stanlthecreator
JF-Expert Member
- Jan 9, 2014
- 1,947
- 648
Kwa hii video,alikiba kajidhihiridha kuwa ni underground kabisaaa,video mbovu sanaa
Video haina ubora kaka....ila ni mahaba yenu na kiba tuu ndio yanayowafanya hamfunguki akili....
Poleni kwa kukumbatia huu ujinga
nimekuzoea kuongea kwa mikwara na vitisho ilhali hoja unakua huna.
Ninakumbuka vizuri fasih niloisoma form three...
Jina la hadith, story au kitabu na picha ambayo ipo juu ya kava uwa kwa kifupi vinaonesha themes kwa nini kipo ndani.
If that is so! Nijibu sasa.
Jina ,chekecha cheketua na vimbwanga vinavyoonekana kuna uhusiano gani.
Ndio maana twasema, hata wale wahusika ktk video hataelewi walichokua wanafanya.0lakin la muhm zaid sidhani kama ilikua na script na kama ilikuwepo basi director hakuielewa.
Ukinijibu ki lofa nakupotezea mazima.
Isingekuwa sawa kwangu kuingia humu na kupita bila ya kuzungumzia habari kubwa iliyopo sasa juu ya ujio wa bonge moja la video la muziki wa Bongo Flava ambayo sio ya waimba muziki wa Naija. Na baada ya kusoma maoni ya baadhi ya watu, nimeona niseme jambo hili kidogo kabla sijaondoka humu.
Binafsi, nahisi sehemu kubwa ya jamii ya Kitanzania haina uelewa wa kutosha kuhusu video za muziki, hudhani ni kuweka tu matukio hata kama hayana maana, wala hayaungani na matukio mengine. Huamini kuwa, ubora wa video ni kuonesha magari ya kifahari na nyumba za kitajiri.
Kama si miongoni mwa watu niliowaeleza hapo juu, hutasita kutoa pongezi kwa video ya Chekecha Cheketua Kiba iliyochezwa kwa mara ya kwanza na kituo cha kimataifa cha runinga cha Trace Urbun, tena kwa namna inayoupa heshima muziki wetu na lugha yetu (swahili).
Kwa heshima zote nakubaliana na video ya Chekecha Cheketua, sio kwa ushabiki au kufuata mkumbo, bali kutokana na malengo ya video kukamilishwa vizuri na timu iliyoitayarisha video hiyo. Umakini wa props, maleba na mapambo ulikuwa ni mkubwa sana kiukweli.
Angalia magari yaliyotumika, angalia redio zilizomo humu ndani. Na sio ajabu Kituo kikubwa kama Trace Urbun kuamua kuipiga kama exclusive, na kupiga mara saba (7) ndani ya saa kumi na mbili (12) za siku moja, ambayo kwa hesabu za haraka, waliipiga kila baada ya saa moja na nusu.
Tueleweshane Kidogo!
Kwa wale waliobahatika kupata nafasi ya kuelimika, naamini watakuwa wakifahamu kuwa muziki ni fasihi. Na maana ya Fasihi ni utanzu (tawi) wa sanaa ambao hutumia lugha ya mazungumzo/vitendo au maandishi ili kufikisha (kuwasilisha) ujumbe fulani kwa hadhira husika.
Katika kazi yoyote ya fasihi lazima pawepo na ustadi wenye kuleta mvuto fulani kwa hadhira (wasikilizaji/watazamaji au wasomaji) husika. Na ustadi (ufundi) huo unaovutia hadhira ndio huitwa FANI, ambayo hujumuisha mambo kama vile:
- Muundo (mtitiriko/msuko/mpangilio wa matukio/visa)
- Mtindo (mbinu inayotumiwa na fanani ili atofautiane na fanani mwingine)
- Wahusika (watu au vitu ambavyo hutumiwa na fanani katika kazi yake)
- Mandhari (eneo ambalo fanani hulitumia katika kuumba kazi yake)
Vilevile kazi yoyote ya fasihi huwa na ujumbe na malengo mbalimbali ambayo hukusudiwa yaifikie jamii husika. Yale yote ambayo msanii wa kazi ya fasihi anakusudia yaifikie jamii husika, ndio huitwa Maudhui (content). Maudhui ya kazi ya fasihi hujumuisha:
- Dhamira
- Ujumbe
- Migogoro
- Falsafa/misimamo
- Mtazamo
Kazi ya fasihi ni kujaribu kusawiri vipengele vya maisha, mahusiano, na hisia za watu katika jamii husika, ambayo huwasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo au vitendo. Na kuna aina kuu mbili za fasihi ambazo ni Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi.
