Aliyeachiwa mauaji ya billionea Msuya (Mredii) aeleza mazito

Aliyeachiwa mauaji ya billionea Msuya (Mredii) aeleza mazito

Hivi sheria ya madai inademaje juu ya swala hili? Ukiamua kufungua kesi ya madai juu ya jamhuri na polisi taratibu zipoje?
 
Moshi. Wakati Shwaibu Jumanne akitafakari jinsi ya kuanza tena maisha uraiani, mambo mawili bado yanamtesa baada ya kukaa mahabusu kwa miaka mitano.

Jumanne, maarufu kwa jina la Mredii, ndiye pekee aliyeepuka hukumu ya kifo wakati Mahakama Kuu ilipotoa hukumu dhidi ya watu sita walioshtakiwa kwa kosa la kumuua mfanyabiashara maarufu wa Mirerani mkoani Manyara, Erasto Msuya.

Washtakiwa wenzake watano wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa, lakini Mredii amerudi uraiani akitafakari maisha mapya baada ya kusimama kazi yake ya uchimbaji madini kwa miaka mitano.

Hata hivyo, tafakuri hiyo inakabiliwa na kumbukumbu mbaya ya tukio lake; kuanzia alipokamatwa hadi maisha ya mahabusu.

“Moja ya mambo ambayo sitakaa niyasahau ni maumivu niliyoyapata wakati nilipokamatwa,” anasema Mrediii katika mahojiano maalumu na Mwananchi baada ya kuachiwa huru.

“Kipigo nilichokipata mikononi mwa polisi kimemsababishia kilema na maumivu.”

Pamoja na kwamba hakusema bayana katika mazungumzo na Mwananchi, Mredii aliiambia mahakama wakati wa utetezi kuwa aliteswa na polisi hadi kupewa ulemavu, ikiwamo kuhasiwa.

Kutokana na kuhasiwa, Mredii alidai aliamua kumpa talaka mmoja ya wake zake, aliyemtaja kuwa ni Zuhura Hassan kwa vile alikuwa hana uwezo tena kama mwanamume. Amebakiwa na mkewe anayeitwa Adile Juma.

Akiongozwa na wakili wake Majura Magafu kutoa utetezi wake, Mredii alidai mbali na kuhasiwa, polisi walimvunja mara mbili mguu wa kushoto na mara moja mguu wa kulia.

Alisema wakati fulani walimfunga kamba na kumning’iniza kama mbuzi aliyebanikwa.

“Kwa hayo mateso niliyopata hapo kituoni nimekuwa mlemavu. Niliwekwa staili ya mbuzi anayechomwa nikiwa sina nguo,” alidai mahakamani.

Katika mahojiano maalumu na Mwananchi, Mredii alisema hakupata matibabu mazuri kutokana na kipigo hicho na kwamba kwa vile sasa yuko huru, moja ya vipaumbele vyake ni kupata matibabu sahihi ya afya yake.

Anasema jambo jingine ambalo hatalisahau ni kulazimishwa kulala saa 9:00 alasiri na kufungiwa vyumbani hata kama huna usingizi. “Wakati mwingine watu wako nje kwenye shughuli zao, lakini sisi tunalazimishwa kulala,” alisema Mredii.

“Hili jambo haliwezi kutoka kwenye akili yangu kwa haraka na litanisumbua kwa muda mrefu sana.

“Kuanzia saa 9:00 (alasiri) mtu unafungiwa ndani, unaambiwa ulale. Kwa kweli yale yalikuwa mateso makubwa kwangu. Halafu chumba kimoja tunalala watu 18 hadi 27. Kwa kweli sitakaa niyasahau maisha haya.”

Hali hiyo ndiyo inamfanya ashauri vijana na watu wengine kutojihusisha na mambo ambayo yanaweza kusababisha wapelekwee gerezani.

“Waepuke kufanya jambo lolote litakalowafanya wapelekwe gerezani kwa kuwa kule ni mahali pa kudhalilisha sana,” anasema.

“Mtu unapokuwa gerezani unakuchukuliwa kama mhalifu na unapokuwa kwenye lile karandinga watu wanaona wewe ni mhalifu na wengine wanakuita mwizi bila kujua ni kosa gani limekupeleka gerezani".

