Ali Kiba - Lupela

Ali Kiba - Lupela

Sio tu kwamba hii video ni mbovu lakini pia hata wimbo wenyewe ni mbovu,
Wimbo huu angeimba ndugu yangu GITAA THE TALENTED wa Mtwara sidhani kama hata kwenye vituo vya redio ungesikika!!!!!
 
wasaniii wetu walifuata sana hawa mashabiki uchwara wataishia hapahapa......alikiba alikuwa mtu wa kushindana na AY kipindi hicho alikiba sio wa leo kakaaa eti kushindana na diamond,hawezi hatomuweza kazoea kukaaa uswahili anaendesha mambo yako uswahili mwenzake anajenga uswahili na nje ya uswahilini.....nyie mashabiki wanafiki mwambieni ukweli hatoweza na hatokuja kuweza
waswahili haohao hela hawana, ukipiga show ya 10000 hawaji, mpk 5000. diamobd hata 100000 ngoma inajaa
 
Watu wengi wanajua uzuri wa video ni rangi kuwa ng'aa tu video ya kiba kuna sanaa imefanywa kitaalam ambayo itamfanya afike mbali mambo ya video za magari na magofora ndio mseme video mzuri yamepitwa Adam kaongea kama mtu anayejua fani hiyo wewe endelea kufuatilia rangi
 
Watu wengi wanajua uzuri wa video ni rangi kuwa ng'aa tu video ya kiba kuna sanaa imefanya kitaalam ambayo utamfanya afike mbali mambo ya video za magari na magofora ndio mseme video mzuri yamepitwa Adam kaongea kama mtu anayejua fani hiyo wewe endelea kufuatilia rangi
sawasawa kabisa..!
 
Ukweli zaman nilikua na bifu na naseeb lakin kwa ss nimekubali namheshim sana kiba kwa kazi zake za huko nyuma zilikua poa sana cjui kwa sababu hakua na mpinzan na alibamba sana na nyimbo zake ikiwemo sindelela na nyingine kibao kikubwa na cho mshauri aachane na ushindani na mtu afanye kama yy unajua kushindana sio mara zote huwa lazima ufanyikiwe anatakiwa afanye mziki kama kazi yake bac
 
Anapo sema kama amemdharau adam juma anakosea kilicho kua kinatakiwa atoe ni ishur nn kimepungua nn kiongezwe unapomdharau adam juma kwa kazi yake unakosea sana juma ni mzalendo huenda hata qulity ya vifaa ikawa ndogo tofaut na wenzetu huko mbele turudi kwa video binafc ni ya kawaida sana kama ukilinganisha na video za naseeb ni tofaut video za kiba zinakosa ubunifu mi nafikir anahitaji kijifunza zaid
 
Nakumbuka mwaka 2000 nilibahatika kuona video ya Uswahilini Matola, wimbo wa Kosa la Marehemu Hakuvaa Kondom, ile video jamaa walikuwa mbele ya camera wanacheza kwa kupishana au wanarudi kwa nyuma ili waonekane wote.

In fact location ilikuwa ni moja, mavazi hayakubadilishwa na ni jamaa tu walikuwa wanachana mbele ya camera. Hii video ya Lupela naifananisha na ile video kwa kiasi kikubwa kwa sababu location ilikuwa ni moja, nguo ni zile zile na inaonekana camera zilikuwa stationed sehemu moja tu.

Nilichokipenda kwenye hii video ni ile hali ya Kiba kujidhihirisha kweli yeye ni Balozi wa Wanyama na asingependa kuona wanyama wanauawa kwa sababu za ujangili.
 
Ukiwa shabiki wa diamond raha sana toka nianze kumshabikia ajawai kuniangusha huyu akifa au akiacha mziki nitabidi na mm niache kama alivyo kufa kanumba na mm muvi yakibongo sijawai kuangalia tena na wala siwezi labda za kanumba hii mashabiki wa kiba mna moyo gani sijawai ona katoa video nzuri ata aende wapi na tena matatizo ya kuiga nayeye anataka atoke audio na video kama simba ameona alivyo aribu
 
Watu wengine wanahitaji msaada,video ya lupela iko vizuri kila idara in fact ina lengo chanya juu ya maliasili zetu wee endelea kushoboka na video za majumba na magari ya kukodisha south
 
Labda ubunifu unaouzungumzia kwake ndio huo wa kuondoa mng'ao
 
endelea kushoboka na video za majumba na magari ya kukodisha south
kwani hiyo LUPELA imerekodiwa sehemu gani mkuu...
au huo ukumbi wanaodai ni wa holiwudi ni waTZ..?
kama ni waUSA basi nao walikodi ukumbi...
au kukodi ukumbi ni halali kuliko kukodi majumba..!?
 
Kwa hiyo mashabiki inabidi wakasomee video sasa ili wajue video nzuri na mbaya? Maybe Lupela ni video kwa ajili ya wataalam wa video production.
 
Hahahahaha

Eti unamdharau AJ kwa comment
Na kusahau video 50+ alizotengeneza
Huu ni ujinga
Wa mwaka!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom