Alhaji Mussa Salum: Mwezi haujaonekana

Alhaji Mussa Salum: Mwezi haujaonekana

Mdau kabla ya teknolojia kukua waislam walikua wanafunga na mwezi wanauona,jaalia zama hizo hakukua na simu wala vyombo vingine vya kielectronic.Suala la mwezi kwa waislam lina maelezo yake.Waislam tumeambiwa tufunge kwa kuuona mwezi na tufungue kwa kuuona mwezi.Na kama siku ya 29 hatujauona basi tukamilishe 30.Pamoja na hayo pia wapo wanaoamini kuwa mwezi ukiandama sehem yeyote duniani mtu akisikia umeandama na afunge au afungue.Lakini mambo haya yatafanyika iwapo watu watakua na mawasiliano,je zama hizo zisizokuwa na mawasiliano??mfano mwezi umeandama Indonesia watu wakaambiwa kuwa mwezi umeandama huku kwetu.Sasa ungekua umeandama huko na mawasiliano hakuna wa huku wangejuaje?Ndo hapo inakuja ile dhana ya "Fungeni kwa kuuona na mfungue kwa kuuona,msipouona basi mkamilishe siku 30".Kwangu mimi waliotungua leo sina tatizo nao maana wao wanaamini kuwa ukipata taarifa kuwa mwezi umeandama any where in the world ww fungua.Ila kwangu mimi nachoamini ni kwamba as long jana sijauona basi leo nakamilisha 30.
Turudi kwako sasa,wewe unakwazika wapi mdau?
Ijumaa njema
Mimi ni mkristo lakini kwa maelezo yako hayo nimeona mambo mawili:-
1-Wewe ni mcha mungu wa kweli
2-Busara na Hekima umepewa.

Nasema hivi kwasababu mtoa mada ametoa ktk hali ya hasira na chuki nyingi kiasi kwamba mtu asiyemvumilivu angemjibu kwa hasira na maneno mabaya.

Mungu azidi kukupa Hekima zaidi na thawabu kwa yale yote yampendezayo kwako
 
Kwa akiri ya kawaida utaona hakuna Mungu hapo! Mungu na sayari wapi na wapi...! Ata mfalme keizer alikuwa ana abudu jua badae akamng'amua Jesus akaondokana na ushwetani ebu mtiini Yesu mtayaona mengi.
 
Ni kweli hainihusu kiimani maana mimi na mwezi wapi na wapi shida impacts zake kwa nchi au jamii maana inatambulika kitaifa maofisi huwa hayafanyi kazi sasa hapo kwenye kujua ni sikukuu au la! Ndipo hapo kero yao...!

Wewe na Uislam au Nchi nani mwenye umri mkubwa mpaka utake uje urekebishe leo, Umezaliwa utamaduni huu umeukuta waachie, waendelee, Jamani Dini sio siasa ni kuamini, ndo maana wewe sio Muislamu kwa sababu ya hizo unazoziona kama kasoro. Na hata wao ndiyo maana sio Wakristo ni kwa sababu hizo hizo wakati wewe ukiona kila kitu kiko sawa ndani ya ukristo, lakini ukita uone utofauti hata ndani ya hizi imani yetu, bado kuna madhehebu ni kuonyesha utofauti ndani ya imani, acha waaminio waamini, siasa ndiyo pekee inaruhusu mwanacha wa cha kingine kukitolea maoni chama kingine, ila dini. Labda kama hujui maana ya imani, wewe ndo uje leo tena ukitumia jina bandia eti unataka watu kubadilisha imani za watu, unarudi kulekule, kila ainie huamini anachomini ndicho sahihi.
 
Mimi ni mkristo lakini kwa maelezo yako hayo nimeona mambo mawili:-
1-Wewe ni mcha mungu wa kweli
2-Busara na Hekima umepewa.

Nasema hivi kwasababu mtoa mada ametoa ktk hali ya hasira na chuki nyingi kiasi kwamba mtu asiyemvumilivu angemjibu kwa hasira na maneno mabaya.