Source : Mwananchi
Huyo awadanganye hao mwananchi kabla ya tukio hilo alikua magereza kwa case ya ujambazi tena alihukumiwa miaka 15,anaijua jela kuliko kamishna mpya wa magereza,istoshe hakua mchimbaji zaidi ya mwizi
 
Duh Walichomfanyia siyo kitu kizuri kama ana uwezo angefungua tu kesi mimi ndo maana siwapendi polisi
 
Ukiisoma hii kesi,huyu jamaa sio kwamba hakuhusika ila kilichokosekana ni ushahidi.refer to Alibi alikuwa anaoa cku ya tukio
kuna ukweli flani hapo.... huyu ni muhalifu sugu so alikuwa anajua anachofanya.hakuacha waa! mzoefu!
ila sasa kesi itahamia nje....watapukutika watu tu ....!
 
Hii haihitaji Mimi kufuta comment yangu Au Wewe kukubali Au kutokubali

Unadhan hao waliokiri Na kushiriki kutoa Ushirikiano mpaka kuwapata wauaji wote walipewa chocolate au bugger?

POlisi kutesa watuhumiwa ipo Dunia nzima

Rejea Mateso ya Guantanamo bay Kwa Watuhumiwa Sio Wahukumiwa wa ugaidi!

Unateswa utoe ushirikiano ikionekana huna hatia utadai fidia

Unadhan kuna njia gani ya kumlazimisha Mtu atoe ushirikiano zaid ya Mateso?
Hakuna sheria inayoruhusu torturing mbona unapotosha watu hivi mkuu.... Hivi kuhasiwa utalipwa fidia gani?? Kulawitiwa?? Kuvinjwa miguu??? Tusipende kutetea kila kitu kisa uchama tu hatutafika popote
 
Sasa kama hakutoa ushirikiano Mapema na wataalam wakimuangalia machoni wakiona kuna kitu kina miss.....

Ila hapo staki Shari hilo jina tu noma ...sijui panafananaje
Kuna Sitakishari na Mabatini,usithubutu!!!!
 
Hivi hawezi kutibiwa akapona kuhasiwa. Naota tu lakini. Huyo mke wake aliesepa nae ako na mambo mob. Why aondoke haraka hivyo.
Hawa vijana wa boda boda wanaharibu sana ndoa za watu[emoji615]
wanazisaga valvu.sasa utaponaje?
 
Hakuna sheria inayoruhusu torturing mbona unapotosha watu hivi mkuu.... Hivi kuhasiwa utalipwa fidia gani?? Kulawitiwa?? Kuvinjwa miguu??? Tusipende kutetea kila kitu kisa uchama tu hatutafika popote

Wewe ndio unaleta mambo ya Chama Kwa Kuwa akili yako imeshindwa kuishi bila ya kuwaza hayo mambo
Nimeeleza vizuri Kama hujaelewa sina neno la ziada kukuelewesha. Jukumu langu ni kutoa ELimu Kwa wenzangu humu sio kulazimisha kuelewa
Narudia Tena Torturing inaruhusiwa Kama Na Ni halali Kama inafanikisha mtuhumiwa kutoa taarifa muhimu Za uhalifu wake Na Wenzake kusaidia upelelezi pale anapokataa kutoa Ushirikiano katika Mazungumzo ya kawaida LAKINI ikitokea torturing hiyo haijazaa Matunda Kwa maana ya Mtuhumiwa kutoa hizo taarifa Basi ana haki ya kudai fidia Kwa defamation hiyo
 
Ukiisoma hii kesi,huyu jamaa sio kwamba hakuhusika ila kilichokosekana ni ushahidi.refer to Alibi alikuwa anaoa cku ya tukio

Haswaa ! Ni kutokua kwenye eneo la tukio siku ya mauaji kwani ndio siku aliyokuwa anafunga ndoa ! But kama ndie aliyewatafuta wauaji/shooters then na yeye ana mchango katika uhalifu uliotokea maana alijua anatafuta watu wa kwenda kuua kwan lengo la mpango mzima ulikuwa wa kufanya mauaji !!!
 
Awasiliane na Amnesty International sio mahakama za Tz. Jisogeze hata hapo nchi jirani. Tz imegeuka ahera na si peponi tena.
 
Maumivu yahuyu Jamaa ni makubwa mnoo

Mtu akasema ' tunaweza kamata mia, tukawaachia wote akabaki mmoja'

Wakati huo hawa 99 unakuta wamepigika mno kwa makosa yasokua yao.

Miaka mitano ? Kiuchum. Kiafya,kijamii, Amerudishwa nyuma sana.
Pamoja na kuachiwa na mahakama, haimaanishi kuwa hakushiriki, ameshiriki ila ushahidi wa kumtia hatiani haukutosha. Ndio maana naye ameishia kulalamika tu, hawezi kueleza kinagaubaga alihusishwa vipi na tukio hilo. Hiyo itabaki siri yake. Ukienda polisi au kwa state attorney, utakuta maelezo yake yamenyoooka kueleza alivyo shiriki
 
Nadhani Polisi wetu wanakosa uweledi na mbinu za kupeleleza ili kupeleka vithibitisho Mahakamani na wanaishi kutorture watuhumiwa iwe waplead guilty.
Jiunge nao uwape mbinu za kisasa
 
Primitive technology,wengi wanakubali kuepuka ulemavu wakifika mahakamani ukana maelezo yao.
Shauri njia rahisi ya confession. Mtu anauwa, kila mtu anasema anamuona, lkn akiulizwa anasema si kweli.

Suluba huwa pia inasaidia kuwapata washirika. Tusivyo na utu sisi binadamu, yaani kifo cha Msuya leo si habari tena, hatufikirii familia ilivyo athirika kwa kukosa baba, kiongozi wa kaya, msaada wa hali na mali. Tunasahau familia ilivyotiwa umaskini.

Leo tunaamua kuwalaumu polisi waliowezesha watu watano kunyongwa kati ya sita waliokamatwa. Tunalaum as if hakuna lililofanywa.

Na ukirejea huko nyuma, walikamatwa zaidi ya sita, kwa nini wote hawakufikishwa courtini? Sababu ni kukosekana kwa ushahjdi. Mredii ameachiwa huru kuna sehem ushahidi haujambana, lkn ni muuaji hiyo
 
Ni rahisi Sana kukili umefanya kosa hata Kama Haujalifanya maana hiko kibano cha huko ni Kusikia tu kwa watu.Mmmhhhh Ewe Mwenyezi Mungu Naomba unihepushe na Hiki kikombe maana
 
Tujikumbushe ilivyo kuwa.

Erasto anayemiliki vitega uchumi kadhaa na anayeaminika kuwa miongoni mwa wafanyabiashara wa Mirerani wanaoongoza kwa utajiri,
aliuawa jana saa 7:00 mchana wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Eneo la tukio kumeokotwa maganda karibu 21 y risasi zinazoaminika ni za SMG, yaani mwili ni matobo kila sehemu kwa kweli ameuawa kinyam sana, alisema polisi mmoja wa Kituo cha Bomangombe.
Kufuatia mauaji hayo yaliyotokea kati ya neo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na mji wa Bomangombe, mji huo ulifurika magari ya wachimbaji kutoka Moshi, Arusha na Mererani.
Habari za uhakika zilieleza kuwa wauaji wake walikuwa katika pikipiki na baada ya kumminia risasi hizo, walimpora kibegi ambacho haikujulikana kama kilikuwa na madini ama mamilioni ya fedha.
Kulingana na vyanzo vya habari, mfanyabiashara huyo alipigiwa simu na kukubaliana kukutana katikati ya mji wa Bomangombe na makutano y Barabara ya Kia katika Barabara Kuu ya Hai kwenda Arusha.
RPC Kilimanjaro afafanua alivyouawa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema kuwa mfanyabiashara huyo aliuaw saa 7:00 mchana eneo la Mjohoroni kati ya mji wa Bomangombe na makutano ya barabara ya Kia.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Eransto alikuwa akitokea Moshi kuelekea Arusha, na alipofika hilo eneo la Mjohoroni alichepuka na kwenda meta 300 nje ya barabara, alisema.
Kamanda Boaz alisema alipofika eneo hilo, alikutana na vijana wawili waliokuwa na pikipiki ambao waliingia ndani ya gari kwa lengo la kufanya mazungumzo yanayodhaniwa ni ya kibiashara.
Hata hivyo, muda mfupi tu Erasto alishuka kwenye gari lake na kuanza kukimbia na ndipo mmoja kati ya wale vijana alishuka kwenye gari l Erasto na kuanza kumminia risasi nyingi.
source: Gazeti Mwananchi
 
Back
Top Bottom