JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Dereva ambaye anatajwa kuhusika katika ajali ya gari iliyopoteza maisha ya watu 6 waliokuwa wakifanya mazoezi pembezoni mwa Barabara ya Sabasaba – Kiseke amepandishwa Mahakamani na kusomewa shtaka moja lenye makosa 15, leo Agosti mosi, 2023.
Mtuhumiwa ni Osward Kaijage Binamungu aliyekuwa akiendesha gari la Toyota Hilux (T476 BZL) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilemela.
Tukio la ajali lilitokea eneo la Shule ya Msingi Lumala Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza mnamo Julai 22, 2023 ambapo pia watu 9 walijeruhiwa.
Kesi hiyo namba 27 ya Mwaka 2023 imesomwa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Anitha Mweri na Mwanahawa Changale wameiambia Mahakama kuwa Osward anakabiliwa na shtaka la kuendesha gari kwa spidi kubwa na kusababisha vifo vya watu sita na kujeruhi watu tisa.
Waendesha mshtaka wamewataja waliopoteza maisha kuwa ni Hamis Nehemiah, Selestine Daudi, Makongoro Manyanda, Peter Fredrick, Amani Matinde na Shadrack Safari.
Waliojeruhiwa kwa kusababishiwa madhara mwilini ni Remidius Ponsian, Grace Chacha, Baraka Jeremiah, Steven Samwel, Maulid Mashaka, Patrick Mathias, Godfrey Benard, Peter Henry na Magnus John.
Mashtakiwa alikana shtaka hilo baada ya kusomwa Mahakamani ambapo upande wa Serikali ukaomba ipangwe tarehe nyingine kwa ajili ya kusoma hoja za awali kufuatia upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.
Upande wa utetezi ukaomba dhamana na kudai mshtakiwa ametoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi, yupo tayari kufuata masharti ya dhamana na kuwa afya yake haipo sawa tangu kutokea kwa ajali hiyo.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilemela, Amani Sumari akasema dhamana ipo wazi.
Mshtakiwa akafanikisha kutoka kwa dhamana, kesi yake inatarajiwa kuendelea Agosti 10, 2023 kwa ajili ya Hoja za Awali.
Pia soma: Mwanza: Ajali iliyoua watu 6 wakifanya mazoezi, dereva afikishwa mahakamani, asomewa makosa 15