Albert Msando afunguka kuhusu Zitto Kabwe

Albert Msando afunguka kuhusu Zitto Kabwe

Watu Kama Hawa Ndio Wanatukatisha Tamaa Kusomesha Watoto, We Kasoma Mpaka Kapewa Chet Cha Uwakili Arafu Uelewa Wake Ndio Huu! Aisee Hii Ni Hatari.

Wao wanasema piga desa kupandisha GPA 😂😂:beer:
 
Zitto asamehewe chondechonde baba yetu mhe.Mbowe, wanachadema tusamehe na tusahau yaliyopita, zitto asamehewe bure bila masharti nawaombeni, tusimuache aende.

Mkuu unaemwombea hayo hataki hicho

Zito anajua anachokifanya

Hayuko chadema siku nyingi sana.

Hamumfahamu zito vizuri nyie
 
Nakuunga mkono

Ni kipengele kinacho mnyima mwana CHADEMA haki yake ya msingi ya kukimbilia Mahakamani

Ni kipengele cha "kishetani"

Jamani, kuwa mwanachama wa chamaa cha siasa ni tendo la hiari..Mahakama ya nini tena? Kama hao wenzio hawakutaki unatoka, unaenda kuanzisha chama chako...Mahakama ya nini hapo? Msajili wa vyama yupo...ni mtumishi wa umma, unaweza kwenda akakusajili ukaanzisha chama chako na hao unaokubaliana nao madhali unakidhi mahitaji ya sheria...Mahakama ya nini hapo?

Safari njema ACT ZZK kama hawajavurugana, otherwise ofisi za msajili zipo wazi...Anza ku-draft katiba ya chama chako kipya...Wewe si unajiitana wanakuita 'kichwa' 'kipanga', 'jembe' nakadhalika....? Mahakama ya nini?
 
Nn maana ya demokrasia?kma swala haljapatikana muafaka ndan ya chama hachukue hatua gan?katiba ya chama ni ya kidikteta nafkria inapnga wanachama kwenda mahakaman il iwakandamize kwa maslai ya wachache.shame chadema

Nasikia demokrasia ni kufuata taratibu mlizojipangia... kwani demokrasia inamsaidia mmoja tu?
 
Mkuu unaemwombea hayo hataki hicho

Zito anajua anachokifanya

Hayuko chadema siku nyingi sana.

Hamumfahamu zito vizuri nyie

wanataka kumtetea mwanamke aliyekolea kwenye kimchepuko chake kwamba arudishwe kwenye ndoa...
 
huyu wakili ni wale wachumia tumbo si ahaame chama kama anaona hakuna demokrasia.
 
Zitto amevuna alichokipanda maana aliifahamu fika katiba ya CHADEMA lakini alipuuza. Sasa ni zamu ya Alberto Msando kufukuzwa CHADEMA ili waende kuimarisha chama chao cha ACT. Nani alisema CHADEMA haiwezekani bila Zitto? Hana nguvu yoyote chamani bali watu wanapenda Sera za chama na si mtu.
 
Mkuu unaemwombea hayo hataki hicho

Zito anajua anachokifanya

Hayuko chadema siku nyingi sana.

Hamumfahamu zito vizuri nyie
Ha ha ha ,
mwiba ukiingia mwilini hautoki kirahisi,
kumbukeni maneno ya zitto,
Alisema atakuwa wa mwisho kutoka chadema kwa hiari yake,
mzee slaa nasikia yupo hoi anawaza zitto akienda chama kingine wamekwisha.
 
Zitto amevuna alichokipanda maana aliifahamu fika katiba ya CHADEMA lakini alipuuza. Sasa ni zamu ya Alberto Msando kufukuzwa CHADEMA ili waende kuimarisha chama chao cha ACT. Nani alisema CHADEMA haiwezekani bila Zitto? Hana nguvu yoyote chamani bali watu wanapenda Sera za chama na si mtu.
Kwani chadema wanasera gani ya maana zaidi ile ya maandamano.
 
