Ali Kiba Fans' Special Thread...

Ali Kiba Fans' Special Thread...

Avemaria kumbe ulipigwa ban, aisee sikuona hiyo kitu, watu wanachukulia jf serious sn aiseee, wataishi maisha magumu sn.

best ban ila iliisha kuna mmoja akasema kabisa hampendi nifah simtaji ila anajijua mwenyewe dah mwenzie akadakia yupo kwenye mfungo..
aiseee kazi wanayo watu!!

unachukia fake id kisa daimond na aly kiba...!!upuuzi mtupu!!au unatukana mzazi wa mtu kisa these two people i dont know siku wakipatana itakuaje..n
 
Last edited by a moderator:
hivi na lazima kwenda south africa...!!!!!.... this was the most anticipated video kibongobongo.....at the end utumbo mtupu
 
Mdakuzi shem darling hasante kwa somo hilo, ila sasa hawa vichwa hewa hiyo lugha umetumia ngumu mnooo, ungewekapo kaudaku kidogo wangekuelewa, sasa hawa wanaojua video ni maghorofa na malambojini sijui hata hawaelewi, shule yenyewe wanajisifia ila sidhani km hata walikwenda, maana mie mwenye kacheti kangu ka QT nimeielewa mnooo hii video,

Ila hawa watu vichwa vigumu nzi imesingiziwa, wanaponda hapa wakayi huko wsnacheketua.
 
Last edited by a moderator:
Sasa >> nana media tour Nigeria

3, july >> Nigeria road to mama

4, july >> Tanzania, sherehe ya miaka 80 ya Yanga, jangwani

8, july >> Singida, with Mohammed Dewji

18, july >> South Africa, MTVMAMA2015 ambapo atatumbuiza na NEYO

24, july >> Kilimanjaro Miss ambassador ambapo show inaweka rekodi kuwa na viingilio vikubwa nje ya dares salaam
30,000/=, mpaka 300,000/=

25, july >> South Africa, African achievers awards ambapo amekuwa nominated kama Most inspiring icon
 
Isingekuwa sawa kwangu kuingia humu na kupita bila ya kuzungumzia habari kubwa iliyopo sasa juu ya ujio wa bonge moja la video la muziki wa Bongo Flava ambayo sio ya waimba muziki wa Naija. Na baada ya kusoma maoni ya baadhi ya watu, nimeona niseme jambo hili kidogo kabla sijaondoka humu.
Binafsi, nahisi sehemu kubwa ya jamii ya Kitanzania haina uelewa wa kutosha kuhusu video za muziki, hudhani ni kuweka tu matukio hata kama hayana maana, wala hayaungani na matukio mengine. Huamini kuwa, ubora wa video ni kuonesha magari ya kifahari na nyumba za kitajiri.
Kama si miongoni mwa watu niliowaeleza hapo juu, hutasita kutoa pongezi kwa video ya Chekecha Cheketua Kiba iliyochezwa kwa mara ya kwanza na kituo cha kimataifa cha runinga cha Trace Urbun, tena kwa namna inayoupa heshima muziki wetu na lugha yetu (swahili).
Kwa heshima zote nakubaliana na video ya Chekecha Cheketua, sio kwa ushabiki au kufuata mkumbo, bali kutokana na malengo ya video kukamilishwa vizuri na timu iliyoitayarisha video hiyo. Umakini wa props, maleba na mapambo ulikuwa ni mkubwa sana kiukweli.
Angalia magari yaliyotumika, angalia redio zilizomo humu ndani. Na sio ajabu Kituo kikubwa kama Trace Urbun kuamua kuipiga kama exclusive, na kupiga mara saba (7) ndani ya saa kumi na mbili (12) za siku moja, ambayo kwa hesabu za haraka, waliipiga kila baada ya saa moja na nusu.