Kisa cha kwenye video ya Chekecha!
Nampongeza mwandishi wa script, muongozaji na wawasilishaji kwa maana ya washiriki wote tuliowaona kwenye video hii. Tukirudi kwenye fasihi, maana (DHAMIRA) ya video hii kuelezea kwa vitendo 'NGUVU YA SANAA YA MUZIKI KWA JAMII'.
Kisa kiko hivi, Kiba anafika kwenye mji usio na maendeleo makubwa na wakazi wake hawako huru kufanya majukumu yao (kutengeneza gari/mke na mume kufunguliana milango ya gari), kufanya wapendacho (kushiriki michezo kama karata/gofu, kusikiliza redio) na kunyimwa haki ya kuzungumza, kwani wako kwenye amri ya kuganda (MIGOGORO).
Na kwa kawaida amri hutolewa na utawala. Kiba anashangazwa sana na hali hiyo, hivyo kuonesha kuwa ndio kwanza anakutana nayo kwa mara ya kwanza. Moja kwa moja anaamua kuwakomboa kwa kutumia silaha ya muziki (sauti ya kumtoa nyoka pangoni), anawaimbia na wote kuwatoa kifungoni.
Hapa ana lengo la kutueleza (UJUMBE) muziki unavyoweza kutumika kutatua migogoro (vita/uonevu) mikubwa ya kiutawala na kufanya dunia kuwa huru. Hatimaye kwa kutwa moja tu, mji ulioonekana kutokuwa na watu (mpweke) ukaonekana kujaa watu wakicheza na kushangilia huku wengine wakibaki kuwa mashabiki.
Kuna kitu cha kupongezwa sana nimekiona kwenye video hii, ambacho ni kukwepa kuonesha tabia za Kimagharibi, kama mavazi, uchezaji wa mitindo ya kuhamasisha ngono, na badala yake kuonesha Uafrica wetu (FALSAFA/MISIMAMO) na taratibu zetu.
Namsifu sana muongozaji wa video hii Meji Alabi kwa kuifanya video isiwe kwenye muonekano wa video za muziki wa Nigeria, na kufanikiwa kuilinda Bongo Flava na zaidi dansa wa Kitanzania, Kellz Mbowe kuwa ndiye dansa aliyeonekana zaidi (ndiye yule aliyefungua boneti ya gari).
Ukirejea maelezo haya utagundua kwamba, kilichofanyika kwenye video ya Chekecha Cheketua kilifuata misingi ya Fasihi kwa umahiri mkubwa, kuanzia Muundo, Mtindo, Wahusika na Mandhari.
Ova
Heheheeeeeeee.
"Kama ni macho ya blueray sema nini unataka" inabidi video ieditiwe ayo macho yaonekane
Lazima kiba tumpe challenge..
Kwa nia nzur tu ili aweze kuzid piga hatua
Lazima kiba tumpe challenge..
