Aliyegeuka Chatu

Kwa wale waliokuwa wakiishi Dar miaka ya 80 mnakumbuka mwaka 1987 kuna jamaa na kati ya Buguruni aliyegeuka kuwa chatu?

Hii stori ilibamba sana kipindi hicho.

Da inaogopesha kwa kweli,au huyo mume labda alikuwa ni pepo na sio binadamu,mkewe alidhani ameolewa na binadamu siku ya siku akajidhihirisha....Mungu apishie mbali.
 
Hahahaha, true mkuu... nilitaka tu tufikirie critically kidogo.
Najua you do ila kuna ambao waliamini ni kweli (maybe)
Sasa naomba, please, unambie hiyo mikasa in bold, what was it? Sijawahi sikia...

Daaah...wewe wa wapi na umezaliwa lini Mwali?
 
I am not young that young Mkuu, believe me. lol
sema tu nilikua vijijini na hatukua na gazeti wala redio.
Haya, lete habari!

Okay, wakati Kajima wanajenga ile barabara ya Bagamoyo/ Ally Hassan Mwinyi tunaambiwa walishindwa kuung'oa ule mbuyu. Inavyosemekana kila walipokuwa wanajaribu wanashindwa hivyo ikawalazimu kujenga barabara around it.

Mumiani ni wanyonya damu. Enzi tukiwa shule ya msingi kulienea uvumi kuwa kuna nyonya damu wanaolenga wanafunzi wa shule za msingi...yaani wanakuja wanakukamata halafu wanakunyonya damu na sindano (shindano) zao.

Nakumbuka siku moja tukiwa darasani mishale kama ya saa nane hivi tukasikia mtu anapiga mayowe...(mumiaaaniiii...mumianiiiiii.....), wanyama acha tutimulie maporini.....

Ukweli wa mambo kulikuwa hakuna mumiani wala nini. Ilikuwa ni uzushi tu.
 
Hizi stori huwaga zipo kwenye jamii. Sasa kama ni huwaga za kweli au la, hilo wengi hatuwezi kulithibitisha.

Mwaka juzi tu hapa iliripotiwa kuna mtu kageuka paka au sijui aliota manyoya kama paka pale Salenda briji. Whether that was true or not, I don't know. But it was the talk of the town for some days.

yah ni kwl mkuu, hata hii ya babu na kikombe naona iko kivile vile, bahati mbaya hatuna mfumo/ jinsi ya kuweza kuyafuatilia / kutambua haya mambo!
 
Okay, wakati Kajima wanajenga ile barabara ya Bagamoyo/ Ally Hassan Mwinyi tunaambiwa walishindwa kuung'oa ule mbuyu. Inavyosemekana kila walipokuwa wanajaribu wanashindwa hivyo ikawalazimu kujenga barabara around it.
Hii nilikua sijaipata. So what prevented them kuung'oa?

Mumiani ni wanyonya damu. Enzi tukiwa shule ya msingi kulienea uvumi kuwa kuna nyonya damu wanaolenga wanafunzi wa shule za msingi...yaani wanakuja wanakukamata halafu wanakunyonya damu na sindano (shindano) zao.

Nakumbuka siku moja tukiwa darasani mishale kama ya saa nane hivi tukasikia mtu anapiga mayowe...(mumiaaaniiii...mumianiiiiii.....), wanyama acha tutimulie maporini.....

Ukweli wa mambo kulikuwa hakuna mumiani wala nini. Ilikuwa ni uzushi tu.
Hahahahaha, hii hata kule nilipokua ilifika.
Nadhani habari ilianza walipo gundua maiti ya mtu haina damu hata tone.
In fact nahisi ni mtu aliuwawa kuingine, akavuja damu yote,
walomuua wakaja kudump maiti yake karibu na kijiji chetu.
Kwa sababu moja au nyingine watu waliamini aliuwawa hapo hapo,
na the only explanation as to why the corpse was so pale ilikua kwamba walimnyonya damu.
So Mumiani ndio kiswahili cha vampire?
 
Hahahaaa...Bi Mkubwa, mimi ni mkubwa vya kutosha ila siyo mzee kama baadhi ya watu wanavyozusha.

Na nyumbani tulikuwa hatukosi magazeti wala kukosa kusikiliza BBC Idhaa ya Kiswahili, Voice of America, na Deutsche Welle.

Ngabu mkubwa ni news junkie. Na yeye ndiye shujaa wangu. Kwa hiyo kila alichokifanya wakati nikiwa mdogo nilikiona kiko "cool" sana ikiwemo kusikiliza taarifa za habari na matukio. Na pia, kwa wastani nina kumbukumbu nzuri tu ya mambo mengi.

Lakini sasa kwa kadri umri unavyozidi kwenda kaskazini na majukumu yanavyozidi kuongezeka kumbukumbu yangu nayo ndivyo inavyozidi kwenda kusini.

Keep well mkuu...unakumbukumbu nzuri pamoja na umri kusogea
 
How did it manifest? Mtu akienda na chainsaw au na dozer, what happens?

Hahahaaaa Mwali bana....I like your inquisitive mind! I really do.

So how did it manifest? Well, I wasn't there. But word on the street is that whenever they got there, when they tried to bring it down they just couldn't.

Some say their equipment malfunctioned, some say the tree just disappeared, and a whole bunch of other things.

I don't believe any of them, of course. I just think they wanted to preserve it and that's why they built around it.
 
doza inapinduka
hata Mwanza hii story ipo
maeneo ya Bugando

kuna bibi nyau nyumba ilikataa kubomoka.
Hii ya Mwanza niliipata. Kuna mtu alikua anaendesha dozer pale alinihadithia.
Alisema kua alifanya kusudi kupeleka dozer pande ya tingitingi na kuizamisha
Alikua anamuogopa huyo bibi, hakutaka kuonekana ni yeye kabomoa nyumba
Na upande mwingine hakutaka makaburu wamuone mshirikina, au waone amekataa kazi
So the 'supernatural power' ilifanya kazi zaidi kama intimidation na watu wakaogopa
ila sidhani kama kulikua na nguvu yoyote ilio mziwia hapo.

Hahahaaaa Mwali bana....I like your inquisitive mind! I really do.

So how did it manifest? Well, I wasn't there. But word on the street is that whenever they got there, when they tried to bring it down they just couldn't.

Some say their equipment malfunctioned, some say the tree just disappeared, and a whole bunch of other things.

I don't believe any of them, of course. I just think they wanted to preserve it and that's why they built around it.
Ukisoma hiyo hadithi ya kongosho utaona what I think.
Kwa kifupi kuna bibi fulani alikataa kuhamishwa, kwa madai kua pesa ya compensation ilikua ndogo
Basi serikali ikawapa matajiri ruhusa ya kubomoa kibanda chake (kama kawa, they are pro-mining, against the poor)
Then kila wakituma dozer kubomoa nyumba either inaharibika kabla ya kufika au inazama katika tingitingi.
Watu wanasema walijaribu mwaka mzima bila kufanikiwa, then wakamuongezea bibi pesa na mambo yakawa sawa.
But in fact katika kipindi cha mwaka mzima walijatibu mara tatu tu... then the house was taken down
na mining ikaendelea.
 
How did it manifest? Mtu akienda na chainsaw au na dozer, what happens?

Iringa eneo la isimila kuna makaburi maarufu ya mzee kiyeyeu pamoja na ubishi wake mwaka jana alikubari kuhama mwenyewe makaburi yamechimbwa mabaki yametolewa na bara bara imepita wakat zaman walishindwa umeme umepita ulipofika hapo wakachepusha nguzo kama 3 hv upande wa pil wa bara bara then wakazirudisha upande wa pil kwa mtu mgeni ukiona kwa mara ya kwanza lazima ushangae tanesco walikuwa wanamaana gan kuhamisha nguzo je walikuwa wanakwepa miti inakuwa mirefu hvyo inagusa nyaya wakat sehem nying wameweza kuikata mit isuguse miti kwanin pawe hapo? Au ndo ukwel umeme ulikuwa haupiti ukifika hapo makaburin? Kweli keyeyeu n nuksi.
 
Mara nyingi hizo rumors zinaanzishwa na watu wa karibu na familia inayo husika.
Mtu wa nje ukiskia inakua vigumu kubisha.
Au hata hizo kampuni kama tanesco au Geita in Mwanza,
Unakuta wafanya kazi wake wanaamini kabisa watadhurika
Kwa kukimbia hiyo kazi wanatunga story nyingi za uongo.
 
Lilikuwa tukio kubwa sana, ilikuwa 1987 nilishinda pale kwa takriban siku nne hivi ili nipate kushuhudia, lakini nilichofanikiwa ni kumuona dada wa kimakonde ambaye ndiye inasemekana aliweka dawa kwenye maji ya kuoga ya huyo Mtu Chatu inayesemekana alitolewa mlango wa nyuma wa kituo hicho, mahabusu wote WALIRUHUSIWA watu wa Maliasili walimbeba wakaondoka naye,, mambo ya serikali, wakakanusha kwa nguvu zote, si tukio hilo tu jingine lilitokea Mwananyamala A kwenye gesti iitwayo Kajima,,,,siku hizi imebadilishwa jina,,,, inatazamana na CCM Mwinyijuma jirani sana na shemeji yetu Pamela, RiP aliyeimbwa na Msondo, kuna wazinifu kutoka Tandale walinasiana, madereva wa teksi walikataa kuwabeba kuwapeleka hospitali,,,,umbali mfupi tu, ikabidi wabebwe na mkokoteni, hospitali ya Mwananyamala wakati huo ilikuwa na seng'enge tu, mtiti wake ulikuwa siyo wa kawaida!
 
Aisee ni hatari,hao walionasiana walifanikiwa kunasuka??
 
Back
Top Bottom