Mwanasheria ambaye pia ni diwani kupitia CHADEMA, Ndugu Albert Msando amehoji yafuatayo;

1. Amehoji je, kama
CHADEMA kinasema ni Cha Kidemokrasia kwanini kinaaamuru Afukuzwe tu kwa kuwa ameenda mahakamani?

2. Amehoji je, ni nani mwenye mandate ya kumvua mwanachama uanachama wake.

3. Je, uamuzi wa kumvua uanachama ulipaswa kutangulia kwa umma au kwa Zitto kwanza?

4. Amehoji je, imekuwaje mtu anayesimamia sakata la Escrow afukuzwe kwa sasa?

5. Amesema pia kuwa Zitto hana haja ya kubaki
CHADEMA kwa kuwa hata akiomba kubaki haitakuwa na mashiko. Pia ameuliza itakuwaje akae meza moja na Tundu Lissu,Wakati Tundu Lissu anatangaza amesema walishamfukuza toka mwaka jana. Naye anaona kuwa Zitto hahitajiki CHADEMA.

6. Pia amesema lengo la kumfukuza Zitto limefanywa kinafiki tu.

7. Amesema kuwa haoni haja ya kulazimisha kila mtu awaze kama Tundu Lissu au Mbowe au Slaa.

9. Pia amesema kuwa mgogoro huu ni funzo kwa Zitto, Wanachadema na Watanzania kujua aina ya viongozi walionao.Pia amesema kuwa migogoro hii isitumike kujenga chuki.

Chanzo: Clouds TV

Nenda kanye uani wew naona mambo tayar huko kwenye surual,mchumia tumbo na mganga njaaa maaruf na cjui Tv gan hiyo ya UDAKU!!!
 
Na wasiwasi na vyeti vya huyo MWANASHERIA kama ni kweli amezungumza yeye itabidi taasisi husika zichunguze uhalali wa vyeti vyaka
 
Mh. Zito Katimuliwa Chadema, Atagombea Kupitia Chama Gani Hapo Mwakani? Kama Ni Cuf Au Nccr Mageuzi Vyama Hivi Vimeungana Na Vinaachiana Wagombea.Mfano, Iwapo Atahamia Cuf,je Chadema Jimbo La Kigoma Watakubali Kumuunga Mkono Mh Zito Yaani Chadema Isisimamishe Mgombea Jimbo Hilo La Kigoma Ili Kumuunga Mkono Zito? Na Je Cuf Itampokea Zito Ambae Alifukuzwa Kwa Madai Ya Kukisaidia Chama Cha C.C.M? Na Kama Itampokea Na Kumsimamisha Ubunge Na Chadema Isimuunge Mkono Zito Hapo Nini Kitatokea? Mi Naona mh. Zito Itabidi Ajiunge Na Vyama Visivyo Na Muungano Wa UKAWA.NAWASILISHA.
 
Ha ha ha ,
mwiba ukiingia mwilini hautoki kirahisi,
kumbukeni maneno ya zitto,
Alisema atakuwa wa mwisho kutoka chadema kwa hiari yake,
mzee slaa nasikia yupo hoi anawaza zitto akienda chama kingine wamekwisha.

Hivi wewe una akili kweli?

Kama anawaza hivyo basi asingefukuzwa.

Zito tumemfukuza...Hatumtaki CHADEMA...Aende chama chochote anachotaka
 
Hukumu ya mahakama ni mtego kwa CDM
hasa ukizingatia kuwa tuna michakato nyeti
yenye kuhitaji utulivu wa fikra katika vyama
vyetu.

CDM kama chama makini cha demokrasia
wangelimsamehe ZZK ili kuudhilisha kuwa
pamoja na njama,hujma na jitihada za kukidhoofisha
chama zinazofanywa na watu lakini chama bado ni imara
kuliko wanavyofikiria.

Msamaha kwa ZZK kwa CDM si jambo la ajabu bali ni
haki ya chama kutokumpoteza mwanachama wake aliyekuwa
mstari wa mbele katika mageuzi ya fikra za watanzania kupitia
siasa.

Kama inavyojulikana kuwa CDM ni mpango wa Mungu,chama
kifanye maamuzi magumu ya kumsamehe ZZK kwani ili mipango
ya Mungu ifanikiwe ni pawepo na vipingamizi vingi sana.

CDM kumfukuza ZZK ni sawa na kurudi hatua mbili nyuma
na ili kurejesha hali hiyo chama kitatumia rasilimali nyngi
sana ikiwemo matumizi ya nguvu yasiyo na ulazima wowote.
 
Back
Top Bottom