Kuna watu wanamshangaa Polepole kwa kufanya yote aliyoyafanya akiwa hapa hapa Tanzania, wanaona kama alikosea. Hii nchi ni ya watanzania na Polepole ni mtanzania, mlitaka aende nchi gani?
Video yake ya jana alisema kuna wazee wameshasaliti na wanaorodhesha watu watakaoshiriki maridiano. Binafsi naamini hao hao wazee ndio wamemchomolea betri; wazee aliowaamini wamemchoma ndugu Polepole
Cha kusikitisha sana ni namna sisi watanzania tunavyo react kwa matukio kama haya
Leo ilikuwa ilikuwa siku nzuri sana ya kuliamsha dude. Starting point ambayo inatafutwa siku zote ilikuwa imepatikana leo asubuhi. Nitatoa sababu zifuatazo;
Leo ilikuwa kesi ya Tundu Lisu, kesi ambayo inakusanya umati mkubwa wa watu. Watu wamepigwa, wameumizwa, wamevunjwa miguu na wengine wako mahututi hospitali
Yote hayo yamefanyika machoni pa viongozI wa CHADEMA! Wakati huo huo tumeamka na taarifa za kutekwa kwa Polepole.
Unabaki unajiuliza, ingekuwa kwa wenzetu hapo jirani tu Kenya, hii haikutosha kuwa starting point?
Yaani tumeamka asubuhi na habari za mshituko na masikitiko za kutekwa kwa Polepole, halafu watu wanapigwa virungu na polisi mahakamani, halafu kuna vijana kibao wamekamatwa mikoa tofauti tofauti...polisi anapomgusa raia na kumpiga virungu, kwanini vagi lisianzie hapo hapo kushinikiza Polepole apatikane, waliokamatwa waachiliwe, kuhoji kwanini imekuwa kawaida polisi kuwapiga raia, tunasubiri tupate sababu gani?
Mimi nakumbuka wakati tunasoma, tuliwahi kurundika hasira mioyoni kwa uonevu mbalimbali tuliyofanyiwa na walimu lakini yalikuja kudhihirika siku ambayo uji uliwekwa sukari kidogo.
Tuligoma kunywa uji kwasababu ya kudai sukari haitoshi, walipoleta sukari ili iongezwe sukari ilimwagwa na madai yakabadilika yakahamia kwenye uonevu wa walimu, baadaye madai yakageuka kwenda kwa Mkuu wa shule, baadaye mawe yakaanza kurindima kuelekea majengo ya ofisi na nyumba za walimu walengwa
Walimu wakakimbia, vikao vikafanyikia wanapojua wao, hadi kufikia mchana shule ilitawaliwa na wanafunzi. Yote haya yalitokea siku hiyo bila kupangwa na yeyote. Hakuna wanafunzi walikaa wakakubaliana eti siku fulani tugome kunywa uji, No! Ni kwamba watu walianzisha minong'ono tu kuwa ooh sukari haitoshi, ooh kwanini sukari haitoshi...watu wakaitikia kweli sukari haitoshi sukari haitoshi...baada ya hapo kilichotokea hakuna aliyeamini
Aliyekuja kuwatuliza wanafunzi ni mwalimu mmoja aliyekuwa anaheshimika japo na yeye alifanya timing; kusubiri joto lishuke kwanza
Starting point huwa haipangwi bali inatokea automatically. Ndiomaana nawashangaa wanaosema octoba 29 sijui wataandamana, mara watatoka, hakuna kitu hapo. Leo ilikuwa ni golden chance!