Ali Kiba - Lupela

Ali Kiba - Lupela

Video ni nzuri hainaubaya na wimbo ni mzuri. Labda tatizo n sis wabongo tumezoea video kunawadada wapo nusu uchi ndio tatizo linaanzia hapo ilakwa wanaosema n mbaya sijui wanatumia kigezo gani.
 
Nawatupia lawama wote mnaomfananisha Kiba na Diamond. Mnampa jukumu kubwa kuzidi uwezo wake. Koffi Olomide mwenyewe alisema anatamani siku moja afanye ngoma na Diamond sasa huyo Kiba mngemwacha kwenye level yake. Watanzania kuweni wazalendo kwa kuacha uonevu dhidi ya Kiba. Mtoto wa Tandale yuko level ya peke yake kwa sasa
Una gubu
 
diamond yupo na nyota safi, kofi kusema angependa afanye kazi naye ni anaangalia upepo umekaa vipi, sio kwamba eti diamond ni nuks zaidi ya Kiba.
Mbona Kiba kafanya kazi na Bella? Bella yuko level nyingine nae kwenye muziki wa dansi.
Ukweli ni kwamba hawa ni wasanii wawili tofauti, kamwe hawatafanana, kila mtu ana kipaji chake. kilichopo hapa ni ushabiki tu na kama ni suala la video kali, Navy Kenzo na Joe Makini wana video kali zaidi ya Mond.
Endelea kujipa moyo. Mtoto wa Tandale kwa sasa anawanyima usingizi wasanii wakubwa Afrika kama kina P square, Fally, D bhanj na wengine. Wasanii waliobakia (kiba na wenzake) wajitahidi kupambania namba 11 maana namba 1 hadi 10 za Chibu Dangote.
 
Endelea kujipa moyo. Mtoto wa Tandale kwa sasa anawanyima usingizi wasanii wakubwa Afrika kama kina P square, Fally, D bhanj na wengine. Wasanii waliobakia (kiba na wenzake) wajitahidi kupambania namba 11 maana namba 1 hadi 10 za Chibu Dangote.
Mimi ni mdau wa muziki na ninapenda kazi za hawa wote, ila unaposema P.Square na D'Bhanj wananyimwa usingizi na Diamond, hapo nitakupinga mpaka mwisho. Hawa jamaa wana fanbase ulaya na marekani, kwa Afrika wako mbali sana. Diamond level yake anawatafuta kina Tekno, sio P.Square na D. Bhanj, tuache ushabiki.
 
Fid q , mwana fa, navy kenzo, chege wametoa video kali mno kuliko za hao wasanii wawili mnao walinganisha peke yao tu..

Kwasasa ben Paul, ommy dimpoz, navy kenzo na chege ni maarufu Africa ukilinganisha na Alikiba
Huyo Ben ni maarufu Afrika ipi!?
 
Mkuu mi nahisi Diamond atakuwa amefanya figisufigisu video itoke mbaya au unasemaje? Kwasababu kuna watu wanatumia pesa nyingi sana ili King azidi kuwa nyuma kama vitobo vya mkasi...
kwa maana hiyo hata ww kidingi unaafiki kuwa video ni low quality?
 
sidhani kama kuna mtu ana uwezo wa kudirect video zaidi ya Mr. Donovan, wamebakia kusema tu mbaya, hawana hoja zinazoeleweka, big up kiba watu wanakufuatilia sana kuliko unavyofikiri, big up wildaid kwa kumtafutia kijana director mkali
jaribu kuangalia tena ulichokiandika Ali Kiba..!!!
 
Narudia tena Diamond mkataba umefika kikomo
Maisha yake ya mziki yapo ukiongoni atakuja kufulia ile mbayaa
 
Ali kiba anasonteshewa nyota yeye anaangalia mwezi....mtu gani asiyekubali maoni ya mashabiki....maoni ya mashabiki!! ...ama kweli nimeanza kumuelewa mzee wa mvi... ELIMU,ELIMU,ELIMU
 
Habarini JF...
Nianze kwa kusema kuwa kila binadamu ana uhuru wakufanya kile akitakacho bila kuvunja sheria! Uhuru wa kuongea na kutoa maoni ni moja ya haki za binadamu ila tu asivunje sheria!

