Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,746
- 218,335
Ni dhahiri sasa kwamba Mh Rais alidanganywa na kuambiwa mambo ya uongo , kwamba kabla ya kukamatwa Mbowe alikimbilia nje ya Nchi baada ya kupata taarifa kuwa miongoni mwa watuhumiwa kwenye kesi hii wamekwishahukumiwa kifungo jela baada ya kukiri makosa yao ya Ugaidi .
Mh Rais alitoa kauli hii hadharani tena kwa kujiamini kabisa , Alipokuwa anahojiwa na BBC ambalo ni shirika la Utangazaji la kimataifa, maana yake ni kwamba habari yake hiyo ilisikika Duniani mote .
Bali sasa ni dhahiri shahili kwamba kauli ile haikuwa ya kweli baada ya Mpelelezi Mkuu na nguli wa kesi hii mwenye uzoefu wa miaka zaidi ya 20 kwenye kitengo hicho , aliyesomea Botswana , Inspector Tumaini Swilla kukanusha jambo hilo Mahakamani mbele ya Mtukufu Jaji Tiganga , Swilla akijibu swali la Wakili wa Utetezi Kibatala , ameiambia mahakama kwamba Watuhumiwa wa Ugaidi wako wanne na ni ambao wameshitakiwa Mahakamani na wala hakuna mwingine yoyote aliyefungwa miongoni mwao .
Kwa kufupisha : Ni nani alimdanganya Mh Rais kuhusu jambo hili kiasi cha kumdhalilisha mbele ya jamii ? je anastahili kuendelea kubaki ofisini , na kwanini asikamatwe na kushitakiwa kwa kumdanganya Rais?
Pia, soma: Rais Samia: Mashtaka dhidi ya Mbowe sidhani kama yamechochewa kisiasa