Ni kweli tupu my
nifah sio mda wote tupo kishabiki na hasa kwa mziki wetu Tanzania. Ila kwa vile unamkubali mtu flani ukishauri kwa nia njema watakuona we ni hater unamuonea wivu na mafanikio yake, wakati mi namuona bado ana safari ndefu.
Hilo tatizo la sifa zisizo na msingi ni tatizo kwake nakumbuka kipindi kile kashinda tuzo Nigeria na ambapo DAVIDO hakushinda nakumbuka Idriss naye alishinda BBA. Sasa domo yeye huwa anafata upepo wa mashabiki bila kupima vitu kwa umakini. Alivoona Davido kaandika statement kuwa time cheat again na ilikua nadhani utani Domo kajiingiza moja kwa zote. Misifa ya kijinga jamani ina mucost sana na kujiona yeye ni top hakuna ka mwingine na kuamua kujiongelea tu bila kufikiria side effects zake.
Hafu tatizo la kuwakashifu wanawake bila sababu limemshushia credibility sana tu Mara Leo yuko hapa kesho kule na kuanza kuwazalilisha hajui kua kwenye jamii wanawake ndo huwa wana support sana kila sector kwa wingi wao na ndo wapiga wazuri. Sasa yeye sijui ndo huwa kiki zake kuwaongelea ma ex na jamii yoyote haipendi tabia chafu za uhuni uhuni, hasa kuzalilisha wanawake eti makombo.
Kikubwa ajiangalie nyendo zake kwa makini atajishusha mwenyewe kwa matendo yake mwenyewe ana safari ndefu. Na aogope mashabiki wa kumsifia bila kumu criticize sio wote wanaompa negative comment ni haters wengine wanazichukuaga na kuzifanyia kazi hadi wanakua best.