Na mimi bila kuvunja sheria Naomba niweke wazi kwa kusema kuwa zamani kabla mziki wetu haujavuka nje ya mipaka ya Tanzania, na kabla ya wasanii wa Kibongo kwenda kushoot Video nje ya Nje kwa kutumia Madirector wa nje nilikuwa naangalia Videos alizo kuwa anafanya ADAM JUMA....kwa kiasi chake alikuwa anafanya vizuri kutokana na Mziki wetu ulivyo kuwa zamani....Ingawa nilikuwa naona Makosa mengi ya kiufundi na kitaalamu katika uongozaji wa videos hizo.....Nikikuwa nikiringanisha na wasanii wa nje nikawa ninaona kuwa ADAM JUMA kuna kitu anakosa.....Nilipo Fuatilia kwa ukaribu sana Videos zake nilikuja kugundua kuwa ni kweli Adam Juma kuna makosa yanafanyika.....Nikaanza kususia Videos anazo zifanya Mdogo mdogo baada ya kuona Anakosa Ubunifu!......Siku nilipo anza Kuziona Videos alizo Fanya Nisher nilianza kuamini kile nilicho kuwa nafikiria toka kwa Adam Juma, na baada ya kuangalia Videos za Goodfather nikajua dhahiri kuwa Adam Juma anazingua!

Pamoja na kuwa Adam Juma ni mzoefu wa Kuongoza videos na ni mkongwe katika kazi hiyo leo nimefikia Rasmi Kumdharau na kudharau kazi zake zote anazo zifanya....Nimefikia hatua hiyo baada ya kuona yale aliyo yaandika kuhusu Video ya Alikiba ya Lupela!

Siongelei kishabiki Lakini nimejiuliza maswali Mengi sana kuhusu Post Ya AJ ya kuisifia video ya Alikiba! Asitake kutumia ukongwe wake wa Kazi pamoja na Uzoefu wake kudanganya watu kuwa Video ile ni nzuri mimi Napinga!

Mtu kama AJ sio wa kukaa na kusema Video ile anaipa A,huku Video ikiwa na gizaa,rangi mbaya ya video,background mbaya,video hata haina Mng'ao ya kifupi ni Low quality! haina ushawisha wa mtu kuangalia mara mbili mbili! halafu AJ Anakuja kusema eti Sisi tunao kosoa Hatujui Art hivi kweli mkongwe kama AJ anasema pale tukiangalia kwa umakini tutajua....tutaona nini cha tofauti hata tuangalie kwa makini?, huo mda tunatoa wapi ilihali video inaumiza Macho?

Wasanii wetu wasilewe sifa za Madirector kama hawa kamwe mziki wetu hauto kuja kusonga mbele!, Huwezi kutoka kimziki nje ya Tanzania kwa Video kama Ya Lupela! Ni dhahiri kuwa AJ Kaongea kishabiki na bila kujua anacho kisema! Eti ukiangalia Video ya Lupela utapata Ujumbe.....Ujumbe gani utapata kwenye video kama ile tuwe wawazi,Kwa asie jua kiswahili ni dhahiri kuwa Lupela itampita kushoto kwa kila kitu!

Mwisho kwa quality ya videos za AJ labda kweli kwake hii ni Best Video! Lakini Naona hapa hawa Wakongwe wote wanapelekana wasiko kujua! siku zote Katika Sanaa,UBUNIFU ni kila kitu....Kuisifu video ya Lupela kwa Msanii mkubwa kama Alikiba ni Unafiki na Dharau kubwa sana....Hata underground sahizi hawatoi video kama Za lupela! Ni heri kuitazama Video ya AIYOLA mara 299 kuliko video ya Lupela

“Lupela @officialalikiba , this is art, watanzania
hatujui kuidadavua art. Hatujui thamani ya kitu,
tunachukulia kiurahisi urahisi tu, kila mtu
anajifanya anajua kitu ambacho sio sawa. Hii sio
video tu, tulia basi angalia kwa umakini utapata
ujumbe usipoelewa inawekana tatizo lipo kwenye
level yako ya kuchanganua ujumbe ktk picha, btw
sio fan wa alikiba ni mwana tu. Ningependa
kusema video ni A one, haifanani na kitu
ambacho tumezoe!!! Go kiba….. . ” – Adam Juma
 
Watu wanaifananisha na ile ya Justine Bieber katika simplicity
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom