Aliens inasemekana kuwasaidia sana jeshi la Marekani katika teknolojia ya silaha

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,542
wanaoaminika kuwazidi binadamu akili ,marekani baada ya kushindwa kuunda kombola la hypasonic wanahaha kuwapata Hawa viumbe

thumb_616_800x420_0_0_auto.jpg

VITABU vitakatifu vimeandika kuwa Mwenyezi Mungu aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana,inaaminika kuwa vitu visivyoonekana ni vingi kuliko vinavyoonekana.

Viumbe hao wa ajabu waishio angani wanaitwa Aliens.Inaaminika wana muonekano kama binadamu isipokuwa hawafanani moja kwa moja na binadamu. Viumbe hao waliogundulika karne kadhaa zilizopita wameshatengenezewa filamu nyingi na wasanii mbalimbali duniani (tutazichambua huko mbele).

Aliens wapo wa rangi tofauti kama kijani, weupe, weusi, njano, zambarau na kila aina ya rangi.Inaaminika kuwa Aliens wanaoishi angani wana akili nyingi kuliko binadamu. Wana mfumo wa kompyuta uitwao Alien Software na wapo juu kiteknojia kuliko binadamu tatizo tuu hawavai nguo!!

Tofauti na binadamu ambaye anafanya kazi kwa hatua moja kwenda nyingine, Aliens wao hufanya mambo kinyume kabisa. Kwa mfano wakitaka kusema ‘naomba maji’ husema ‘maji naomba’ yaani cha nyuma kinakwenda mbele na cha mbele kinarudi nyuma. Kama tunavyowashangaa, nao pia wanatushangaa na kutuona viumbe wa ajabu.

Haijulikani moja kwa moja viumbe hawa wa ajabu wanaishi sayari gani lakini Pia inaaminika waliwahi kuonekana Kisiwa cha Bermuda pwani ya Mashariki mwa Marekani, Kisiwa cha Puerto Rico kilichopo Kaskazini mwa Carrebian na Fort Lauderdale huko Florida, Marekani.

Aliens wanatajwa kuhusika na upotevu wa watu duniani ikiaminika kuwa labda watu hao walikufa lakini ukweli ni kwamba huchukuliwa na viumbe hao.Ndege za kijeshi zimeripotiwa mara nyingi kupotea au kutokuonekana milele ,inaaminika viumbe Aliens ndiyo wahusika wa upotevu huo.Wapo binadamu wanaoamini kuwa Aliens walikuwepo duniani tangu enzi hizo kabla ya binadamu na hawajaondoka.

Inaaminika viumbe hawa wamekuwa wakitua maeneo mbalimbali duniani na kuna baadhi ya serikali duniani zinawajua.Wataalam wa anga wanadai kuwa kazi ambazo zinafanywa na Aliens kwa siku moja binadamu anaweza kutumia miaka 100 kufanyakazi hiyo kwa hiyo viumbe hao wako mbali kimaendeleo na wanafanya wanavyotaka
 
Msiwe mnalishwa matango pori nanyi mnayabeba hivyo hivyo. Ukisubiri aliens waje hapo makao makuu ya jeshi kuwasaidia kuborrsha jeshi lenu mtasubiri sana.

facts.
bajeti ya jeshi la marekani inayo elekezwa kwenye tafiti zinazo lenga uboreshwaji wa silaha na mambo mengine ya kijeshi ni sh. Ngapi?

taifa hilo linazalisha wataalamu wangapi ambao ni wabobezi wa maswala ya teknolojia za kivita?

makampuni/mashirika mangapi binafsi yameingia mikataba na jeshi la marekani kuwauzia teknolojia mpya mpya?

Tazania babu yako akikutwa na gobole huko kijijini alilojitengenezea unadhani Kamanda Sirro atamfanya nini?

Tanzania bajeti ya matumizi na ile ya tafiti ukizilinganisha zinakupa majibu gani?
 
Hadithi za kusadikika tu hizo, hakuna cha Aliens wala nini.

Russia wapelekee moto hao kenge wa magharibi.
Mungu aliumba vinavyoonekana na visiovyoonekana kama unauelewa huu mstari huwezi pinga kuhusu viumbe hivi.

Alliens ni viumbe vichache kati ya viumbe mfanano na binadamu vilivyopo nje ya ulimwengu.

Pana sayari nyingi Sana zaidi ya hizo chache zilizogundulika na huko kuna mamilioni ya viumbe vingine pia.

Kwa mujibu wa watu wenye phd ya elimu kuhusu viumbe visiovyoonekana. Outer worlds.
 
Hiyo midoli ndio unasema ina akili kuliko binadamu? 😂😂

Inamaana hii dozi Urusi anayogawa ndio imefanya mkachanganyikiwa namna hii au nini ndugu zetu?

Za kuambiwa changanya na za kwako! Ingekuwa kweli, basi Marekani alivyo na roho ya kichawi angeshamdunda Russia kwa kutumia tecnolojia za hao midoli 🤣🤣💪🇷🇺🇷🇺🇷🇺
 
ukweli ni kuwa aliens are evil spirits. wazungu atheists hawataki kukubali tu kuwaita mapepo kwa sababu ukisema ni mapepo you become religious na unakiri kuwa Mungu yupo
Alliens sio evil spirit,si kila kiumbe kisichoonekana na evil spirit.
 
Alliens wapo more advanced miaka elf 3 mbele yetu. Vifaa vyao mfano UFO Hakuna kifaa chochote cha binadamu kinaweza kikamata ni lazima kiyeyuke. Technology zote unazoziona duniani ni copy and paste ya vilivyomo katika technology ya ulimwengu usioonekana vitu kama radar, smart tv, phone, jet fighter, satellite, mifumo mbalimbali ya kidunia ulimwengu usioonekana wanavyo tangu kabla. Elites au watu ambao ni magenius mfano kina Tesla, elon musk, Ford, nk hawa wamepewa uwezo (ideas) kwa kulink visiovyoonekana. Hata wazungu wengi ni mchanganyiko wa genies za alliens na binadamu.
Haya mambo huwezi yaelewa hadi uwe na elimu kuhusu viumbe vya ulimwengu usioonekana.
 
Hata elon musk zile akili sio za kibinadamu
Ana link na viumbe visiovyoonekana.Hata wewe unaweza ukalink na external world ukawa na akili za ajabu, utajiri wa ajabu, uwezo mkubwa Sana wa kufikiri,kuona,kutabiri,ukafungua milango sita au kumi ya ufahamu ( tunda la mti wa katikati,means mti wa mema na ujuzi)
 
wanaoaminika kuwazidi binadamu akili ,marekani baada ya kushindwa kuunda kombola la hypasonic wanahaha kuwapata Hawa viumbe​

thumb_616_800x420_0_0_auto.jpg

VITABU vitakatifu vimeandika kuwa Mwenyezi Mungu aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana,inaaminika kuwa vitu visivyoonekana ni vingi kuliko vinavyoonekana.

Viumbe hao wa ajabu waishio angani wanaitwa Aliens.Inaaminika wana muonekano kama binadamu isipokuwa hawafanani moja kwa moja na binadamu. Viumbe hao waliogundulika karne kadhaa zilizopita wameshatengenezewa filamu nyingi na wasanii mbalimbali duniani (tutazichambua huko mbele).

Aliens wapo wa rangi tofauti kama kijani, weupe, weusi, njano, zambarau na kila aina ya rangi.Inaaminika kuwa Aliens wanaoishi angani wana akili nyingi kuliko binadamu. Wana mfumo wa kompyuta uitwao Alien Software na wapo juu kiteknojia kuliko binadamu tatizo tuu hawavai nguo!!

Tofauti na binadamu ambaye anafanya kazi kwa hatua moja kwenda nyingine, Aliens wao hufanya mambo kinyume kabisa. Kwa mfano wakitaka kusema ‘naomba maji’ husema ‘maji naomba’ yaani cha nyuma kinakwenda mbele na cha mbele kinarudi nyuma. Kama tunavyowashangaa, nao pia wanatushangaa na kutuona viumbe wa ajabu.

Haijulikani moja kwa moja viumbe hawa wa ajabu wanaishi sayari gani lakini Pia inaaminika waliwahi kuonekana Kisiwa cha Bermuda pwani ya Mashariki mwa Marekani, Kisiwa cha Puerto Rico kilichopo Kaskazini mwa Carrebian na Fort Lauderdale huko Florida, Marekani.

Aliens wanatajwa kuhusika na upotevu wa watu duniani ikiaminika kuwa labda watu hao walikufa lakini ukweli ni kwamba huchukuliwa na viumbe hao.Ndege za kijeshi zimeripotiwa mara nyingi kupotea au kutokuonekana milele ,inaaminika viumbe Aliens ndiyo wahusika wa upotevu huo.Wapo binadamu wanaoamini kuwa Aliens walikuwepo duniani tangu enzi hizo kabla ya binadamu na hawajaondoka.

Inaaminika viumbe hawa wamekuwa wakitua maeneo mbalimbali duniani na kuna baadhi ya serikali duniani zinawajua.Wataalam wa anga wanadai kuwa kazi ambazo zinafanywa na Aliens kwa siku moja binadamu anaweza kutumia miaka 100 kufanyakazi hiyo kwa hiyo viumbe hao wako mbali kimaendeleo na wanafanya wanavyotaka
Inashangaza sana kuona mtu mzima. Kama wewe unaamini huu ujinga. Filamu zimekutoa ktk mstari
 
Back
Top Bottom