Ali Kiba Fans' Special Thread...

Ali Kiba Fans' Special Thread...

Mtani badilisha avatar...!
Teh Teh...namimi nimeiangalia hiyo video kwa hiyo nimesaidia kuongeza ...and i did it for you...Teh Teh...

Hahahaaaaaa!!! Hiyo avatar its there to stay aisee, nikibadili ujue namuweka huyohuyo ila picha tofauti, huoni tumemotivate watu nao kuweka picha,
Hasante sana mtani wangu hebu kaangalie tena uje tucheketue vizuri.
 
we hukuwepo kwenye uzi wa aly kua balozi wa wanyamapori yani kiba amenifanya nipate ban kwa mara ya kwanza..halafu wiki nzima imeisha last week...!yani bado hoja zilivyowazidi wakamuingiza mama angu,wakaja na baba angu dahhh...
nilichoka sana!!ila nimejifunza kitu kua kuna watu matusi haswa ya wazazi ni sehemu ya maisha yao bila kutukana hawaishi...

yani that day nilijua kweli kuna watu hua wanakuchukia mtu even if natumia fake id,hunijui sikujui na wengine walifurahi sana mie kupigwa halafu kumbe we waweza kua unachukulia ushabiki tu kumbe mtu hakupendi hadi moyoni daahh...!!
poleni wenye roho nyepesi...!$
Avemaria kumbe ulipigwa ban, aisee sikuona hiyo kitu, watu wanachukulia jf serious sn aiseee, wataishi maisha magumu sn.
 
Last edited by a moderator:
nifah ungestick tu to ur promise.

Kwamba ungerudi hapa baada ya mfungo.

Kinyume na hapo utakuwa wajishindisha njaa tu.

SORRY.

who ar u to judge people?afunge,ashinde na njaa we inakuhusu?
 
Last edited by a moderator:
aisee wanasema kiba ndo msanii anayetumia kiswahili fasaha kwenye mziki mfano "mwenda omo na tezi marejeo ngamani " anasema maana yake mwenye pupa hafanikiwi hta siku moja

Mrisho mpoto vp ila nackia pia kiba ndo msanii anaeogoza kuchukua tuzo nyingi bongo :what:
 
Yaani walitegemea magari ya kifahari na location expensive ila alichofanya meji alabi ni hatari, kachukua van moja model ya zamani na ile nyingine tulikuwa tunaita mgongo chura, pia kellys alifanya kazi nzuri kwenye kuvaa #vivakiba
peterchoka atoto cut b nifah unanitaka Avemaria@mdakuzi mwanaspot ni gazet la heshima sio la udaku jana wameandika hivyo ukisoma yaliyomo utazid kumpenda kibaaa
 

Attachments

  • 1435689413775.jpg
    1435689413775.jpg
    59.9 KB · Views: 56
  • 1435689436265.jpg
    1435689436265.jpg
    51.3 KB · Views: 54
  • 1435689453523.jpg
    1435689453523.jpg
    45.5 KB · Views: 48
  • 1435689473228.jpg
    1435689473228.jpg
    60.1 KB · Views: 51
  • 1435689491998.jpg
    1435689491998.jpg
    60 KB · Views: 61
Last edited by a moderator:
Hahahaaaaa!! Wazeee wa mashindano takwimu naona zimeanza, uwiiii Kiba nenda na watu taratibu jamani, sio kwa relay hiyo!!
 
Avemaria kumbe ulipigwa ban, aisee sikuona hiyo kitu, watu wanachukulia jf serious sn aiseee, wataishi maisha magumu sn.

kiba anaheshima na anaandikwa na magazet ya heshima atoto si umeona hawajaifungulia thread hiyo habari ingekuwa ni udaku ila cc wala tupo cool tu we love u kiba
 
Last edited by a moderator:
Isingekuwa sawa kwangu kuingia humu na kupita bila ya kuzungumzia habari kubwa iliyopo sasa juu ya ujio wa bonge moja la video la muziki wa Bongo Flava ambayo sio ya waimba muziki wa Naija. Na baada ya kusoma maoni ya baadhi ya watu, nimeona niseme jambo hili kidogo kabla sijaondoka humu.
Binafsi, nahisi sehemu kubwa ya jamii ya Kitanzania haina uelewa wa kutosha kuhusu video za muziki, hudhani ni kuweka tu matukio hata kama hayana maana, wala hayaungani na matukio mengine. Huamini kuwa, ubora wa video ni kuonesha magari ya kifahari na nyumba za kitajiri.
Kama si miongoni mwa watu niliowaeleza hapo juu, hutasita kutoa pongezi kwa video ya Chekecha Cheketua Kiba iliyochezwa kwa mara ya kwanza na kituo cha kimataifa cha runinga cha Trace Urbun, tena kwa namna inayoupa heshima muziki wetu na lugha yetu (swahili).
Kwa heshima zote nakubaliana na video ya Chekecha Cheketua, sio kwa ushabiki au kufuata mkumbo, bali kutokana na malengo ya video kukamilishwa vizuri na timu iliyoitayarisha video hiyo. Umakini wa props, maleba na mapambo ulikuwa ni mkubwa sana kiukweli.
Angalia magari yaliyotumika, angalia redio zilizomo humu ndani. Na sio ajabu Kituo kikubwa kama Trace Urbun kuamua kuipiga kama exclusive, na kupiga mara saba (7) ndani ya saa kumi na mbili (12) za siku moja, ambayo kwa hesabu za haraka, waliipiga kila baada ya saa moja na nusu.

Tueleweshane Kidogo!
Kwa wale waliobahatika kupata nafasi ya kuelimika, naamini watakuwa wakifahamu kuwa muziki ni fasihi. Na maana ya Fasihi ni utanzu (tawi) wa sanaa ambao hutumia lugha ya mazungumzo/vitendo au maandishi ili kufikisha (kuwasilisha) ujumbe fulani kwa hadhira husika.
Katika kazi yoyote ya fasihi lazima pawepo na ustadi wenye kuleta mvuto fulani kwa hadhira (wasikilizaji/watazamaji au wasomaji) husika. Na ustadi (ufundi) huo unaovutia hadhira ndio huitwa FANI, ambayo hujumuisha mambo kama vile:
  • Muundo (mtitiriko/msuko/mpangilio wa matukio/visa)
  • Mtindo (mbinu inayotumiwa na fanani ili atofautiane na fanani mwingine)
  • Wahusika (watu au vitu ambavyo hutumiwa na fanani katika kazi yake)
  • Mandhari (eneo ambalo fanani hulitumia katika kuumba kazi yake)

Vilevile kazi yoyote ya fasihi huwa na ujumbe na malengo mbalimbali ambayo hukusudiwa yaifikie jamii husika. Yale yote ambayo msanii wa kazi ya fasihi anakusudia yaifikie jamii husika, ndio huitwa Maudhui (content). Maudhui ya kazi ya fasihi hujumuisha:
  • Dhamira
  • Ujumbe
  • Migogoro
  • Falsafa/misimamo
  • Mtazamo

Kazi ya fasihi ni kujaribu kusawiri vipengele vya maisha, mahusiano, na hisia za watu katika jamii husika, ambayo huwasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo au vitendo. Na kuna aina kuu mbili za fasihi ambazo ni Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi.

Kisa cha kwenye video ya Chekecha!
Nampongeza mwandishi wa script, muongozaji na wawasilishaji kwa maana ya washiriki wote tuliowaona kwenye video hii. Tukirudi kwenye fasihi, maana (DHAMIRA) ya video hii kuelezea kwa vitendo 'NGUVU YA SANAA YA MUZIKI KWA JAMII'.
Kisa kiko hivi, Kiba anafika kwenye mji usio na maendeleo makubwa na wakazi wake hawako huru kufanya majukumu yao (kutengeneza gari/mke na mume kufunguliana milango ya gari), kufanya wapendacho (kushiriki michezo kama karata/gofu, kusikiliza redio) na kunyimwa haki ya kuzungumza, kwani wako kwenye amri ya kuganda (MIGOGORO).
Na kwa kawaida amri hutolewa na utawala. Kiba anashangazwa sana na hali hiyo, hivyo kuonesha kuwa ndio kwanza anakutana nayo kwa mara ya kwanza. Moja kwa moja anaamua kuwakomboa kwa kutumia silaha ya muziki (sauti ya kumtoa nyoka pangoni), anawaimbia na wote kuwatoa kifungoni.
Hapa ana lengo la kutueleza (UJUMBE) muziki unavyoweza kutumika kutatua migogoro (vita/uonevu) mikubwa ya kiutawala na kufanya dunia kuwa huru. Hatimaye kwa kutwa moja tu, mji ulioonekana kutokuwa na watu (mpweke) ukaonekana kujaa watu wakicheza na kushangilia huku wengine wakibaki kuwa mashabiki.
Kuna kitu cha kupongezwa sana nimekiona kwenye video hii, ambacho ni kukwepa kuonesha tabia za Kimagharibi, kama mavazi, uchezaji wa mitindo ya kuhamasisha ngono, na badala yake kuonesha Uafrica wetu (FALSAFA/MISIMAMO) na taratibu zetu.
Namsifu sana muongozaji wa video hii Meji Alabi kwa kuifanya video isiwe kwenye muonekano wa video za muziki wa Nigeria, na kufanikiwa kuilinda Bongo Flava na zaidi dansa wa Kitanzania, Kellz Mbowe kuwa ndiye dansa aliyeonekana zaidi (ndiye yule aliyefungua boneti ya gari).
Ukirejea maelezo haya utagundua kwamba, kilichofanyika kwenye video ya Chekecha Cheketua kilifuata misingi ya Fasihi kwa umahiri mkubwa, kuanzia Muundo, Mtindo, Wahusika na Mandhari.

Ova
 
peterchoka atoto cut b nifah unanitaka Avemaria@mdakuzi mwanaspot ni gazet la heshima sio la udaku jana wameandika hivyo ukisoma yaliyomo utazid kumpenda kibaaa

Ngoja nikaisome online, nione namna wenye utimamu wao wanavyomuongelea King, maana watoto wa BRN hata hawajui wanaongelea nn ni mihemko tuuuu, king ni badest news wallah!
 
Last edited by a moderator:
Yeah tena wanashangaa hatari, hiki kipaji sio cha kupoteza hataaaa kwa bahati mbaya kwakweli, hiki ndicho kipaji cha kujivunia kama nchi haswaaaaaaa!

haswaaa kibaaaa
 
kiba anaheshima na anaandikwa na magazet ya heshima atoto si umeona hawajaifungulia thread hiyo habari ingekuwa ni udaku ila cc wala tupo cool tu we love u kiba

Ingekuwa wao zingefunguliwa nyuzi hamsini, sijui wanashindanaga kufungua nyuzi wale watu, Kiba anajitambua thats why anaongelewa na watu wanaojitambua kama sisi(km namuona mwafulani na booonnge la sonyo), hahahaaaa King wakae mbali na wewe kwakweli
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom