Alhamisi nitafunguka-Lwakatare

Status
Not open for further replies.
...
...
...

Wakati hayo yakiendelea mtandao wa You Tube unamuonyesha Naibu Katibu Mkuu CCM Mwigulu Nchemba akitamba kwenye kampeni za udiwani Arusha kwamba ndiye aliyegharamia vifaa vyote vilivyotumika kumrekodi Lwakatare na hatimaye mateso yote yaliyomfika Lwakatare.
...
...
...

Source:Tanzania Daima.
Hivi hii nchi ina Polisi kweli?? Kwa hii kauli angekua labda ni Lema ndo kaongea angeshakamatwa!!

Kweli Mwigulu ana roho mbaya aisee
 
Kama ametoka mahabusu atulie tu na familia yake. Kuropoka kutamfanya apate majanga mapya kabisa.
Familia yake ipi? inaonesha jinsi mwenzetu ulivyoshiba. Kama akina Mandela wasingeropoka wasingepata umaarufu huu. Endelea tu dada kupumzika, sisi tutapambana na kuhakikisha familia na vizazi vyetu vijavyo vinafaidika na raslimali za ardhi yetu. Endelea kupunga tu upepo, maana wapenda starehe lakini kumbuka hutakumbukwa kwenye historia kama Rwakatare.
 
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfred Lwakatare amesema atatoa ya moyoni siku ya Alhamisi.

Akizungumza na waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi mara baada ya kupata dhamana aliomba subira kwa watanzania kwani anayo siri nzito moyoni.

Lwakatare alisema anawaomba waandishi wa habari watulie kwani anatarajiwa kuzungumza kwanza na viongozi wake wakuu wa chama na jopo la wanasheria wake nguli ndipo azungumze na dunia.

Wakati hayo yakiendelea mtandao wa You Tube unamuonyesha Naibu Katibu Mkuu CCM Mwigulu Nchemba akitamba kwenye kampeni za udiwani Arusha kwamba ndiye aliyegharamia vifaa vyote vilivyotumika kumrekodi Lwakatare na hatimaye mateso yote yaliyomfika Lwakatare.

Viongozi wakuu wa Chadema tayari wameelezea furaha yao baada ya Lwakatare kupata dhamana.Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe yuko Dodoma katika vikao vya bunge wakati Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa yuko kwenye ziara ya kichama barani Ulaya.Katika salamu zake jana alizozitoa akiwa Ujerumani Dr Slaa alimpa pole Lwakatare na hapo hapo kuelezea furaha yake na ya watanzania wanaoishi Ujerumani kwa Lwakatare kupata dhamana na kuweza kuungana na familia yake tena baada ya mateso ya miezi mitatu.

Source:Tanzania Daima.
Molemo
Waambie wanazi wenzako babu yupo matibabuni ujerumani; usidanganye watu yupo kwenye ziara ya kichama ulaya; mtaongopa mpaka lini?
 
Last edited by a moderator:
Slaa alihangaika weeee kuanika mafisadi lakini hakuna chochote cha maana alicho-achieve
bado naamini kuwa wewe ni inteligent na uko-well informed na siasa zetu na maendeleo kwa ujumla but leo unaniangusha. Slaa hana personal objectives katika harakati zake na chama chake dhidi ya mafisadi. Nafaham kuwa unalijua hili. Ndo maana nasema umeniangusha dadaangu
 
Hakushinda kesi, bali katoka kwa dhamana, kama sheria inavyoweka, kitu cha kujiuliza ni ilikuwaje huyu Bw aliweza kurecodiwa, na yeye is head of security. Ni mzembe wa aina gani, and in his own house hicho halisameheki. Chadema should take him to task, kwani yeye ndie anayepaswa kuhakikisha anachunga siri za chama hazitoki, na pia anasimamia upelelezi wa vyama vingine katika mambo yao ya siasa, ili kuweza kukipa chama chake kuwa na advantage ya kujua nini kinaendelea kwa wapinzani wao. Leo unarekodiwa nyumbani kwako ukuzungumzia mambo ya kutekeleza ujangili. How stupid, Na bado mnataka kusema he is innocent, Watanzania sio wapumbavu wa hivyo.

Mtakuja na kila aina ya ID lakini hamtafanikiwa.
 
Hivi yule msaidizi wa Lwakatare aliyekuwa anaonyesha alama za Chadema mahakamani naye katoka.
 
Molemo
Waambie wanazi wenzako babu yupo matibabuni ujerumani; usidanganye watu yupo kwenye ziara ya kichama ulaya; mtaongopa mpaka lini?

We mbunye kweli, mbona huna fikra hivyo?
ikiwa lengo kuu la safari lilikuwa ziara thena akaamua afanye pia matibabu kuna tatizo wapi? we hujawahi kwenda sehemu kwa ajili ya jambo 1 lakini ukafanya mambo zaidi ya yale uliyoendea ingawa lengo kuu lilikuwa lingine?

Poor chama,
Poor thinking,
Poor CCM!
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom