Ajali iliyoua watu 6 Dodoma: Wanaopaswa kukamatwa na kuwekwa ndani ni Mfugale na Meneja wa Dodoma wa TANROADS Dodoma, sio dereva wa lori

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
7,722
Points
2,000

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
7,722 2,000
Nimesoma habari kuwa ajali imetokea huko Dodoma usiku wa Jumapili 29 December wakati lori lenye namba T364 AZZ lilipokuwa likijaribu kukwepa shimo kubwa barabarani liliigonga Coaster yenye namba T846AYU na watu sita kufa hapo hapo. KUna majeruhi wako hospitali wengine ICU.

Kutokana na tukio hili polisi wanamshikilia dereva wa lori.

Acha tuseme ukweli humu JF. Ajali hii imesababishwa na nani hasa? Je si uzembe wa Tanroads katika kufukia mashimo makubwa barabara kuu na kuyaacha kwa muda mrefu? Hivi ndio tuseme Tanroads, hata kama hawana fedha za kuziba mashimo kwa lami, wameshindwa hata kuyafukia kwa mchanga ili kuepusha ajali za uzembe wa Tanroads kama huu?

Je, huyu meneja wa Tanroads wa Dodoma, ni mara ngapi anatuma vikosi kukagua barabara katika mkoa wake na kuhakikisha hazina mashimo yanayoweza kusababisha ajali? Je Mfugale ameweka huu utaratibu kwa Mameneja wote wa Tanroads mikoani? Mimi ni dereva, na nimewaki kuepuka kifo kwa kuingia porini baada ya basi kuingia upande wangu wakati dereva akikwepa shimo kubwa barabarani. Dereva wa basi hata aliniomba msamaha na kusema hakujua kuna shimo kubwa hiyo sehemu. Na mara kadhaa nimeingia mashimo makubwa ya ghafla barabarani.

Labda swali kubwa kuliko yote ni kwamba kwa kila lita ya dizeli au petroli tunayonunua, kuna fungu linaloenda Tanroads kwa ajili ya kurekebisha barabara. Ndio tuseme fedha hizo hazitoshi hata kufukia mashimo makubwa barabarani kwa kokoto na mchanga kama hawawezi kuziba kwa lami?

Acha tumsifie Mfugale kwa kujenga flyover na kuzipa jina lake, lakini kwa hili la mashimo makubwa yanayoachwa kwa muda mrefu katika barabara zilizo nchini ya Tanroads hawezi kukwepa lawama. Ndio maana nasema wazi kuwa Polisi wanamuonea dereva wa lori katika ajali hii. Waliosababisha hivi vifo vya watu sita na vingine vingi pamoja na uhalibifu wa mali vinavyosababishwa na mashimo makubwa ya ghafla barabarani ni Tanroads.

Reference: Sita wafariki dunia kwa kuparamiwa na lori

1577806124185.png
 
nipekidogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2019
Messages
1,161
Points
1,980

nipekidogo

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2019
1,161 1,980
Hivi kwa akili ya kawaida dreva asababishe ajali iliyochukua maisha ya watu sita halafu useme anaonewa? Kwahiyo ulitaka baada ya ajali aambiwa ni makosa ya tanroads we nenda kasherehekee sikukuu!

Ninaungana na wewe kwamba tanroads wanahusika kwa kutoziba hayo mashimo lakini unamuondoaje kwenye hatia dereva wa roli aise? Hivi dereva hawajibiki kuhakikisha gari analoendesha, la nyuma na mbele yake yako salama?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sajo

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Messages
649
Points
500

sajo

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2010
649 500
Tanroads ni wazembe sana, kutoka Makambako kwenda Mbeya kuna kipande fulani cha barabara pale katikati kinaweza kukutoa roho kwa mashimo yaliyopo.
Nimepita pale jumatatu iliyopita, tena ilikuwa usiku, aisee hawa TANROADS watatumaliza.

Ingawa na sisi tunawachukuliaga poa, hakuna hata kesi wanaposhtakiwa kwa uzembe na kwa kutotekeleza wajibu waliopaswa kutekeleza.
 
wazunguwawili

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2019
Messages
1,029
Points
2,000

wazunguwawili

JF-Expert Member
Joined May 29, 2019
1,029 2,000

Kuna ile majinja ilichinja kutokana na hizi sababu za mashimo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Messages
1,172
Points
2,000

brazaj

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2016
1,172 2,000
Nimesoma habari kuwa ajali imetokea huko Dodoma usiku wa Jumapili 29 December wakati lori lenye namba T364 AZZ lilipokuwa likijaribu kukwepa shimo kubwa barabarani liliigonga Coaster yenye namba T846AYU na watu sita kufa hapo hapo. KUna majeruhi wako hospitali wengine ICU.

Kutokana na tukio hili polisi wanamshikilia dereva wa lori.

Acha tuseme ukweli humu JF. Ajali hii imesababishwa na nani hasa? Je si uzembe wa Tanroads katika kufukia mashimo makubwa barabara kuu na kuyaacha kwa muda mrefu? Hivi ndio tuseme Tanroads, hata kama hawana fedha za kuziba mashimo kwa lami, wameshindwa hata kuyafukia kwa mchanga ili kuepusha ajali za uzembe wa Tanroads kama huu?

Je, huyu meneja wa Tanroads wa Dodoma, ni mara ngapi anatuma vikosi kukagua barabara katika mkoa wake na kuhakikisha hazina mashimo yanayoweza kusababisha ajali? Je Mfugale ameweka huu utaratibu kwa Mameneja wote wa Tanroads mikoani? Mimi ni dereva, na nimewaki kuepuka kifo kwa kuingia porini baada ya basi kuingia upande wangu wakati dereva akikwepa shimo kubwa barabarani. Dereva wa basi hata aliniomba msamaha na kusema hakujua kuna shimo kubwa hiyo sehemu. Na mara kadhaa nimeingia mashimo makubwa ya ghafla barabarani.

Labda swali kubwa kuliko yote ni kwamba kwa kila lita ya dizeli au petroli tunayonunua, kuna fungu linaloenda Tanroads kwa ajili ya kurekebisha barabara. Ndio tuseme fedha hizo hazitoshi hata kufukia mashimo makubwa barabarani kwa kokoto na mchanga kama hawawezi kuziba kwa lami?

Acha tumsifie Mfugale kwa kujenga flyover na kuzipa jina lake, lakini kwa hili la mashimo makubwa yanayoachwa kwa muda mrefu katika barabara zilizo nchini ya Tanroads hawezi kukwepa lawama. Ndio maana nasema wazi kuwa Polisi wanamuonea dereva wa lori katika ajali hii. Waliosababisha hivi vifo vya watu sita na vingine vingi pamoja na uhalibifu wa mali vinavyosababishwa na mashimo makubwa ya ghafla barabarani ni Tanroads.

Reference: Sita wafariki dunia kwa kuparamiwa na lori

View attachment 1308620
Tanroads ni jipu ambalo limeiva ikapitiliza.
 
wazunguwawili

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2019
Messages
1,029
Points
2,000

wazunguwawili

JF-Expert Member
Joined May 29, 2019
1,029 2,000
Hivi kwa akili ya kawaida dreva asababishe ajali iliyochukua maisha ya watu sita halafu useme anaonewa? Kwahiyo ulitaka baada ya ajali aambiwa ni makosa ya tanroads we nenda kasherehekee sikukuu!

Ninaungana na wewe kwamba tanroads wanahusika kwa kutoziba hayo mashimo lakini unamuondoaje kwenye hatia dereva wa roli aise? Hivi dereva hawajibiki kuhakikisha gari analoendesha, la nyuma na mbele yake yako salama?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujawahi kuwa dereva na kukutana na hizo kasheshe barabarani.

Kujaribu kukwepa ama kulipitia posibility ya impact inayofanana bado ipo. Unaweza lipitia ukapasua tair hadi rim ama ukakosa balance pia.

Utamshikiria dereva sawa lakini unapokuja kwenye proximity cause unaweza mchomoa dereva.

Hawa tanroads wanamagari lakini sijui huwa wanayatumia wapi kama hata kufanya ukaguzi tu na kurekebisha ama kuweka alama za tahadhari hawafanyi.

Hivi hakuna sheria ya kuwashitaki hawa watu kwa kushindwa kutimiza wajibu zao.

Sawa hawana hela za kurekebisa,basi haya alama za tahadhari wanashindwa kweli.?Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama sheria ya kuwashtaki haipo ilikuwa vyema kuanzisha mchakato wa haraka. Wametia hasara sana hawa watu.
 
samurai

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2010
Messages
7,234
Points
2,000

samurai

JF-Expert Member
Joined Oct 16, 2010
7,234 2,000
Hivi kwa akili ya kawaida dreva asababishe ajali iliyochukua maisha ya watu sita halafu useme anaonewa? Kwahiyo ulitaka baada ya ajali aambiwa ni makosa ya tanroads we nenda kasherehekee sikukuu!

Ninaungana na wewe kwamba tanroads wanahusika kwa kutoziba hayo mashimo lakini unamuondoaje kwenye hatia dereva wa roli aise? Hivi dereva hawajibiki kuhakikisha gari analoendesha, la nyuma na mbele yake yako salama?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kua uyaone...
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
7,722
Points
2,000

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
7,722 2,000
Hivi kwa akili ya kawaida dreva asababishe ajali iliyochukua maisha ya watu sita halafu useme anaonewa? Kwahiyo ulitaka baada ya ajali aambiwa ni makosa ya tanroads we nenda kasherehekee sikukuu!

