ICC... Hapa nmepotea jukwaa
 
Dr Samia, sina la kujazia amefit katika kila sekta, uchumi 100%, Maendeleo 100% Michezo 100%, hapo kitambo ungekuta timu zimesha kalishwa au kutolewa kitambo mno.
HONGERA RAIS WETU KILA SEKTA SAFI.
N. B-Yapo makundi watakaokuwa wanaumia kweli kwa mafanikio haya ya kila sekta.

IMG_2756.jpg
 
Kufanya hivyo peke yake haitoshi mpira ni ajira na ni pesa pia hivyo uwekezaji wa maana unahitaji kufanyika ili kupata matunda yenye kustahili anachokifanya hakina tija sana kwenye soka letu zaidi ya kuwapa hamasa ya kushinda mechi mbili tatu halafu tunarudi kusema tumejitahidi. Hakuna nia ya dhati kuwekeza kwenye mpira na michezo mingine motisha (incentives) inapaswa kutolewa kwa watt/taasisi zinazoamua kuwekeza kwenye mpira na michezo mingine kama kufungua academis, kutengeneza viwanja vya michezo nk
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom