Eugen TZA
Member
- Aug 7, 2023
- 61
- 98
#KashindeUpdates Stori za viumbe wa angani (Aliens ) na UFO's zimerejea tena kwa kasi katika vyombo mbalimbali vya habari Duniani wiki sio kwamba (Mothership) au chombo chao kimetua White House ikulu ya Marekani hapana bali ni kwasababu NASA wiki hii wametoa ripoti yao kuhusu UFO's wakielezea kuhusu tafiti zao katika anga za mbali, chini ya maji Duniani na hata angani n.k
Ripoti hiyo ya kwanza kabisa kutolewa na NASA Wakishirikiana na watafiti huru wa umma na wachunguzi wa vitu visivyo vya kawaida (Unidentified Anomalous Phenomena) (UAP) imehashiria hatua za awali watu Duniani kuelezwa ukweli wote, Sasa baada ya tukio hilo kuzua Gumzo, Mexico wamefuata wakitangaza uchunguzi wao wa kile walichokiita uchunguzi wa mabaki ya Aliens Duniani.
Picha za uchunguzi huo zimetolewa na mwandishi wa maswala ya Anga nchini humo Jaime Maussan ambaye katika ripoti yake ameelezea kuwa mabaki ya viumbe hao wawili wa angani (Ambayo watu wengi wamedai ni feki) yaligunduliwa huko Peru karibu na Columbian Nazca Lines mwaka 2017 kwa mujibu wa Reuters wameripoti, Ambapo baada ya uchunguzi wamegundua mabaki hayo yana umri wa miaka 1,000 na ni ya kipekee tofauti na viumbe wa sayari yetu ya Dunia.
Mabaki hayo ya miili au mifupa ya Aliens wa mchongo wa Mexico mmojawapo ni mwili wa kike ambapo madaktari wanesema wamegundua mayai ndani yake, Wana macho mawili, mdomo, mikono miwili na miguu miwili, Katika kufananisha mabaki hayo na viumbe wa Dunia hii takribani milioni madaktari wanesema kuwa hawajapata kuelewa vyema miili hiyo kutokana na kuwa na utofauti mkubwa mbali sana na uelewa wa binadamu.
Hata hivyo baada ya kuenea kwa taarifa hii Mwandishi wa habari wa BBC, Sam Cabral amewauliza NASA kama wamewasilia na Mexico kufuatilia uchunguzi huo, David Spergel kiti wa NASA's UAP Study Team amemjibu akisema kuwa kama yamepatikana mabaki ya Aliens walipaswa kuweka wazi kuruhusu watu wengine kutafiti kama wanavyofanya NASA kualika watafiti kuchangia kuchunguza kabla ya kuweka wazi kwa umma.
Stori za viumbe wa angani (Aliens) UFO's zimekua zikiripotiwa katika maeneo mbalimbali Duniani kwa muda sasa, Nchi za Urusi, Uchina, na America wamekua wakichunguza kile kinachoitwa vyombo vya ajabu vinavyonaswa na camera angani, kwenye Space, mwezini au chini ya maji baharini Duniani bila kupata majibu, Kwa sasa watafiti wengi wameendelea kuwekeza muda wao kuchunguza kuhusu vyombo hivyo na huenda mbeleni tukapata majibu.
#PeaceOverInterest