Ulimboka alisema atatoa ya moyoni na kweli akayatoa kupitia wakili wake na hakuna lilofanyika,kibanda nae anajua kabisa waliohusika na tukio lake na yeye alisema soon ataweka kila kitu wazi na matokea yake kaenda ikulu kuonana na makamu wa rais,na sasa lwakatare nae anasema alhms ataweka yaliyomoyoni ili ulimwengu ujue what real happend,"nilishikwa siku 6<11/03/2013 baada ya kibanda kutekwa na leo nimetoka siku 6<11/06/2013 baada ya kibanda kurejea toka kwenye matibabu" na kama ilivyo ada Chadema huwa tuna msemo wetu"tulianza na Mungu na tunamaliza na Mungu"
ndugu yangu lwatakare najua wewe uliumia zaidi yetu sisi japo wengine tulifunga kwa maombi kwa ajiri yako sababu tunajua kabisa umeonewa kwani baada ya mda yale mashitaka ya director wa movie yako yalitupwa mbali na mahakama kuu na sasa kesi ya msingi iliyobakia ni ile ya kutishia japo nayo ilipigwa dana dana kibao ila Jopo la mawakili nguli halikukata tamaa kufatilia kesi yako na hatimaye leo hii12/06/2013 uko uraiani,nyumbani kwako wamejaa ndugu na jamaa kuja kukupa pole ila vichwani mwao na hata katika pole zao wanatamka jina la Mandevu"pole ndugu yangu ila huyu mandevu ipo siku yake" hao wageni wamejengewa chuki ya kulipiza,ebu basi niko chini ya miguu yako msamehe huyu mtu,toa yote yaliyo moyoni mwako na mwisho maliza na ile kauli ya chama pamoja na neno "nimemsamehe kwa moyo wa dhati kwani hajui alitendealo" na hapo Mungu atamaliza nae kwani wewe ulianza na Mungu since day1 ulipopelekwa JELA.Amina