Aliyekanyagwa na lori aishi kwa kukinga haja kubwa tumboni

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Wahenga walisema hujafa hujaumbika. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Supa Ngussi aliyepata changamoto katika sehemu ya kutolea haja kubwa na ndogo, baada ya kupata ajali ambayo ilikwenda kubadili kabisa mwelekeo wa maisha yake.

Ngussi (21) ni baba wa mtoto mmoja, alipata changamoto hiyo katika sehemu za kutolea haja, Septemba 27, 2021 baada ya kupata ajali maeneo ya Ubungo External na baadaye kulazimika kutumia mipira kutolea haja kubwa na ndogo.

Hata hivyo, kutokana na kushindwa kumudu gharama za kununua mirija ya haja kubwa, anasema wakati mwingine hulazimika kutumia kitambaa kukinga haja kubwa inapotokea.

Kabla ya hapo Ngussi alikuwa ndio tegemeo kwa familia yake, mke pamoja na mtoto ambaye kwa sasa ana umri wa miaka miwili na miezi saba.

Kupitia kazi yake ya udereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda, alijipatia kipato kuhakikisha familia yake inapata mahitaji yote ya muhimu wakiishi kwenye nyumba ya kupanga jijini hapa.

Mwananchi lilifika katika nyumba anayoishi kijana huyo maeneo ya Tabata Kimanga, ambapo Ngussi alieleza kuwa ajali hiyo imemfanya kuwa tegemezi hali iliyosababisha hata mkewe kumkimbia.

Ajali ilivyokuwa
Anasimulia kuwa Septemba 27, 2021 saa 9 usiku akiwa anatokea Kibo baada ya kushusha abiria akielekea Tabata Kimanga, alipofika eneo la Riverside aligongwa na lori la kubeba mafuta na hivyo kuvunjika mguu wa kulia na kuumia maeneo ya kiuno kiasi cha kusababisha kushindwa kutoa haja zote mwenyewe.

“Niligongwa na lori la mafuta na kunirusha hadi pembezoni mwa barabara, wakati watu wanataka kusogea kunisaidia gari hilo lilirudi tena kwa mwendo kasi hali iliyowafanya watu hao kukimbia na kunikanyaga tena maeneo ya kiuno, ni ajali mbaya ambayo sitaweza kuisahau,” alieleza Ngussi huku machozi yakimlengalenga.

Anasema baada ya ajali dereva alikimbia lakini watu waliokuwa katika eneo la tukio walimsaidia kupiga simu kwa ndugu kisha akapelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

“Nilipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo awali nililazwa ICU (chumba cha uangalizi maalum) kwa takribani wiki moja nikiwa sina fahamu.

“Baada ya kupata fahamu na kuanza kupata afueni nilihamishiwa wodini ambapo nililazwa tangu Septemba 2021 hadi Januari 11 mwaka huu baada ya kuruhusiwa na nikashauriwa niwe nahudhuria kliniki,” alisema.

Anasema gharama za matibabu alizopatiwa katika kipindi chote alichokuwa hospitali ilikuwa Sh4 milioni lakini kwa kipindi alichokuwa anaruhusiwa hospitali alifanikiwa kulipa Sh250,000 pekee ambayo ilipatikana kwa kuchangiwa na ndugu, jamaa na marafiki pamoja na mama na mjomba yake kuuza mashamba waliyokuwa wakimiliki, hivyo bado ana deni la Sh3 milioni ambalo ameshindwa kulilipa hadi sasa.

“Niliruhisiwa kutoka hospitali kwa makubaliano ya kuendelea kulipa deni taratibu, lakini kutokana na hali yangu na maumivu makali ninayopitia nashindwa kuendelea kulipa deni hilo kutokana na kushindwa kufanya kazi au shughuli yoyote ya kujipatia kipato,” alisema.

Baada ya kuruhusiwa
Kutokana na kushindwa kuendelea kumudu gharama za matibabu zaidi na kuhudhuria kliniki, anasema alichukua uamuzi wa kurudi mkoani kwao Iringa akisubiri kudra za Mungu.

