Ali Kiba - Lupela

Ali Kiba - Lupela

VIDEO YA AIYOLA IMEFANYWA NA GOODFATHER, SOUTH AFRICA
VIDEO YA LUPELA IMEFANYWA MAREKANI NA MADAIREKTA WAKUBWA TENA
HEBU CHEKI VIDEO KAMA YA CHRIS BROWN DONT JUDGE ME, CHECK VIDEO KAMA YA CHRIS BROWN DEUCE, CHECK VIDEO YA NELLY JUST A DREAM, N.K
GIVE IT A TIME.

WAKATI WEWE UNATANGAZA KUMDHARAU MTU, JIULIZE MKUU YEYE ANAKUTHAMINI?
NASHAURI USISEME UNAMDHARAU TU, KABLA YA KUSEMA HIVYO UNGEWAHI KUANDIKA HAPA KWAMBA BWANA ADAM BADILIKA KTK UTAYARISHAJI WA VIDEO ZAKO KWA KUFANYA MOJA MBILI TATU INGEKUWA POA.

LINGINE, TUSILALAMIKE VIDEO MBAYA, TOA MAONI YAKO, VIDEO IMEKOSEWA WAPI???? ILI NEXT TIME AJIFUNZE KAMA KUNA KOSA...
MTVBASE WAMEPOSTI VIDEO INSTAGRAM JANA HALAFU NYIE MNALALAMIKA,
MSHAURI MWENZIO ABADILIKE KAMA ANAKOSEA...

BUT TO ME, HIYO NYIMBO IMETULIA NA VIDEO NI BABU KUBWA......
WATZ MUMEZOEA KUONA GHOROFA, MAJI, MELI, BEACH.....KUNA SIKU MTU ATAFANYA VIDEO PORINI MTAIDISI...

SANAA KAMA TAWI LA FASIHI HUBURUDISHA, HUELIMISHA N.K
 
Mimi ni mdau wa muziki na ninapenda kazi za hawa wote, ila unaposema P.Square na D'Bhanj wananyimwa usingizi na Diamond, hapo nitakupinga mpaka mwisho. Hawa jamaa wana fanbase ulaya na marekani, kwa Afrika wako mbali sana. Diamond level yake anawatafuta kina Tekno, sio P.Square na D. Bhanj, tuache ushabiki.
Tekno, Davido, Wiz Kid ni wakubwa sana kwa Diamond, na hawezi kuwafikia hili tuongee kwa uwazi tu...

Tukiacha mambo ya tuzo, hebu tujiulize ni lini Diamond alienda kupiga show West Africa (acha show za matukio) au South Africa au nchi yeyote ya Africa ukitoa huku East Africa?? Ila hao akina Tekno, Davido, Wiz Kid wanapiga show nchi mbali mbali na wote hao walishakuja Tz kupiga show pia... Diamond ni Msanii maarufu/mkubwa anayetokea East Africa ila si Msanii Mkubwa Africa...
 
Habarini JF...
Nianze kwa kusema kuwa kila binadamu ana uhuru wakufanya kile akitakacho bila kuvunja sheria! Uhuru wa kuongea na kutoa maoni ni moja ya haki za binadamu ila tu asivunje sheria!

Na mimi bila kuvunja sheria Naomba niweke wazi kwa kusema kuwa zamani kabla mziki wetu haujavuka nje ya mipaka ya Tanzania, na kabla ya wasanii wa Kibongo kwenda kushoot Video nje ya Nje kwa kutumia Madirector wa nje nilikuwa naangalia Videos alizo kuwa anafanya ADAM JUMA....kwa kiasi chake alikuwa anafanya vizuri kutokana na Mziki wetu ulivyo kuwa zamani....Ingawa nilikuwa naona Makosa mengi ya kiufundi na kitaalamu katika uongozaji wa videos hizo.....Nikikuwa nikiringanisha na wasanii wa nje nikawa ninaona kuwa ADAM JUMA kuna kitu anakosa.....Nilipo Fuatilia kwa ukaribu sana Videos zake nilikuja kugundua kuwa ni kweli Adam Juma kuna makosa yanafanyika.....Nikaanza kususia Videos anazo zifanya Mdogo mdogo baada ya kuona Anakosa Ubunifu!......Siku nilipo anza Kuziona Videos alizo Fanya Nisher nilianza kuamini kile nilicho kuwa nafikiria toka kwa Adam Juma, na baada ya kuangalia Videos za Goodfather nikajua dhahiri kuwa Adam Juma anazingua!

Pamoja na kuwa Adam Juma ni mzoefu wa Kuongoza videos na ni mkongwe katika kazi hiyo leo nimefikia Rasmi Kumdharau na kudharau kazi zake zote anazo zifanya....Nimefikia hatua hiyo baada ya kuona yale aliyo yaandika kuhusu Video ya Alikiba ya Lupela!

Siongelei kishabiki Lakini nimejiuliza maswali Mengi sana kuhusu Post Ya AJ ya kuisifia video ya Alikiba! Asitake kutumia ukongwe wake wa Kazi pamoja na Uzoefu wake kudanganya watu kuwa Video ile ni nzuri mimi Napinga!

Mtu kama AJ sio wa kukaa na kusema Video ile anaipa A,huku Video ikiwa na gizaa,rangi mbaya ya video,background mbaya,video hata haina Mng'ao ya kifupi ni Low quality! haina ushawisha wa mtu kuangalia mara mbili mbili! halafu AJ Anakuja kusema eti Sisi tunao kosoa Hatujui Art hivi kweli mkongwe kama AJ anasema pale tukiangalia kwa umakini tutajua....tutaona nini cha tofauti hata tuangalie kwa makini?, huo mda tunatoa wapi ilihali video inaumiza Macho?

Wasanii wetu wasilewe sifa za Madirector kama hawa kamwe mziki wetu hauto kuja kusonga mbele!, Huwezi kutoka kimziki nje ya Tanzania kwa Video kama Ya Lupela! Ni dhahiri kuwa AJ Kaongea kishabiki na bila kujua anacho kisema! Eti ukiangalia Video ya Lupela utapata Ujumbe.....Ujumbe gani utapata kwenye video kama ile tuwe wawazi,Kwa asie jua kiswahili ni dhahiri kuwa Lupela itampita kushoto kwa kila kitu!

Mwisho kwa quality ya videos za AJ labda kweli kwake hii ni Best Video! Lakini Naona hapa hawa Wakongwe wote wanapelekana wasiko kujua! siku zote Katika Sanaa,UBUNIFU ni kila kitu....Kuisifu video ya Lupela kwa Msanii mkubwa kama Alikiba ni Unafiki na Dharau kubwa sana....Hata underground sahizi hawatoi video kama Za lupela! Ni heri kuitazama Video ya AIYOLA mara 299 kuliko video ya Lupela

“Lupela @officialalikiba , this is art, watanzania
hatujui kuidadavua art. Hatujui thamani ya kitu,
tunachukulia kiurahisi urahisi tu, kila mtu
anajifanya anajua kitu ambacho sio sawa. Hii sio
video tu, tulia basi angalia kwa umakini utapata
ujumbe usipoelewa inawekana tatizo lipo kwenye
level yako ya kuchanganua ujumbe ktk picha, btw
sio fan wa alikiba ni mwana tu. Ningependa
kusema video ni A one, haifanani na kitu
ambacho tumezoe!!! Go kiba….. . ” – Adam Juma
najua utaipeenda utaiangalia kidizain hata kwa jicho moja utaichungulia ha ha sio makosa yako ni wivu tu unautesa moyo wako support kazi za wasanii wetu wa nyumbani unapoponda haisaidii kitu mkuu
 
