Mh. Zito Katimuliwa Chadema, Atagombea Kupitia Chama Gani Hapo Mwakani? Kama Ni Cuf Au Nccr Mageuzi Vyama Hivi Vimeungana Na Vinaachiana Wagombea.Mfano, Iwapo Atahamia Cuf,je Chadema Jimbo La Kigoma Watakubali Kumuunga Mkono Mh Zito Yaani Chadema Isisimamishe Mgombea Jimbo Hilo La Kigoma Ili Kumuunga Mkono Zito? Na Je Cuf Itampokea Zito Ambae Alifukuzwa Kwa Madai Ya Kukisaidia Chama Cha C.C.M? Na Kama Itampokea Na Kumsimamisha Ubunge Na Chadema Isimuunge Mkono Zito Hapo Nini Kitatokea? Mi Naona mh. Zito Itabidi Ajiunge Na Vyama Visivyo Na Muungano Wa UKAWA.NAWASILISHA.
Mh. Zito Katimuliwa Chadema, Atagombea Kupitia Chama Gani Hapo Mwakani? Kama Ni Cuf Au Nccr Mageuzi Vyama Hivi Vimeungana Na Vinaachiana Wagombea.Mfano, Iwapo Atahamia Cuf,je Chadema Jimbo La Kigoma Watakubali Kumuunga Mkono Mh Zito Yaani Chadema Isisimamishe Mgombea Jimbo Hilo La Kigoma Ili Kumuunga Mkono Zito? Na Je Cuf Itampokea Zito Ambae Alifukuzwa Kwa Madai Ya Kukisaidia Chama Cha C.C.M? Na Kama Itampokea Na Kumsimamisha Ubunge Na Chadema Isimuunge Mkono Zito Hapo Nini Kitatokea? Mi Naona mh. Zito Itabidi Ajiunge Na Vyama Visivyo Na Muungano Wa UKAWA.NAWASILISHA.
Kama kweli ZZK anahusika na ACT ni wazi kuna tatizo, huwezi kuanzisha taasisi ndani ya taasisi nyingine tena kwa siri.
Wanaolifahamu hili na kulielewa wanajua kuwa huwezi kukaa na mwanachama wa namna hii. Ndio maana Mh. Kafulila alivyotofautiana na chama chake 'hakufungua ofisi' FB/Twitter bali aliomba msamaha na akasemehewa na sasa anajenga taifa.
Alafu kama huyu wakili kayaongelea haya kwenye hiyo radio ni wazi lao ni moja!
Zitto amevuna alichokipanda maana aliifahamu fika katiba ya CHADEMA lakini alipuuza. Sasa ni zamu ya Alberto Msando kufukuzwa CHADEMA ili waende kuimarisha chama chao cha ACT. Nani alisema CHADEMA haiwezekani bila Zitto? Hana nguvu yoyote chamani bali watu wanapenda Sera za chama na si mtu.
CHADEMA watamkumbuka sana ZITTO.
Mwanasheria feki huyu. Mh tundu ametoa kwenye katiba ya CHADEMA hakutunga yeye yakwambaaa mwana CHADEMA yeyote atakae shitaki mahakaman moja kwa moja atakua amejivua uanachama so huyu mwanasheria Alienda shule kafanya nn? Da!
Ha ha ha ,
mwiba ukiingia mwilini hautoki kirahisi,
kumbukeni maneno ya zitto,
Alisema atakuwa wa mwisho kutoka chadema kwa hiari yake,
mzee slaa nasikia yupo hoi anawaza zitto akienda chama kingine wamekwisha.
Hukumu ya mahakama ni mtego kwa CDM
hasa ukizingatia kuwa tuna michakato nyeti
yenye kuhitaji utulivu wa fikra katika vyama
vyetu.
CDM kama chama makini cha demokrasia
wangelimsamehe ZZK ili kuudhilisha kuwa
pamoja na njama,hujma na jitihada za kukidhoofisha
chama zinazofanywa na watu lakini chama bado ni imara
kuliko wanavyofikiria.
Msamaha kwa ZZK kwa CDM si jambo la ajabu bali ni
haki ya chama kutokumpoteza mwanachama wake aliyekuwa
mstari wa mbele katika mageuzi ya fikra za watanzania kupitia
siasa.
Kama inavyojulikana kuwa CDM ni mpango wa Mungu,chama
kifanye maamuzi magumu ya kumsamehe ZZK kwani ili mipango
ya Mungu ifanikiwe ni pawepo na vipingamizi vingi sana.
CDM kumfukuza ZZK ni sawa na kurudi hatua mbili nyuma
na ili kurejesha hali hiyo chama kitatumia rasilimali nyngi
sana ikiwemo matumizi ya nguvu yasiyo na ulazima wowote.
Huyu jamaa ni Hopeless kweli kauliza maswali ya Kijinga kweli kweli. mi hata sijui kama ana uwezo mzuri wa kumshauri zitto na tatizo kubwa la zitto ana washauri wahuni wahuni tu kama huyu jamaa. anasema nani anamfukuza zitto?
1. anasema kwa nini kama CHADEMA ni chama cha kidemokrasia kinaamuru tu afukuzwe kwa sababu ameenda mahakamani, hili si ni swali la kijinga kabisa? chama cha Kidemokrasia si kinafata katiba? katiba yao inasemaje?
2. mwenye mamlaka ya kumfukuza zitto ni katiba. katiba haiwez toa sauti hivyo mtu mmoja anaongea kwa niaba ya katiba na mwanasheria wa chama ni sahihi kuongea kwa niaba ya katiba
3.uamuzi wa kumfukuza unapaswa uwekwe wazi kama ambavyo yeye alipoweka suala hili kwa umma mahakamani na jinsi ambavyo lipo wazi ni kuwa alishajifukuza kwa mujibu wa katiba. Biblia inasema usiue ukiua tayari umejifukuzisha kwenye kusanyiko la watu wenye kuamini biblia hivyo haina haja tena ya kuja kukwambia kwa siri sababu toka mwanzo umejifunza biblia imeandikwa usiue
hizo points nyingine zimekaa kihisia zaidi kiasi kwamba hata najisikia uvivu kumjibu. huyu nadhani alitumwa tu kumsaidia zitto kuanguka naye zitto hakuwaza vizuri akaanguka kweli kwenye mtego huo mdogo wa kupitia msando