Dereva aliyefariki katika ajali iliyoua watu 19 mkoani Songwe kushtakiwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini, kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi, Fortunatus Muslim ameagiza dereva wa gari lililosababisha ajali iliyoua watu 19 akiwamo yeye mwenyewe katika Mlima Senjele wilayani Mbozi mkoa wa Songwe ashtakiwe.

Aidha, ametoa maagizo matatu ya kutekelezwa haraka ili kukomesha ajali zinazojitokeza mara kwa mara na kuua watu wengi katika eneo hilo.

Alitoa maagizo hayo jana siku moja baada ya kutokea ajali ya lori kugongana na basi aina ya Coaster na kusababisha vifo vya watu 19 katika mlima Senjele Mbozi mkoa wa Songwe.

Akizungumza katika eneo ajali hiyo iliyotokea Februari 21 mwaka huu saa 3:15 usiku, kamanda Muslim alitaja jambo la kwanza ni polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kupata chanzo cha ajali hiyo na hatua kuchukuliwa kwa dereva na mmiliki wa gari hilo.

“Hata kama dereva wa gari hilo amefariki lakini ipo sheria inayotumika kumshitaki na pia mmiliki wa lori hilo amekwishajulikana na askari wa usalama barabarani wanamfuatilia ili naye aje ajibu tuhuma za kuruhusu gari lake kutembea barabarani likiwa bovu,” alisema.

Kamanda Muslim alisema jambo lingine ni kuweka askari wa usalama barabarani kwenye vituo viwili katika eneo hilo ambao watakuwa wakiwasiliana kisha kuyaruhusu malori kwa zamu hatua ambayo alisema imeleta mafanikio katika mlima Iwambi mkoani Mbeya ambako tangu Julai mwaka jana hakuna ajali iliyotokea baada ya kuanza kutumia mbinu hiyo.

Alisema hatua nyingine ni kuanzisha kituo cha ukaguzi wa malori makubwa yanayoingia nchini kutoka nje kwa vile husafiri mwendo mrefu sambamba na madereva kuelimishwa umuhimu wa kuendesha kwa kujihami muda wote.

Wakati huohuo, mganga mkuu wa mkoa wa Songwe, Dk Kheri Kagya alisema miili 17 ya watu waliofariki katika ajali hiyo hadi jana asubuhi ilikuwa imetambuliwa na kuchukuliwa na ndugu zao na kwamba miwili bado inahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya mkoa wa Songwe (Vwawa).

Chanzo: Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi akikutwa na hatia itakuwaje??
Msisahau adhabu ya Kuua in KUNYONGWA!!

Je Marehemu atakuwa anahudhuria mahakamani kusikiliza kesi yake??

NB
Mawakili mkamtetea marehemu asinyongwe!!!

Dunia inamambo hii !!!!!!!
Screenshot_20190224-120723.jpg
Screenshot_20190224-120732.jpg
Screenshot_20190224-120751.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
😂😂😂 Haiwezekani, hicho ni kitisho kwa madereva wazembe kuwa makini.
 
Ni yule aliyesababisha ajali iliyoua watu 19 huko Songwe akiwemo na yeye mwenyewe.
Bosi huyo wa trafiki amesema dereva huyo na mmiliki wa roli alilokuwa analiendesha na kugonga Coadter ajali iliyosababisha vifo hivyo wote washtakiwe.

Source gazeti la Mwananchi
Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom