Ali Kiba - Lupela

Ali Kiba - Lupela

wimbo upo vizuri sana na video iko poa,,sema hamjajua kutofautisha nyimbo anazoimba diamond na style ya Ally Kiba,,,style zao ni tofauti. After all hii nyimbo imetolewa maalimu kwa ajili ya wanyama ndiomaana ata background inaonesha kama wako mbugani.

note: video ya msanii ikiwa mbaya laumu director not msaniii
 

Mwacheni Balozi wa Wanyama apige kazi, yeye kama Balozi wa Wanyama aliyejitangaza lazima aonyeshe angalau mnyama mmoja au zaidi kwenye video yake.

Kwa hiyo unataka kusema Kiba anasafiria nyota ya bifu?
Ninachosema ni ujinga kuwashindanisha wakati wao wanapiga pesa..
 
Fan wa muziki kiukweli hawezi kuamua uzuri wa nyimbo kwa kutizama video! Mie hata sihitaji kuona hiyo video ndio nitoe uamuzi. Ngoma nimeidownload na ni tamu saaaaana. LUPELA MBONA IKO SAWA!
Kwa hivyo;thriller ya Michael Jackson haikupaishwa na video???
 
Nakuunga mkono
Alikiba mkali lakin sio mchangamfu kama domo afu ana usharo wa zaman
Nakuunga mkono kabisa ktk hili, nimemuona Alikiba juzi juzi kupitia Tv akihojiwa ktk the sporah show, hajibu maswali anayoulizwa, na kama akijibu lazima atajilinganisha indirectly na diamond, alafu hajachangamka, hana ucheshi.
Ila pia nimewahi muona diamond ktk show hiyo hiyo, jamaa ni mcheshi sana na yuko down to earth kabisa. Nafikiri kwa diamond ule uswahili unamsaidia sana, hajali lolote, yeye anaongea na kucheka kuhusu lolote lililopo ktk ubongo wake.
Kiba aliambiwa aimbe wimbo mmoja wa diamond akakataa. In fact, alisema haimbagi nyimbo za watu, husikiliza tu.
 
Namkubali Alikiba ni mtunzi mzuri ni mwimbaji mzuri na ana sauti nzuri sana, ila video zake mara nyingi haziendani na anachoimba.

Ukiangalia hii video yake haileti hamasa ya kuendelea kuiangalia, haivutii na haina udadisi.

Labda kama lengo la video ni kutetea Tembo, lakini kama ni ya kushindana na Diamond ni sawa baiskeli dhidi ya piki piki.



8f531b79d056fc9bfdf9351491317dbe.jpg

Sasa nimeiona hii video, na NASEMA KUWA NI MZURI, tatizo naloliona kwa watu ni kutaka kazi zake zifanane na za diamond. Haiwezekani akatoa video zinazofanan na za diamond, akopi ili iweje?? Lazima tukubali kuwa jamaa ni tofauti na diamond, binafsi nimeipenda video. Video iko na serene nature fulani hivi. Watu wamezoea na wamekariri kuwa hapa Tz laZima kuwe na Simba na Yanga, ccm na chadema, kiba na diamond. Upuuzi mtupu.
Big up Kiba.
 
Binafsi sioni sababu za kuleta uteam katk hili.. N suala la kiba n diamond tujue hawa ni watu wa wili tofauti hata iweje kiba stl ata kuwa kiba n diamond the same... Cha msingi tusapot mzik mzuri na tuache izo mambo za uteam
 
sidhani kama kuna mtu ana uwezo wa kudirect video zaidi ya Mr. Donovan, wamebakia kusema tu mbaya, hawana hoja zinazoeleweka, big up kiba watu wanakufuatilia sana kuliko unavyofikiri, big up wildaid kwa kumtafutia kijana director mkali
 
Namkubali Alikiba ni mtunzi mzuri ni mwimbaji mzuri na ana sauti nzuri sana, ila video zake mara nyingi haziendani na anachoimba.

Ukiangalia hii video yake haileti hamasa ya kuendelea kuiangalia, haivutii na haina udadisi.

Labda kama lengo la video ni kutetea Tembo, lakini kama ni ya kushindana na Diamond ni sawa baiskeli dhidi ya piki piki.



8f531b79d056fc9bfdf9351491317dbe.jpg

Na ww kiazi kweli..unafikiri Kiba anafanya kazi kwa ajiri ya domo??
 
Nawatupia lawama wote mnaomfananisha Kiba na Diamond. Mnampa jukumu kubwa kuzidi uwezo wake. Koffi Olomide mwenyewe alisema anatamani siku moja afanye ngoma na Diamond sasa huyo Kiba mngemwacha kwenye level yake. Watanzania kuweni wazalendo kwa kuacha uonevu dhidi ya Kiba. Mtoto wa Tandale yuko level ya peke yake kwa sasa
 
Fid q , mwana fa, navy kenzo, chege wametoa video kali mno kuliko za hao wasanii wawili mnao walinganisha peke yao tu..

Kwasasa ben Paul, ommy dimpoz, navy kenzo na chege ni maarufu Africa ukilinganisha na Alikiba
 
Nawatupia lawama wote mnaomfananisha Kiba na Diamond. Mnampa jukumu kubwa kuzidi uwezo wake. Koffi Olomide mwenyewe alisema anatamani siku moja afanye ngoma na Diamond sasa huyo Kiba mngemwacha kwenye level yake. Watanzania kuweni wazalendo kwa kuacha uonevu dhidi ya Kiba. Mtoto wa Tandale yuko level ya peke yake kwa sasa
diamond yupo na nyota safi, kofi kusema angependa afanye kazi naye ni anaangalia upepo umekaa vipi, sio kwamba eti diamond ni nuks zaidi ya Kiba.
Mbona Kiba kafanya kazi na Bella? Bella yuko level nyingine nae kwenye muziki wa dansi.
Ukweli ni kwamba hawa ni wasanii wawili tofauti, kamwe hawatafanana, kila mtu ana kipaji chake. kilichopo hapa ni ushabiki tu na kama ni suala la video kali, Navy Kenzo na Joe Makini wana video kali zaidi ya Mond.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom