Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhaji Musa Salum,kwa niaba ya Kaimu Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir,amesema kuwa mwezi haujaonekana na hivyo Waislam wataendelea na mfungo kesho.
Alhaji Salum amesema swala ya Eid itafanyika Jumamosi tarehe 18 na kimkoa itakuwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kitaifa ni mkoani Geita.
Chanzo: East Africa Radio
kutokana na kawaida yake hiki chombo BAKWATA kuwa kimya kwenye mas'ala ya waislam. lakini itakuwa ni ajabu kutoisikia BAKWATA kwenye hili la kufunga na kufungua Ramadan kwa waislam wa Tannganyika ikijitutumua kujionyesha kuwa IPO. LKN kumbe mioyoni mwa waislam HAIPO.
TUMEISIKIA JANA KWENYE VYOMBO VYA HABARI IKIJITUTUMUA NA KUSHADADIA KUHUSU MUANDAMO MWEZI. bakwata kwahili ndio tunawasikia na kuwatambua kuwa kumbeee MPOOO!!! HONGERNI SANA!!
Lakin kwenye mas'ala mengineyo haswa ya kila siku hususan kushughulikia suala la KAADH na MAHKAMA YA WAISLAM kwa hili hatuwaoni mkijitoa kimasomaso kama manavyoshupalia kuugawa mwezi eti mwezi wa kitaifa na Mwezi wa KIMATAIFA!!! kah!!!
hivii ni wapi pameandikwa au kulezewa kuwa hapa duniani kuna miezi TAIFA na MIEZI KIMATAIFA???
BAKWATA JICHUNGENI SANA.
HAYA!! JANA ALHAD MUSSA amesema swaum inaendelea na IDD itakuwa ni kesho j1. napata shida sana hapa mfano jirani zetu KENYA, UGANDA ambao yeye mwenyewe na shehe wake jana katika tv chanel10 wametueleza kuwa wanasali IDD leo hii IJUMAA. najiuliza! jee mikoa jirani mfano MWANZA, BUKOBA, KIGOMA wakisema wafuate taarifa za nchi jirani watakuwa wamekosea wakitoa taarifa kuwa jirani zetu wanasali SALA YA IDD leo IJUMAA?
Haya! kama issue ni kauli ya quraan inaposema kuwaambia waislam.. FUNGENI KWA KUUONA MWEZI NA FUNGUENI KWA KUUONA.
SWALI: huyu maamuma mlemavu wa MACHO aka KIPOFU anapataje taarifa ya kufunga kufungua iwapo yeye ni kipofu haoni kabsaaa!! hapa inakuwaje?
jibu: kwa vyovyote vile mlemavu huyu atatekeleza ibada ya kufunga baada ya kupewa au kupata taarifa kutoka kwa waliouona mwezi. je hatuoni kuwa hapa linaingia suala la kupata taarifa bila kuuona?
mtume muhamamad SAW Mtume Mtukufu amepokelewa akisema, ''Tafuteni elimu hata kama ni kutoka China. Hadithi hiyo kama zilivyo hadithi nyinginezo,
inasisitizia umuhimu wa elimu katika Uislamu. Sisitizo na ushawishi huo, kuhusiana na elimu, ndivyo vimewafanya Waislamu kutilia umuhimu na kufanya juhudi kubwa za kutafua elimu duniani. ili waweze kuwaelimisha maamuma wasiokuwa na uelewa huswusan katika hili la MFUNGO WA RAMADAN.
TUSIWAPUUZE HAWA WANAZUONI WANAOJITOLEA KUTUFUMBUA MACHO NA MASKIO ILI TUWEZE KUELIMIKA KUTOKANA NA WANAYOJIFUNZA.
TUAMKE WAISLAM WA TANGANYIKA.
Assalaam alaykum warahmatul llah wabarakatuh