“Nilirudishwa kijijini nikiwa bado sijiwezi hata kutembea maisha yaliendelea hivyo huku nikiendelea kutumia dawa nikaanza kufanya mazoezi kidogokidogo hadi kufikia kuanza kutembea,” anaeleza.

Baada ya kuona nimeanza kutembea nilirudi tena Dar es Salaam ili kuangalia uwezekano wa kuendelea kupata matibabu ya sehemu za kutolea haja.

“Nilikwenda hospitali na baada ya kuchukuliwa tena vipimo nilishauriwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi juu ya changamoto katika sehemu za kutolea haja,” alisema.

Aomba msaada wa matibabu
Supa anaomba msaada wa kimatibabu wa ili aweze kupona na kuendelea kufanya shughuli zake za kujipatia kipato.

‘‘Naomba Watanzania wenzangu mnisaidie niweze kupata matibabu ili niweze kurudi katika shughuli zangu za kujipatia riziki,” anasema.
Mjomba wake afunguka

Mjomba wa kijana huyo anaejulikana kama Ellyudi aliiambia Mwananchi kuwa pamoja na changamoto ya kukosa fedha kuhudhuria kliniki na kiendelea kulipa deni wakati mwingine wanashindwa kupata hata chakula na dawa kwani kuna wakati mgonjwa hupata maumivu makali.

“Nilishauriwa na madaktari kuhakikisha ninampatia vyakula vyenye lishe, lakini kutokana na kuyumba kiuchumi baada ya Supa kupata ajali nashindwa.

“Muda mwingine eneo alilotobolewa kwa ajili ya kupitisha mirija ya haja anapata maumivu makali lakini nashindwa hata kumpatia dawa, inaniuma sana nikimuona katika hali hii,” alieleza mjomba huku akibubujikwa na machozi.

Mwananchi pia ilizungumza na Afisa habari wa hospitali ya taifa ya Muhimbili, Sophia Mtakasimba ambaye alithibitisha kuwa kijana huyo alipatiwa matibabu katika hospitali hiyo ambapo hadi anaruhusiwa alikuwa anadaiwa kiasi cha Sh4 milioni na alifanikiwa kulipa kiasi cha Sh250, 000.

“Kiasi alichokuwa anadaiwa wakati anaruhusiwa ni zaidi ya Sh4.13 milioni na katika kiasi hicho alifanikiwa kulipa Sh250, 000 pekee,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
Pole Sana Ndugu Supa. Boda Boda ilikuwa ya Kwako Mwenyewe, au uliajiriwa na Mtu kumuendeshea? Kama ilikuwa ni Ajira, Aliyekuajiri anakusaidia chochote, au Umeishapata Ajali ndio basi Tena Hakujui Tena???
 
So sad
 
Hii stori ndio ilinifanya ninunue gazeti la Mwananchi,akaja jamaa mmoja ambae simjui akaniomba asome wakati mimi mwenyewe sijamaliza akanisahaulisha na kutokomea nalo.

Wabongo kwa uswahili bana?!

Afadhali Mkuu umeiweka hapa
Kuna vitu vianiudhi sana, unakuta mmekaa na watu, mtu wa magazeti anapita wao wanakunywa bia, ukinunua gazeti tuu kabla hujaanza kusoma yeye anawahi naomba nisome kichwa cha habari! Analichukua anakunja nne halafu anakwambia wewe si unaenda nalo nyumbani acha mimi nisome.
 
Tabia za kishenzi sana, unakuta yeye hela yake ina shughuli za kununua Pombe, na ukimwambia na mimi nipe ninywe kidogo matusi yataporomoshwa.
 
Pia akafanye maombi ya kumlaani Dereva aliyefanya kitendo hicho na kutokomea
Haitasaidia demand ya madereva wa magari ya mafuta ni kubwa mno tofauti na malori mengine.

Huyo dereva huenda kahamia kampuni nyingine anapiga kazi.
 
Back
Top Bottom