Mungu azidi kukupa Hekima zaidi na thawabu kwa yale yote yampendezayo kwako
Nashukuru mdau,na mwezi huu ndo tunasisitizwa kuwa wachamungu zaidi ili baada ya mfungo tuendeleze tulojifunza ndani ya ramadhan japo wanadham hukengeuka ila RAMADHAN NI KAMA CHUO CHA KUKIFUNZA.DIni inafundisha subira na kuvumiliana ila kimaumbile wanadam hatuna subira na kuvumiliana imekua mtihani kwetu.Siku njema
 
Mimi huwa siwaelewi hawa jamaa zetu katika Mungu mmoja. Wao sikukuu yao kutegemea mwandamo wa mwezi si hoja kwangu ila hoja ya msingi ni shida na mahangaiko ya kuuona huo mwezi km umeandama.

Ebu mtuondoleeni uvivu wa kufikiri ktk zama hizi za sayansi na technolojia mnashindwa kuwa na technolojia ya kuona km mwezi umeandama au bado.

Maana huwa mnatusumbua ata wengine tusiokuwemo mtu unaamka hujui ni Eid au la! Unawaza uende kazini au vipi jamani ebu badirikeni kila kitu kinawezekana acheni uvivu.

Acha porojo wewe waislamu wanachombo chao na kimetangaza toka Jana kua Leo hakuna sikukuu na siku yakazi sasa sasa wewe hujaelewa nini!

Wewe subiri sikukuu zako ulizapangiwa tarehe na ma.bwa.na zako usherehekee yahuku hayakuhusu niheri upige kimya Tu!
 
Mimi shida yangu siku kuu yenu ina athari kwa mambo ya kitaifa mfano watu wanataka kujua km kuna kazi au hamna pia ukiacha wafanyakazi kuna wapokea huduma za mofisini, kuna wanafunzi yaani kiukweli ni shida tupu...!

Usiwe mvivu wa kufuatilia kwenye vyombo vya habari jana taarifa za habari za Itv na Azam zilizungumza kupitia shehe mkuu kuwa Leo itakua Ramadhani.

Tatizo bado munahangaika kumtafuta mgombea. Mengine yakiwapita msilalamike.
 
Nimekimbia riadha kama mwendawazimu kwa suala hilo hilo...wanaudhia sana..kama vipi iondolewe kwenye siku zinazo athiri siku za kazi kitaifa maana tutakuja fukuzana kazi.
Shit
 
Wapo wanaosema leo ni eid na wapo wanasema sio eid nimeshindwa nimwamini nani

ni EID kwa baadhi ya hao wanaofuata watu ... ila kwa serekali ya Tz leo sio EID ... kazi kama kawaida wadau ....
 
Uctoe sapot zczo na maana ili uonkane umesema kwny hoja tata..al had iwe ana kubalka au hakubalk haijalsh..ishu n kwamb wanaptsha ummah tena mchna kweupe..kukbalka kwke haina maana ypo sahh,mnaomkbal n watu kma ww ambao hamtak kfkiria zaid ya kawaida mliyoizoea..bakwata ni tatzo kwa waislam wa tz..aliwa muft acwe muft matatzo ya bakwata palepale..kwa sabb wanafuata mfumo na co dini..

Mbona unaandika kitoto namna hivyo? Hiyo keyboard yako ina matatizo gani? Si ajabu siku moja ukiandika barua ya kuomba kazi ukaandika hivyo hivyo.

Andika maneno kama yalivyo bwana acha hizo dot com.

Tiba
 
Yeye na wale anao wakokota kiimani waendelee kufunga, sisi wengine hatufungi wala hatufungui kwa maelekezo yake yeye, kwahiyo KESHO NI IDDI.

ndugu,kabla hujaandika tafakari kwanza,na hivyo hivyo kabla hujapost,hatupo hapa kwa ajili ya kutukanana....ANAEFUNGUA LEO AFUNGUE,NA ANAEFUNGA AFUNGE...Mbona kina Shafii na Maliki (awawie radhi M/mungu)hawajaishi hivyo???KAENI CHINI MSOME..
 
Kwa akiri ya kawaida utaona hakuna Mungu hapo! Mungu na sayari wapi na wapi...! Ata mfalme keizer alikuwa ana abudu jua badae akamng'amua Jesus akaondokana na ushwetani ebu mtiini Yesu mtayaona mengi.

Akiri = Akili
 
Kuna mwaka flan mwezi uligoma sasa...wakabidi waseme umeonekana masri yani misri......
 
Back
Top Bottom