Alhamisi nitafunguka-Lwakatare

Alhamisi nitafunguka-Lwakatare

Status
Not open for further replies.
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfred Lwakatare amesema atatoa ya moyoni siku ya Alhamisi.

Akizungumza na waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi mara baada ya kupata dhamana aliomba subira kwa watanzania kwani anayo siri nzito moyoni.

Lwakatare alisema anawaomba waandishi wa habari watulie kwani anatarajiwa kuzungumza kwanza na viongozi wake wakuu wa chama na jopo la wanasheria wake nguli ndipo azungumze na dunia.

Wakati hayo yakiendelea mtandao wa You Tube unamuonyesha Naibu Katibu Mkuu CCM Mwigulu Nchemba akitamba kwenye kampeni za udiwani Arusha kwamba ndiye aliyegharamia vifaa vyote vilivyotumika kumrekodi Lwakatare na hatimaye mateso yote yaliyomfika Lwakatare.

Viongozi wakuu wa Chadema tayari wameelezea furaha yao baada ya Lwakatare kupata dhamana.Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe yuko Dodoma katika vikao vya bunge wakati Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa yuko kwenye ziara ya kichama barani Ulaya.Katika salamu zake jana alizozitoa akiwa Ujerumani Dr Slaa alimpa pole Lwakatare na hapo hapo kuelezea furaha yake na ya watanzania wanaoishi Ujerumani kwa Lwakatare kupata dhamana na kuweza kuungana na familia yake tena baada ya mateso ya miezi mitatu.

Source:Tanzania Daima.

ile video ya bukoba inamuonesha sana LWAKATARE akipanga njama za kumdhuru DENIS MSACKY, mbona amekimbilia kuhusisha kukamatwa kwake na Kibanda na siyo MSACKY? Anataka kukwepa nini hapa, hana jipya asitake kutuhadaa watanzaia wenye akili timamu, awafurahishe wapambe wake ila watanzania wapenda amani tutaendelea kumtambua kama Gaidi
 
Slaa alihangaika weeee kuanika mafisadi lakini hakuna chochote cha maana alicho-achieve
Kwisha habari yake huyu mzee, kwa mjibu wa rasimu ya katiba mpya hana sifa za kuwa rais wa Tanzania, labda awe rais wa wachagga wanaomtumia kama kibaraka
 
Tanzania daima.
Dr ameongea na watanzania wanaishi ujerumani kuonyesha furaha yake kwa Rwakatale kuwa huru.
Viongozi wa juu dr Slaa na Mbowe.
 
mkuu kumbe chanzo cha habari tanzania daima kwa heri mkuu.

Ivi buku saba mnazopewa huwa haijalishi umeandika nini?haya yamezungumzwa live mahakamani na Lwax baada ya kuachiwa huru, halafu jitu linaisema vibaya Tanzania Daima.
 
Ivi buku saba mnazopewa huwa haijalishi umeandika nini?haya yamezungumzwa live mahakamani na Lwax baada ya kuachiwa huru, halafu jitu linaisema vibaya Tanzania Daima.

Jifunze kuheshimu maoni ya wenzako. Kama hana imani na hilo gazeti, ni vigumu sana kumlazimisha awe nayo.
 
hujitambui wewe,Mwigulu kapata Aibu sasa anaomba msamaha
kweli sikio la kufa halisikii dawa, hivi kuwekewa dhamana ndiyo kushinda kesi kweli? Kupata dhamana ni haki yake, ila kamwe hawezi kukwepa kifungo huyu, kaingia mkenge na kutumiwa kama chambo na wachagga, haoni mwenzake SLAA anatumiwa lakini anakuwa mjanja, anawapa masharti ile mbaya.
 
Kama ametoka mahabusu atulie tu na familia yake. Kuropoka kutamfanya apate majanga mapya kabisa.

Furaha ya watanzania hasa wapenda haki ni mtu anayetuhumiwa kwa ugaidi kupata dhamana.
Watanzania wanapenda kujua ukweli ni upi na uwingo ni upi.
Baada ya hapo unaweza ukamwambia sasa akatulie na familia yake kwa muda halafu mchakato wa ukombozi unaanza na kuweka kumbukumbu sahihi kwa vizazi vijavyo
 
Terrorism na treason ni kesi ambazo hazina dhamana. Lwakatare anashtakiwa kwa kesi gani?
 
Jifunze kuheshimu maoni ya wenzako. Kama hana imani na hilo gazeti, ni vigumu sana kumlazimisha awe nayo.

mkuu hicho chama kipo hai kwa sababu ya propaganga za Tanzania Daima, lazima waumgurume gazeti lao linapoguswa, nathamani amani itoweke halafu watu wapelekwe the hague tuone kama mkurugenzi wa freemedia atasalimika.
 
Slaa alihangaika weeee kuanika mafisadi lakini hakuna chochote cha maana alicho-achieve

I absolutely agree na watu wanaosema kuwa kushabikia CCM ni lazima uwe na akili za maiti......unadhani awareness ya watanzania kuhusu kupigania rasilimali zao sio zao la Dr.Slaa na CDM kuanika ufisadi na mafisadi?
 
Terrorism na treason ni kesi ambazo hazina dhamana. Lwakatare anashtakiwa kwa kesi gani?
Wewe hauana akili, kuna sehemu nimetaja ugaidi hapo? Kwani wote waliofungwa wamefungwa kwa kosa la ugaidi? Ndo mnajifariji hivyo siyo? Ana kesi ya kujibu ndiyo maana hajaachiwa huru bali kawekewa dhamana tu mkuu.
 
Huyo Kibanda mwenyewe alirudi na mbwembwe nyiiingi. Ooh nitawataja ooh nitawaweka hadharani. Kiko wapi sasa kudadadeki?

Ndiyo tatizo la wabongo na matambo mengi halafu zero!
Ulimboka naye kaahidi kusema ya moyoni, mpaka leo kimya!

Ila naamini Lwakatare ataropoka ukweli we subiri
 
Kama ametoka mahabusu atulie tu na familia yake. Kuropoka kutamfanya apate majanga mapya kabisa.

......inaonekana usiku wa leo umenyimwa unyumba ndo mana una comment upimbi asubuh asubuhi,bora ungekaa kimya tu.
 
Wewe hauana akili, kuna sehemu nimetaja ugaidi hapo? Kwani wote waliofungwa wamefungwa kwa kosa la ugaidi? Ndo mnajifariji hivyo siyo? Ana kesi ya kujibu ndiyo maana hajaachiwa huru bali kawekewa dhamana tu mkuu.

Lwakatare alikamatwa kwa kosa gani?
Mara chache jaribu kuficha upumbavu wako uje kama GT
 
  • Thanks
Reactions: Pai
Furaha ya watanzania hasa wapenda haki ni mtu anayetuhumiwa kwa ugaidi kupata dhamana.
Watanzania wanapenda kujua ukweli ni upi na uwingo ni upi.
Baada ya hapo unaweza ukamwambia sasa akatulie na familia yake kwa muda halafu mchakato wa ukombozi unaanza na kuweka kumbukumbu sahihi kwa vizazi vijavyo

wewe haujui chochote kuhusiana na sakata la LWAKATARE. Kesi ya ugaidi alishafutiwa sasa hivi ana kesi ya jinai ya kupanga njama za kutaka kuteka watu na kuwadhuru.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom