Aliyeishuhudia ajali iliyoua dereva bodaboda Goba saa 1 usiku (8-6-2021), tufahamishe ilivyokuwa

2014
Nilikuwa nazo 5 kmr MWISHO
Jun nikapigiwa simu mdogowako ANAKUJA DAR MSAIDIE PIKPIK moja aendeshe (mtotowamamdogo)

26 Sept napigiwa simu kapata ajali hatunae Tena...(3 months only)

NILIRUDI nikazikusanya nkatangaza Sana fb na jf thx that guy wa jf aliezichukua zote nilikuwa nikiona pik NAHISI israel anakuja

#mpakaleooomamamdgo haongei na mm
Nishidaa

Kiufupi kama huna haraka panda. Basi
Wengi hawana hata leseni

Bodaboda sipandi kwenye lami hata siku moja,natumia nje ya mji tu na porini kwenye shughuli zangu za kukata mkaa,hata niwe na haraka gani sipandi bodaboda mjini,mama mdogo ana haki ya kutoongea na wewe kabisa maana wewe ndio chanzo cha mwanae kufariki ila kaa nae chini na familia mmalize tofauti ingawa ulikuwa na lengo jema.

Kuna jamaa ni fundi mwenzangu ujenzi namtumia kama kibarua(saidia fundi) ,kumbe wakati anajenga alikuwa anakusanya fedha ya kiingilio ya kuchukua bodaboda za mkopo kwa wahindi,alivyotimiza laki akenda kuchukua boxer ya mkataba kwa muhindi,jamaa hajui hata kuendesha baada ya siku moja akaanza kuchukua abiria ,siku kama hakuna mishe za ujenzi anakuwa bodaboda siku akiwa na mishe anampa deiwaka bodaboda mwengine.....Ni full "lena" hana control lakini anabeba abiria ,hana hata leseni.....Madada wanapenda sana kupanda bodaboda.
 
Msiwe wepesi wa kuhukumu, kuna watu wana roho nyepesi mno hawawez kabisa kuangalia ajali hasa ya mtu aliyeumia kama hivyo mana inawaathiri kisaikolojia.Mtu unaweza kukuta mwezi mzima na zaidi hilo tukio la ajali halijamtoka kichwani na linamdisturb vibaya

Sent from my SM-G900I using JamiiForums mobile app
Yaap ni kweli kabisa. Licha ya kushuhudia live kwa macho ,pia hata kuangalia kwenye video ajali au mauaji ya kikatili . Lazima uwe disturbed... Ndio wanasaikolojia wanasema hali hiyo huitwa post traumatic stress disorder nadhani
 
Kwa jinsi Dereva ' Bodaboda ' alivyokuwa kaumia vibaya Kichwani na Kuburuzwa nilishindwa Kujizuia na Kusikitika sana tu na kujikuta nakimbia ( natoka Baru ) eneo la Tukio kwa Kiwewe.

Najua ( Huenda ) Tukio lile lilishuhudiwa na mwana JamiiForums mwingine hivyo naomba asimulie hali nzima ilivyokuwa. Ni Ajali iliyotokea Goba Saa 1 Usiku wa leo Jumanne.

Jamani Wadogo zetu na Kaka zetu mnaoendesha hizi ' Bodaboda ' hasa ' Kibiashara ' jioneeni Huruma jinsi mnavyokufa na kulemazwa hovyo kwa Ajali za Barabarani kwa Kuendesha kwa Nidhamu, kuwa Makini na kufuata sana Sheria. Taifa linawahitaji mno tu.
Ajali humkuta hata mwenye tahadhari
 
nilikuwepo inatisha sana maana mdau alikua anatoka damu puani na mdomoni kwa kifupi amekufa kwa mateso sana mpaka inasikitisha aise na inasemekana alianguka mwenyewe bila kuguswa na gari yeyote.
Asante kwa Ufafanuzi wako huu ila unaposema alianguka tu Mwenyewe pale inaoneka aligongwa na Gari iliyokimbia, ikamburuta vibaya hadi ' Helmet ' nayo ikamtoka na hata Vioo vilivyopasuka vilionekana nashindwa Kukuelewa. Na Marehemu alionekana Kapasuka Kichwani na alikuwa ni pande la Mtu ( Mnene ) hivi.
 
2014
Nilikuwa nazo 5 kmr MWISHO
Jun nikapigiwa simu mdogowako ANAKUJA DAR MSAIDIE PIKPIK moja aendeshe (mtotowamamdogo)

26 Sept napigiwa simu kapata ajali hatunae Tena...(3 months only)

NILIRUDI nikazikusanya nkatangaza Sana fb na jf thx that guy wa jf aliezichukua zote nilikuwa nikiona pik NAHISI israel anakuja

#mpakaleooomamamdgo haongei na mm
Nishidaa

Kiufupi kama huna haraka panda. Basi
Wengi hawana hata leseni
Pole sana, ila funzo hutakiwi kumpa kazi ya bodaboda nduguyo.
 
Jinsi wanavyoendesha hizo pikipiki, walio wengi hawajali maisha yao hata huwa sina haja ya kuwasikitikia. Maana wao wenyewe hawajijali na kujisikitikia
Kuna Mmoja mwaka Juzi niko Tegeta Masaiti akanipita kwa Spidi Kali huku akiwa anafanya Mbwembwe ( Mikogo ) yake mbele kidogo akakutana uso kwa uso na IST kwa Hasira niliyokuwa nayo dhidi yake na ukizingatia hata Nauli ya ninakokwenda ilikuwa haijatimia nilipomkuta katupwa Mtaroni akiwa anakaribia kuiacha Dunia wala sikuhangaika nae sana nilimsachi Mfukoni nakukuta ana ' Jero ' tu Pumbavu yule na ' Condoms ' kama Mbili ambazo ' nilizikomba ' zote na kumuacha pale pale ila Simu yake nzuri sikumchukulia kwani shida yangu ilikuwa ni hiyo Nauli tu na zile ' Condoms ' nilizozibahatisha Kumkuta nazo.
 
Bodaboda wasipo tuliza wenge barabarani watapasuliwa sana!! Most of them ni wapuuzi na hawajui sheria na hawana nidhamu wakiwa barabarani....Itoshe kusema wapasuliwe tu maana hakuna namna kwa madereva wazembe.
Hivi ni kwanini huwa hawasikii tu hawa?
 
kuna dogo pia hapa mtaani leo nimeletewa daftari la michango,maskini ni mdogo sana hata 25 hajafika.amekutana na fuso ikapita nae!yaani nimesikitika kwa maelezo ya wenzie ni kwamba fuso ilimpanda kabisa miguuni hivyo mguu mmoja kuanzia kwenye paja umekatwa!!😣huo mwingine una afadhali
Jamani tuwasaidie vipi hawa Bodaboda?
 
Pole kwa walioguswa, ila wale vijana wanavyoendesha vibaya Mungu atusamehe kwa tunayowatakia, nina orodha ndefu ya ndugu, rafiki na jamaa waliogongwa au kung'olewa side mirrors na hao boda isiyoisha ikiwepo yangu ya kimaskini, tatizo nafikiri ni zile bangi na pombe za haraka haraka vijiweni, bado matusi watakayokushambulia wakikataa kata hawana makosa, ni tabu kabisa aise
Mkuu Bangi si mbaya kama ukiiheshimu.
 
Back
Top Bottom