Alichaguliwa chuo mwaka jana aka-confirm ila hakuripoti mwaka huu status bado inasoma selected kabla hata ya kuomba tena

NEGAN

JF-Expert Member
May 12, 2023
647
1,442
Habari zenu wakuu. Mwanafunzi mwaka jana aliomba vyuo viwili akapata vyote CBE na TIA. Aka-confirm CBE. Shida ikatokea mkopo hakupata hivyo hata chuo hakuripoti kabisa sababu mpaka batch zote zinatoka hakufanikiwa kupata kabisa na anapoishi ni mkoani.

Sasa mwaka huu wakati dirisha limefunguliwa wakati anajaribu kuomba tena database ya CBE ikamjulisha kuwa tayari ana account kwenye chuo husika kujaribu kulogin ikakubali na status inasoma selected kwa kozi ile ile ya mwaka jana.

Swali langu je hii ina maana bado anatambulika kama mwanafunzi wao CBE hivyo haihitaji tena kuomba mwaka huu sababu alisha-aconfirm tangu mwaka jana hivyo aombe mkopo tu akisubiri kujiunga rasmi hapo oktoba?. Au hii ni system glitch tu?

Nimeomba ushauri kwa wajuzi wa elimu nipate mwanga wa kuanzia japo kesho tutawapigia ili tupate ukweli zaidi.
 
Nenda mnazi mmoja kuna maonyesho ya Vyuo Vikuu mpaka jmosi kuna banda lao CBE
 
Na mimi nina kesi kama hii ngoja tuwasubiri wajuzi
Yaani nimewapigia simu kesho ndio wamesema niwapigie washughulikie. Wanadai ile ya mwaka jana inabidi iondolewe halafu tuombe tena upya. Chuo kikubwa ila mfumo wa hovyo wa mtandao.
 
Wame block ili usiombe tena sababu status itaonyesha ulishachaguliwa wewe usilete za kulete system inskuonanuko chuo unasoma vizuri tu haiwezi kuku select tena kasome Veta au nje ya nchi
 
Yaani nimewapigia simu kesho ndio wamesema niwapigie washughulikie. Wanadai ile ya mwaka jana inabidi iondolewe halafu tuombe tena upya. Chuo kikubwa ila mfumo wa hovyo wa mtandao.
Mkuu mfumo wa hovyo WAP wakat wenyew mlifanya uzembe tena mkubwa Ishu kuhairisha mwaka mbna nindogo Sana SAA zngne muache kuwapa vyuo lawama zisizo za msingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tayari tatizo limetatuliwa nimewapigia na wamemuondoa kwenye mfumo na mwanafunzi ameomba tena.
 
Ilikuwa ishu ndogo sana
Yeah yaani haya mambo mwanafunzi alikosa mkopo nilimshauri aende chuo akaahirishe asikaushe tu yeye akawa mbishi nikamwambia itaokoa gharama kwa wazazi wake na chance ya kuchaguliwa itapungua pia mwaka huu ushindani unawaweza ongezeka na ile kozi aliyopata ya accountancy anawezq kuikosa tena mwaka huu akawa mbishi. Juzi anajaribu kuomba mambo yakamfika shingoni kanifuata anatoa macho kama panya aliyebanwa na mlango😃
 
Habari zenu wakuu. Mwanafunzi mwaka jana aliomba vyuo viwili akapata vyote CBE na TIA. Aka-confirm CBE. Shida ikatokea mkopo hakupata hivyo hata chuo hakuripoti kabisa sababu mpaka batch zote zinatoka hakufanikiwa kupata kabisa na anapoishi ni mkoani.

Sasa mwaka huu wakati dirisha limefunguliwa wakati anajaribu kuomba tena database ya CBE ikamjulisha kuwa tayari ana account kwenye chuo husika kujaribu kulogin ikakubali na status inasoma selected kwa kozi ile ile ya mwaka jana.

Swali langu je hii ina maana bado anatambulika kama mwanafunzi wao CBE hivyo haihitaji tena kuomba mwaka huu sababu alisha-aconfirm tangu mwaka jana hivyo aombe mkopo tu akisubiri kujiunga rasmi hapo oktoba?. Au hii ni system glitch tu?

Nimeomba ushauri kwa wajuzi wa elimu nipate mwanga wa kuanzia japo kesho tutawapigia ili tupate ukweli zaidi.
Kama hajafanyaga usajili chuoni hawez kuhesabika kama 'admited candidate' aombe upya kila kitu
 
I am talking from the experience

Ishu ni kuclear admission
✓chukua barua chuo alichochaguliwa na kupeleka Ofisi za TCU posta.
✓Subiri majibu ndani ya wiki kwa kupigiwa simu na TCU au Kama vipi unawashtua wenyewe. Usisahau kuchukua namba za simu.
✓Endelea na utaratibu wa kuapply kama kawaida.
 
Back
Top Bottom