MWALLA
JF-Expert Member
- Dec 12, 2006
- 16,952
- 10,512
"Tamko lisilo na mipaka maalum."
Ama jambo la kusema kila watu na mtenguko wao wa jua kwa hivyo wana wakati wao wa kuswali na kufunga (Swaum) ndio hivyo hivyo; ni vyema ieleweke hivyo ni vitu viwili tofauti. Swala imeambatana na mitenguko ya jua na Swaum imeambatana na kuandama kwa mwezi. Mas-ala ya nyakati za Swala yameshaelezwa na kufafanuliwa na Mwenyewe Mwenyezi Mungu katika Qur-aan na pia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amelibainisha kwa uwazi kabisa katika Hadiyth. Wala hakuna ikhtilafu yoyote mbele ya Wanazuoni juu ya jambo hilo. Ijmai ya Wanazuoni wamekubaliana kuwa kila sehemu, wala si kila nchi nzima inaweza kusali kwa wakati mmoja. Kwani mtenguko wa jua unaweza kutofautiana hata katika nchi moja. Angalia Dar es Salaam na Kigoma wanaswali na kufuturu tofauti, lakini wanafunga kwa mwandamo mmoja.
Kila sehemu itaswali kwa wakati wake kwa kutegemea mtenguko wake wa jua. Mwenyezi Mungu Amebainisha hayo katika Surat Bani Israil (17: 78) kama ifuatavyo:
{{أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَىٰ غَسَقِ اللَّيْلِ}}
{{Simamisha Swala jua linapopinduka (likaenda magharibi) mpaka giza la usiku.}}