Ninaungana na wewe kwamba tanroads wanahusika kwa kutoziba hayo mashimo lakini unamuondoaje kwenye hatia dereva wa roli aise? Hivi dereva hawajibiki kuhakikisha gari analoendesha, la nyuma na mbele yake yako salama?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata kisheria inakubalika. Ila unaonekana huna upeo wa kuelewa vitu kama hivi. Wewe unachoona ni ajali na aliyesababisha ni dereva. Kisheria naweza kukuua na kosa likawa ni lako wewe sio mimi muuaji.
 
black sniper

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2013
Messages
14,947
Points
2,000

black sniper

JF-Expert Member
Joined Dec 10, 2013
14,947 2,000
Tanroad wana husika na vifo hivyo
Haiwezekani washindwe kujua mashimo ambayo yanakaa mda mrefu bila kurakabatiwa wakati kila kukicha wananchi wanatoa kodi
Hapo pamoja na kumkamata dereva lakini Na Tanroad wawajibishwe pia kwa uzembe wao na watu watimuliwe na kushtakiwa
Huo ni uzembe dhahiri usiopingika na hii tabia ya kuacha mashimo bila kutengeneza zipo barabara nyingi tu
Kama wanashindwa kuzitengeneza kwa wakati hata polisi pia wanashindwa kuweka alama za PUNGUZA MWENDO (SHIMO)
Akili hizi sijui zinatumika kwa kulia chakula tu

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
7,722
Points
2,000

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
7,722 2,000
Nimepita pale jumatatu iliyopita, tena ilikuwa usiku, aisee hawa TANROADS watatumaliza.

Ingawa na sisi tunawachukuliaga poa, hakuna hata kesi wanaposhtakiwa kwa uzembe na kwa kutotekeleza wajibu waliopaswa kutekeleza.
Mie sijawahi kuona sababu za msingi za Magufuli kumsifia Mfugale. Inafanya niwe tu na wasiwasi uhusiano wao wakati Magufuli ni waziri kwa kuwa tunajua wazi miradi ya barabara ina fedha nyingi na mianya mingi ya ufisadi.Na Mfugale toka asifiwe inaonekana amejisahau sana.

Ajali na vifo kutokana na uzembe wa Tanroads katika barabara za nchini haviwezi kusafishwa na kujenga fly over Dar es Salaam. Ajali zinazotokana na mashimo makubwa ya muda mrefu barabarani ni uzembe unaopaswa Mfugale sio tu atumbuliwe kwa uzembe bali pia ashitakiwe na kufikishwa mahakamani, pamoja na kosa la matumizi mabaya ya mfuko wa kurekebisha barabara tunaochangia kwa kununua mafuta. Lakini tunajua Magufuli hawezi kumtumbua na watu wataendelea kufa kwa kuwa Tanroads hawana muda wa kufikia mashimo makubwa ya ghafla kwenye hizi barabara zetu.
 
Slow pancha

Senior Member
Joined
Mar 16, 2013
Messages
184
Points
225

Slow pancha

Senior Member
Joined Mar 16, 2013
184 225
Ingine ya kuitarajia ni pale kutoka msolwa kuja mdaula darajani pale wanapoosha vijana magari Kama unakuja mdaula mkono wa kushoto pale kuna handaki moja hatari,na juzi fulani nilikuta roli lililokua limepakia rami limeanguka pale,na leo mi kdg linitoe nje ya barabara lile handaki
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
7,722
Points
2,000

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
7,722 2,000
Tanroad wana husika na vifo hivyo
Haiwezekani washindwe kujua mashimo ambayo yanakaa mda mrefu bila kurakabatiwa wakati kila kukicha wananchi wanatoa kodi
Hapo pamoja na kumkamata dereva lakini Na Tanroad wawajibishwe pia kwa uzembe wao na watu watimuliwe na kushtakiwa
Huo ni uzembe dhahiri usiopingika na hii tabia ya kuacha mashimo bila kutengeneza zipo barabara nyingi tu
Kama wanashindwa kuzitengeneza kwa wakati hata polisi pia wanashindwa kuweka alama za PUNGUZA MWENDO (SHIMO)
Akili hizi sijui zinatumika kwa kulia chakula tu

Sent from my iPhone using Tapatalk
Sasa utakuta kwa unafiki mkubwa wa Tanroads, baada ya hii ajali iliyoua watu ndio wanakimbia kuziba lile shimo. Unajiuliza ni nini kimewawezesha kuziba shimo baada ya ajali na watu kufa ambacho hawakuweza kufanya kabla ya ajali? Unaweza kufikiri labda imebidi wakate mishahara ya January ya wafanyakazi wa Tanroads ili kupata hela ya kuzibia shimo baada ya ajali!
 
abdi ally

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2018
Messages
1,581
Points
2,000

abdi ally

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2018
1,581 2,000
Na siku hz wanachimba mashimo yao hata alam za tahadhar hawaweki hata kidogo juz kat nilikuwa Niko mwendo kidogo hv Hamad shimo hili hapa nikafunga brek za ghafla wa nyuma manusura anivae

Tulichofanya tulifukia shimo lenyewe tukasepa na Kijiji waje watoe Tena mchanga tulioweka alafu wakarabati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forum statistics

Threads 1,392,696
Members 528,663
Posts 34,115,407
Top