Kwa nia nzur tu ili aweze kuzid piga hatua
Sasa >> nana media tour Nigeria
3, july >> Nigeria road to mama
4, july >> Tanzania, sherehe ya miaka 80 ya Yanga, jangwani
8, july >> Singida, with Mohammed Dewji
18, july >> South Africa, MTVMAMA2015 ambapo atatumbuiza na NEYO
24, july >> Kilimanjaro Miss ambassador ambapo show inaweka rekodi kuwa na viingilio vikubwa nje ya dares salaam
30,000/=, mpaka 300,000/=
25, july >> South Africa, African achievers awards ambapo amekuwa nominated kama Most inspiring icon
Jamaniii mi nataka saule kama mapenzi gorofa yamejaa Kariakoo
Mi nna mapenzi tele kama kwetu kule -
Wanao nitaka ni wengi ila kwako nyanga nyanga nyanga
Nini unataka mi nina miujiza nini unataka-
Ama ni maji ya bluelight sema nini unataka-
Nikugeuze Princess sema nini unataka
Unavyo biringa bayondo hivyo mi ndo nataka taka sana natakaa
Nini unataka mi nina miujiza nini unataka-
Nikugeuze Princess sema nini unataka
Siamini yaani siamini yamenipanda kichwani mahaba ya kuota sinitimi yamenikoleza mwilini
Siamini ooh siamini yamenipanda kichwani mahaba ya kuota sinitimi yamenikoleza mwilini
Aya chekecha
Chekecha (x11)
Aya chekesha cheketua cheke chekecha cheketua -cheke chekesha cheketua cheke chekesha cheketua cheke
Masia Uluso kitaa Abu Daddy-
Penzi alinipa mama nami leo nakupatia tena sitaki lawama penzi kiapo hakuna-
Mi ntakupenda sana mpaka wivu utakimbia nami ntalia na wewe mimi kwako nyanga nyanga nyanga-
Nini unataka mi nina miujiza nini unataka-
Ama ni maji ya bluelight sema nini unataka-
Nikugeuze Princess sema nini unataka
Unavyo biringa bayondo hivyo mi ndo nataka taka sana natakaa
Nini unataka mi nina miujiza nini unataka-
Nikugeuze Princess sema nini unataka
Siamini yaani siamini yamenipanda kichwani mahaba ya kuota sinitimi yamenikoleza mwilini
Siamini ooh siamini yamenipanda kichwani mahaba ya kuota sinitimi yamenikoleza mwilini
Aya chekecha
Chekecha (x11)
Aya chekesha cheketua cheke chekecha cheketua -cheke chekesha cheketua cheke chekesha cheketua cheke
Yeah uuh cheke chekecha -aah heyiiii-
Eti eeeeeh! Haya chekechaaaa cheketuaaaaaaaa
blogger am talking about this.
Hiyo treni ni mpya kabisa inashepiwa kizamani kwa akili zako ndogo huwezi kuyajuwa haya.
Mm simkUbali kiba kabisa...
Alafu lov unanikosea kikubwa sana.
Ndo nini unaleta fujo ukwen?
unashindwa kuwaheshimu ata shemeji zako?
Acha izo bhana si unajua siwezi kukulabulia maneno?
Basi stop it
Mm simkUbali kiba kabisa...
Kuna tofauti kubwa kati ya Challenge na roho ya kwanini!
Unachallenge kila kitu?.Unaponda tuu, unakashifu, unasiliba, unakosoa!
Hivi hujioni kuwa una matatizo?
Mpaka mnajiapiza kuwa Kiba hawezi, hawezi!
Mxiiu.....
There is a thin line between love and hate.
Nawaona watu wapo obsessed na mampungufu ya kiba mwanzo mwisho.
Video nzuri sana ina viwango vya kimataifa .
Kuna tofauti kubwa kati ya Challenge na roho ya kwanini!
Unachallenge kila kitu?.Unaponda tuu, unakashifu, unasiliba, unakosoa!
Hivi hujioni kuwa una matatizo?
Mpaka mnajiapiza kuwa Kiba hawezi, hawezi!
Mxiiu.....
There is a thin line between love and hate.
Nawaona watu wapo obsessed na mampungufu ya kiba mwanzo mwisho.
Video nzuri sana ina viwango vya kimataifa .
Hapo sijazungumzia mazingira ya video, masalusalu yameanikwa mtaani.,mauchafu uchafu, watu wenyewe wale ni kama ilikua ni asubuhi wametoka aamka hata mswaki bado.
Acheni upofu, ongeeni ukweli.