Habarini JF...
Nianze kwa kusema kuwa kila binadamu ana uhuru wakufanya kile akitakacho bila kuvunja sheria! Uhuru wa kuongea na kutoa maoni ni moja ya haki za binadamu ila tu asivunje sheria!
Na mimi bila kuvunja sheria Naomba niweke wazi kwa kusema kuwa zamani kabla mziki wetu haujavuka nje ya mipaka ya Tanzania, na kabla ya wasanii wa Kibongo kwenda kushoot Video nje ya Nje kwa kutumia Madirector wa nje nilikuwa naangalia Videos alizo kuwa anafanya ADAM JUMA....kwa kiasi chake alikuwa anafanya vizuri kutokana na Mziki wetu ulivyo kuwa zamani....Ingawa nilikuwa naona Makosa mengi ya kiufundi na kitaalamu katika uongozaji wa videos hizo.....Nikikuwa nikiringanisha na wasanii wa nje nikawa ninaona kuwa ADAM JUMA kuna kitu anakosa.....Nilipo Fuatilia kwa ukaribu sana Videos zake nilikuja kugundua kuwa ni kweli Adam Juma kuna makosa yanafanyika.....Nikaanza kususia Videos anazo zifanya Mdogo mdogo baada ya kuona Anakosa Ubunifu!......Siku nilipo anza Kuziona Videos alizo Fanya Nisher nilianza kuamini kile nilicho kuwa nafikiria toka kwa Adam Juma, na baada ya kuangalia Videos za Goodfather nikajua dhahiri kuwa Adam Juma anazingua!
Pamoja na kuwa Adam Juma ni mzoefu wa Kuongoza videos na ni mkongwe katika kazi hiyo leo nimefikia Rasmi Kumdharau na kudharau kazi zake zote anazo zifanya....Nimefikia hatua hiyo baada ya kuona yale aliyo yaandika kuhusu Video ya Alikiba ya Lupela!
Siongelei kishabiki Lakini nimejiuliza maswali Mengi sana kuhusu Post Ya AJ ya kuisifia video ya Alikiba! Asitake kutumia ukongwe wake wa Kazi pamoja na Uzoefu wake kudanganya watu kuwa Video ile ni nzuri mimi Napinga!
Mtu kama AJ sio wa kukaa na kusema Video ile anaipa A,huku Video ikiwa na gizaa,rangi mbaya ya video,background mbaya,video hata haina Mng'ao ya kifupi ni Low quality! haina ushawisha wa mtu kuangalia mara mbili mbili! halafu AJ Anakuja kusema eti Sisi tunao kosoa Hatujui Art hivi kweli mkongwe kama AJ anasema pale tukiangalia kwa umakini tutajua....tutaona nini cha tofauti hata tuangalie kwa makini?, huo mda tunatoa wapi ilihali video inaumiza Macho?
Wasanii wetu wasilewe sifa za Madirector kama hawa kamwe mziki wetu hauto kuja kusonga mbele!, Huwezi kutoka kimziki nje ya Tanzania kwa Video kama Ya Lupela! Ni dhahiri kuwa AJ Kaongea kishabiki na bila kujua anacho kisema! Eti ukiangalia Video ya Lupela utapata Ujumbe.....Ujumbe gani utapata kwenye video kama ile tuwe wawazi,Kwa asie jua kiswahili ni dhahiri kuwa Lupela itampita kushoto kwa kila kitu!
Mwisho kwa quality ya videos za AJ labda kweli kwake hii ni Best Video! Lakini Naona hapa hawa Wakongwe wote wanapelekana wasiko kujua! siku zote Katika Sanaa,UBUNIFU ni kila kitu....Kuisifu video ya Lupela kwa Msanii mkubwa kama Alikiba ni Unafiki na Dharau kubwa sana....Hata underground sahizi hawatoi video kama Za lupela! Ni heri kuitazama Video ya AIYOLA mara 299 kuliko video ya Lupela
“Lupela @officialalikiba , this is art, watanzania
hatujui kuidadavua art. Hatujui thamani ya kitu,
tunachukulia kiurahisi urahisi tu, kila mtu
anajifanya anajua kitu ambacho sio sawa. Hii sio
video tu, tulia basi angalia kwa umakini utapata
ujumbe usipoelewa inawekana tatizo lipo kwenye
level yako ya kuchanganua ujumbe ktk picha, btw
sio fan wa alikiba ni mwana tu. Ningependa
kusema video ni A one, haifanani na kitu
ambacho tumezoe!!! Go kiba….. . ” – Adam Juma