Tueleweshane Kidogo!
Kwa wale waliobahatika kupata nafasi ya kuelimika, naamini watakuwa wakifahamu kuwa muziki ni fasihi. Na maana ya Fasihi ni utanzu (tawi) wa sanaa ambao hutumia lugha ya mazungumzo/vitendo au maandishi ili kufikisha (kuwasilisha) ujumbe fulani kwa hadhira husika.
Katika kazi yoyote ya fasihi lazima pawepo na ustadi wenye kuleta mvuto fulani kwa hadhira (wasikilizaji/watazamaji au wasomaji) husika. Na ustadi (ufundi) huo unaovutia hadhira ndio huitwa FANI, ambayo hujumuisha mambo kama vile:
  • Muundo (mtitiriko/msuko/mpangilio wa matukio/visa)
  • Mtindo (mbinu inayotumiwa na fanani ili atofautiane na fanani mwingine)
  • Wahusika (watu au vitu ambavyo hutumiwa na fanani katika kazi yake)
  • Mandhari (eneo ambalo fanani hulitumia katika kuumba kazi yake)

Vilevile kazi yoyote ya fasihi huwa na ujumbe na malengo mbalimbali ambayo hukusudiwa yaifikie jamii husika. Yale yote ambayo msanii wa kazi ya fasihi anakusudia yaifikie jamii husika, ndio huitwa Maudhui (content). Maudhui ya kazi ya fasihi hujumuisha:
  • Dhamira
  • Ujumbe
  • Migogoro
  • Falsafa/misimamo
  • Mtazamo

Kazi ya fasihi ni kujaribu kusawiri vipengele vya maisha, mahusiano, na hisia za watu katika jamii husika, ambayo huwasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo au vitendo. Na kuna aina kuu mbili za fasihi ambazo ni Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi.

Kisa cha kwenye video ya Chekecha!
Nampongeza mwandishi wa script, muongozaji na wawasilishaji kwa maana ya washiriki wote tuliowaona kwenye video hii. Tukirudi kwenye fasihi, maana (DHAMIRA) ya video hii kuelezea kwa vitendo 'NGUVU YA SANAA YA MUZIKI KWA JAMII'.
Kisa kiko hivi, Kiba anafika kwenye mji usio na maendeleo makubwa na wakazi wake hawako huru kufanya majukumu yao (kutengeneza gari/mke na mume kufunguliana milango ya gari), kufanya wapendacho (kushiriki michezo kama karata/gofu, kusikiliza redio) na kunyimwa haki ya kuzungumza, kwani wako kwenye amri ya kuganda (MIGOGORO).
Na kwa kawaida amri hutolewa na utawala. Kiba anashangazwa sana na hali hiyo, hivyo kuonesha kuwa ndio kwanza anakutana nayo kwa mara ya kwanza. Moja kwa moja anaamua kuwakomboa kwa kutumia silaha ya muziki (sauti ya kumtoa nyoka pangoni), anawaimbia na wote kuwatoa kifungoni.
Hapa ana lengo la kutueleza (UJUMBE) muziki unavyoweza kutumika kutatua migogoro (vita/uonevu) mikubwa ya kiutawala na kufanya dunia kuwa huru. Hatimaye kwa kutwa moja tu, mji ulioonekana kutokuwa na watu (mpweke) ukaonekana kujaa watu wakicheza na kushangilia huku wengine wakibaki kuwa mashabiki.
Kuna kitu cha kupongezwa sana nimekiona kwenye video hii, ambacho ni kukwepa kuonesha tabia za Kimagharibi, kama mavazi, uchezaji wa mitindo ya kuhamasisha ngono, na badala yake kuonesha Uafrica wetu (FALSAFA/MISIMAMO) na taratibu zetu.
Namsifu sana muongozaji wa video hii Meji Alabi kwa kuifanya video isiwe kwenye muonekano wa video za muziki wa Nigeria, na kufanikiwa kuilinda Bongo Flava na zaidi dansa wa Kitanzania, Kellz Mbowe kuwa ndiye dansa aliyeonekana zaidi (ndiye yule aliyefungua boneti ya gari).
Ukirejea maelezo haya utagundua kwamba, kilichofanyika kwenye video ya Chekecha Cheketua kilifuata misingi ya Fasihi kwa umahiri mkubwa, kuanzia Muundo, Mtindo, Wahusika na Mandhari.

Ova

asante Mdakuzi kwa ufafanuzi wako
 
Last edited by a moderator:
best ban ila iliisha kuna mmoja akasema kabisa hampendi nifah simtaji ila anajijua mwenyewe dah mwenzie akadakia yupo kwenye mfungo..
aiseee kazi wanayo watu!!

unachukia fake id kisa daimond na aly kiba...!!upuuzi mtupu!!au unatukana mzazi wa mtu kisa these two people i dont know siku wakipatana itakuaje..n

Wale watu nimegundua wana matatizo binafsi ambayo inabidi tu tuyavumilie kwakweli, thats the way they r even in their real lives, nimewahi shuhudia wakigeukana humu na kuchambana hatari, nikapigia tu mstari, hivyo yaani siku hizi nawadharau hamna mfano.
 
Lazima mjue kutofautisha kati ya

+Anaetoa video kali ya kimataifa level za mtv na bet awards kwasababu anauwezo na kipaji

+Anaetoa video kuepuka lawama za mashabiki kumbe ndio anawaongezea mzigo wa mawazo

Hata hivyo mlikuwa mnafikiria nini mlivyokuwa mnamlazimisha atoe?? ndio maana alikuwà anasita ALIKUWA ANAOGOPA HAYAHAYA HAHAHAHA
 
hivi na lazima kwenda south africa...!!!!!.... this was the most anticipated video kibongobongo.....at the end utumbo mtupu

Hahahaaaaaa!!! Km zile sijui nn hivi kwann mlikwenda south? Au mlifuata lambojini?? Mkijijibu hilo basi potea tu usiendelee kujitia aibu humu.
 
asante Mdakuzi kwa ufafanuzi wako

Asante sana ndugu yangu. Naambiwa PM ningefungulia thread hayo maelezo niliyoyatoa, muda umeniishia hapa, yeyote anaweza kufanya hivyo kwa niaba yangu. Asanteni wote kwa PM, asanteni ndugu zangu wa Team Kiba, nilitaka nikae sana hapa, ila natakiwa kujiandaa kwa safari.

Ova
 
Ngoja nikaisome online, nione namna wenye utimamu wao wanavyomuongelea King, maana watoto wa BRN hata hawajui wanaongelea nn ni mihemko tuuuu, king ni badest news wallah!

itakuwa umefanya la maana sana ukiiisoma hiyo habari KINGKIBA domo kaa mbali sio maneno yangu bwana ni ya mwanaspoti nilifurahi saana kuiona hii newz
 
mkuuu mambo hayooo

Sasa >> nana media tour Nigeria

3, july >> Nigeria road to mama

4, july >> Tanzania, sherehe ya miaka 80 ya
Yanga, jangwani

8, july >> Singida, with Mohammed Dewji

18, july >> South Africa, MTVMAMA2015 ambapo
atatumbuiza na NEYO

24, july >> Kilimanjaro Miss ambassador ambapo
show inaweka rekodi kuwa na viingilio vikubwa
nje ya dares salaam
30,000/=, mpaka 300,000/=

25, july >> South Africa, African achievers awards
ambapo amekuwa nominated kama Most
inspiring icon
 
Yaani walitegemea magari ya kifahari na location expensive ila alichofanya meji alabi ni hatari, kachukua van moja model ya zamani na ile nyingine tulikuwa tunaita mgongo chura, pia kellys alifanya kazi nzuri kwenye kuvaa #vivakiba

Yani hii video nimeipenda sana idea yake iko simple hadi matukio yako well arranged. Hasa hapo kwa hyo redio ya kizamani magari hadi uvaaji.
In short hii video imenikosha I love the idea.
 
nifah ungestick tu to ur promise.

Kwamba ungerudi hapa baada ya mfungo.

Kinyume na hapo utakuwa wajishindisha njaa tu.

SORRY.

daah braza heshimu imani ya Mtu bosi,anae jua funga ya kweli ni Mungu peke yke na si vinginevyo sio busara kuanza kutoa hukumu za kipuuzi.

ukianza kui ngiza haya mambo ya kufunga mara nini sijui utakua unawakoseA waislam wote walio funga wanao ingia jf.

tuheshimu imani za wenzetu hata km ni wa team tofauti na yko.

jf tunapita tu!
 
Last edited by a moderator:
Ingekuwa wao zingefunguliwa nyuzi hamsini, sijui wanashindanaga kufungua nyuzi wale watu, Kiba anajitambua thats why anaongelewa na watu wanaojitambua kama sisi(km namuona mwafulani na booonnge la sonyo), hahahaaaa King wakae mbali na wewe kwakweli

sisi tunajielewa kama king hatufungui uzi kimyakimya
 
Back
Top Bottom