Bongo kume jaa wajuaji wasio jua ili video iwe nzuri unataka uone magari na magorofa?
by the way hakuna kizuri kwa wote . ukitaka kujua kma video ni nzuri au mbaya angalia YouTube kuna poll ya like na dislike utapata ukweli. Ova
 
kwani hiyo LUPELA imerekodiwa sehemu gani mkuu...
au huo ukumbi wanaodai ni wa holiwudi ni waTZ..?
kama ni waUSA basi nao walikodi ukumbi...
au kukodi ukumbi ni halali kuliko kukodi majumba..!?
wewe ni walewale mashabiki vilaza haya sasa video imetoka na ujumbe tumepata tulinde maliasili zetu kwa vizazi vijavyo hao wanaokodi majumba ya kifahali umechukuwa ramani siyo haya kajenge
 
wewe ni walewale mashabiki vilaza haya sasa video imetoka na ujumbe tumepata tulinde maliasili zetu kwa vizazi vijavyo hao wanaokodi majumba ya kifahali umechukuwa ramani siyo haya kajenge
JINA lako na AKILI zako vinafanana...
papiso!!!
 
Nashukuru kijana tutazidi kutoa elimu sababu hamna namna
badilisha kwanza hiyo avatar yako ukitaka uwape elimu watu wenye akili TIMAMU..!
avatar yako inajieleza kila kitu kuhusu uwezo wako wa KUFIKIRI..!
ahsanteh...
 
Kiba kwenye lupela kakurupukaa tusifiche ukweli tu
 
Naona jinsi moyo wako univyofura kwa hasira, kisa AJ kapongeza kazi nzuri iliyofanywa na Director mwenzie! hii ni zaidi ya chuki. I bet jamaa angeiponda hii video, ungekuwa mtu wa kwanza kuleta uzi hapa ukimsifu AJ kama director aliyetukuka, anayejua kazi yake barabara!

Namna hii mziki wetu unasafari ndefu! kwani kumpenda Diamond ni lazima umchukie Alikiba?
 
Naona jinsi moyo wako univyofura kwa hasira, kisa AJ kapongeza kazi nzuri iliyofanywa na Director mwenzie! hii ni zaidi ya chuki. I bet jamaa angeiponda hii video, ungekuwa mtu wa kwanza kuleta uzi hapa ukimsifu AJ kama director aliyetukuka, anayejua kazi yake barabara!

Namna hii mziki wetu unasafari ndefu! kwani kumpenda Diamond ni lazima umchukie Alikiba?
 
Nakumbuka mwaka 2000 nilibahatika kuona video ya Uswahilini Matola, wimbo wa Kosa la Marehemu Hakuvaa Kondom, ile video jamaa walikuwa mbele ya camera wanacheza kwa kupishana au wanarudi kwa nyuma ili waonekane wote.

In fact location ilikuwa ni moja, mavazi hayakubadilishwa na ni jamaa tu walikuwa wanachana mbele ya camera. Hii video ya Lupela naifananisha na ile video kwa kiasi kikubwa kwa sababu location ilikuwa ni moja, nguo ni zile zile na inaonekana camera zilikuwa stationed sehemu moja tu.

Nilichokipenda kwenye hii video ni ile hali ya Kiba kujidhihirisha kweli yeye ni Balozi wa Wanyama na asingependa kuona wanyama wanauawa kwa sababu za ujangili.
Sio kila video lazima zionyeshe mashori na magari ya kifahari na nyumba za ghorofa...

Hao Tembo ni kwasababu hii video imedhaminiwa na Wild Aid..

Hebu angalia hii video aliyodirect Eif Rivera moja kati ya directors wakubwa sana US.. Tatizo watu wanataka kama Chibu aliweka wazungu na magari kwenye video zake basi na Kiba afanye hivyo

 
Sio kila video lazima zionyeshe mashori na magari ya kifahari na nyumba za ghorofa...

Hao Tembo ni kwasababu hii video imedhaminiwa na Wild Aid..

Hebu angalia hii video aliyodirect Eif Rivera moja kati ya directors wakubwa sana US.. Tatizo watu wanataka kama Chibu aliweka wazungu na magari kwenye video zake basi na Kiba afanye hivyo



Mkuu maneno yangu usiyachukulie serious, nachangamsha genge tu na simaanishi nachokisema hapa, ila kuna watu nataka kuona mapovu yao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom