Hahahaaaaa! We si uliambiwa coming sooon?? Kwani soon ni lini? Tuisubiri hiyo soon ifike, kiba ashapoteza mashabiki wake wa ukweli wengi tu ila hajui, ngoja ajazwe upepo tu na mamluki wa insta ajione kamaliza.
Achaga hizo jamaa yangu.
Chekecha cheketua tunaitaka sana......kwani hujui kuwa hii nyimbo inatakiwa ije ichukue tuzo zaidi ya tano?!
Kutoitolea video ni kuipoteza kwa makusudi!
Achaga hizo jamaa yangu.
Chekecha cheketua tunaitaka sana......kwani hujui kuwa hii nyimbo inatakiwa ije ichukue tuzo zaidi ya tano?!
Kutoitolea video ni kuipoteza kwa makusudi!
We abou wewe si uliaga lkn? Inatosha sasa kalale ujumbe ashaupata, asipoufanyia kazi tena sijui kwakweli, ila pia tusimpe pressure sn ataharibu, atulize kichwa afanye vya msingi, i'll always be his fan kwakweli ule muziki mtamu nauachaje kwa mfano?
Hahahaaaaaaa!! Unaanzaje kuhama sasa, huu mziki mzuri umuachie nani? Hatuyumbishwi siye pa ukweli tunasema alafu life goes on like nobody's business, hatufugi ujinga na anafiki usio na msingi hao ndio mashabiki wa ukweli ati, Kiba anapaswa ajivunie sie sn.
hahahaaaaaaa!! Unaanzaje kuhama sasa, huu mziki mzuri umuachie nani? Hatuyumbishwi siye pa ukweli tunasema alafu life goes on like nobody's business, hatufugi ujinga na anafiki usio na msingi hao ndio mashabiki wa ukweli ati, kiba anapaswa ajivunie sie sn.
well its nobody's business, we are just keeping it real! Kiba is our boy, sisi ndiye tunajua tunapata nini.hizi bataz za mtaa wa pili just dont matter.
Achaga hizo jamaa yangu.
Chekecha cheketua tunaitaka sana......kwani hujui kuwa hii nyimbo inatakiwa ije ichukue tuzo zaidi ya tano?!
Kutoitolea video ni kuipoteza kwa makusudi!
Avemaria karibu mamii, leo ilikuwa ni "truth be told" tulikuwa tunamuweka kijana sawa ili achangamkie fursa, now we r waiting for good things from him maana milango ishafunguka kazi ni kwake kupita afanye wonders.
well its nobody's business, we are just keeping it real! Kiba is our boy, sisi ndiye tunajua tunapata nini.hizi bataz za mtaa wa pili just dont matter.
Hahahaaaaaa!! They didnt mata then how ll they mata now??? Nakumbuka kale kamsemo ka Matola eti wanajitekenya na kufanya nini......? Wanadhani na sie wanafiki km wao eti, now the game gooooooooz on ama nene! Yaani hivyo tu yaani
VITA! Saa chache tu baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar akitokea nchini Marekani kwa shughuli za kimuziki, staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ametangaza kile kinachotafsirika kuwa ni vita dhidi ya hasimu wake kwenye anga la muziki huo, Nasibu Abdul Diamond Platnumz, Ijumaa Wikienda lina full stori.
Staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba.
TUJIUNGE ENEO LA TUKIO
Ali Kiba alitema cheche Alhamisi ya wiki iliyopita ndani ya Hoteli ya Sea Cliff, Masaki jijini Dar, kulikokuwa na uzinduzi wa kampeni ya kupinga vita ujangili, iliyoratibiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, huku akiwa ni mmoja wa mabalozi sanjari na mlimbwende wa zamani, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi K-Lyin.
Nasibu Abdul Diamond Platnumz.
USO KWA USO NA PAPARAZI
Baada ya shamrashamra za event hiyo, haraka sana kama mshale wa Mmakonde, mwandishi wetu alimfuata Ali Kiba, lengo kuu likiwa ni kusikia chochote juu ya ushindi wa Tuzo za Kili ambapo alizoa tano binafsi na moja ya kushirikishwa.
Kiba alisema anaamini alistahili kushinda tuzo zote kwani vigezo na sifa anazo na amejiandaa kikamilifu kupambana na yeyote anayedhani kuwa ni mfalme wa muziki huo.
JINA LA DIAMOND LAMCHEFUA!
Katika mahojiano hayo, mwandishi wetu alimkumbusha Ali Kiba uwepo wa Diamond ambapo kwa haraka sana alimkata kauli mwandishi kwa kusonya na kuweka wazi kuwa miongoni mwa mambo ambayo humpa kichefuchefu, ni pamoja na kusikia jina la Diamond likitajwa mahali popote penye uwepo wake!
Kaka, sitaki kabisa kulisikia jina hilo, linanipa kichefuchefu, unajua kwa kipindi ambacho nilikaa kimya, nilikuwa nausoma mchezo lakini hakuna aliyeweza kuchukua kiti changu na kuamua kurejea ulingoni kwa kishindo na kuanzia sasa hivi ni mapambano mwendo mdundo, alisema Kiba na kuongeza:
Simaanishi kuwa hakuna msanii mzuri kama mimi, naomba nisieleweke vibaya, wapo lakini siyo huyo dogo (Diamond), muziki ni zaidi ya mbwembwe, niko kikazi na sasa nimedhamiria kweli, kama anaamini yuko fiti, kazi zitaweka wazi ukweli na si drama za kitoto.
VIPI KUHUSU YEYE NA WEMA?
Mwandishi wetu alitaka kujua kulikoni msanii huyo alimuweka Wema Sepetu kwenye ukurasa wake wa Instagram akimmwagia shukrani lukuki na si mtu mwingine?
Wema amekuwa ni shabiki wangu wa siku nyingi mno, alianza kunipenda kupitia wimbo wangu wa Hands Across the World (kwenye Project ya One-Eight) na kuanzia hapo amekuwa akinipa sapoti kubwa sana, siwezi kukaa naye mbali eti kisa huyo jamaa (Diamond).
Naamini kwa asilimia nyingi sana hata huu ushindi wangu wa tuzo, umechangiwa na sapoti yake pamoja na wadau wangu wengine, alisema Kiba.
AFUNGUKA KUHUSU VIDEO YA MWANA!
Pia, mwandishi wetu alimtaka staa huyo kufafanua madai ya kutoitendea haki video ya Wimbo wa Mwana, ambapo alisema, watu wengi walitarajia aifanye kulingana na mawazo yao ndiyo maana akaamua afanye vile anavyoaamini ingekuwa bora.
Kila mtu alikuwa ameshatengeneza picha ya jinsi video ya wimbo itakavyokuwa, halafu sifanyi kazi kwa kushindana na mtu, ndiyo maana ilionekana tofauti na mawazo ya wengi, namalizia kwa kusema salamu zimfikie jamaa (Diamond) kuwa mapambano ndiyo kwanza yameanza, alisema Kiba.
DIAMOND ANASEMAJE?
Hadi tunakwenda mitamboni, jitihada za kumpata Diamond aweze kuzungumzia vita hiyo iliyofufuka upya hazikuzaa matunda kufuatia simu ya staa huyo aliyekuwa nchini Afrika Kusini kikazi, kuita bila majibu. TUJIKUMBUSHE
Kwa muda mrefu sasa, Kiba na Diamond wamekuwa wakiripotiwa kuwa na bifu la chini kwa chini linalotokana kugombania ufalme wa muziki Bongo.
Ananijitekenya na kujijambisha mwenyewe lazima amchukie Daimond Kwan hatujui Hilo sio geniii,hasira zake za kukosa pesa ya kumalizia video ya cheketua asmmalizie Daimond,atakunya huku kasimama shenziiiiiiiii!;;;;;!!!!!!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.