Hivi mkuu kuachiwa huru, kiuhalisia unakuwa haujatenda wala kujihusisha kwa namna yoyote na kosa hilo ulilotuhumiwa nslo, ama ni technic tu za kisheria ndizo zinazokutema?
Nijuavyo, mimi kushinda kesi haimaanishi haujatenda kosa.
Yaweza kuwa ni udhaifu wa uandaaji wa mashitaka ama weledi wa mawakili wa utetezi.
Rejea kesi ya kina Zombe na wenzake, baadaye yeye kutemwa, je hakuhusika na mauaji hayo?
Huyu Mredii kwa waliofuatilia hii kesi tangu mwanzo, kwa namna fulani alihusika na mauaji hayo.
Maana alikiri kuwa alifanya udalali wa kutafuta wauwaji pamoja na mahali wanapoweza kwenda kununua bunduki ya kufanyia mauwaji hayo.
Cha msingi hapo amuungamie Mungu wake na atubu na kujuta dhambi zake kama anavyojuta sasa.
Lakini hili la kusema alionelewa kufanyiwa hayo aliyofanyiwa na watuhumiwa wenziye, hapana, hapo atakuwa anakosea sana.