Alloyce PR
JF-Expert Member
- Nov 15, 2020
- 590
- 706
Uchambuzi wa Kikatiba chini ya Ibara ya 74(11) na (12) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977
Utangulizi
Demokrasia ya kweli hujengwa juu ya misingi ya kuheshimu Katiba, taasisi, na sheria. Katika muktadha wa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kuna umuhimu mkubwa wa kufanya tathmini ya nafasi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ndani ya mfumo wa kikatiba wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Makala hii inalenga kutoa tafakuri ya kitaaluma juu ya wajibu wa vyama vya siasa kuheshimu mamlaka ya Tume, kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 74(11) na (12) ya Katiba ya mwaka 1977, iliyorekebishwa mara kadhaa.
1. Mamlaka Huru ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa Mujibu wa Ibara ya 74(11)
Ibara ya 74(11) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasisitiza kwamba
"Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, Tume ya Uchaguzi haitalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote au idara yoyote ya Serikali, au maoni ya chama chochote cha siasa."
Tafsiri ya kifungu hiki ni kwamba INEC inatekeleza majukumu yake kwa uhuru na bila kuingiliwa na taasisi nyingine za Serikali au vyama vya siasa. Huu ni msingi muhimu wa kuhakikisha uadilifu wa mchakato wa uchaguzi. Katika mfumo wowote wa kidemokrasia, taasisi inayosimamia uchaguzi lazima iwe huru ili kutoa uwanja sawa kwa washindani wote na kulinda haki ya wananchi kuchagua viongozi wao kwa uhuru na haki.
Vyama vya siasa vinapaswa kutambua kuwa haki ya kuhoji au kupendekeza maboresho haimaanishi kutoa mashinikizo kwa INEC, bali kushiriki katika mchakato wa kisheria wa mapendekezo, ushauri, na maboresho ya mifumo ya kisiasa kwa kutumia majukwaa rasmi.
2. Ukingo wa Mamlaka ya Mahakama kwa Mujibu wa Ibara ya 74(12).
Katiba, kupitia Ibara ya 74(12), inasema:
"Hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii."
Hili ni agizo lenye uzito mkubwa wa kikatiba. Linamaanisha kuwa NEC inalindwa dhidi ya uchunguzi wa mahakama katika kutekeleza majukumu yake ya kikatiba. Hii ni hatua ya kipekee inayolenga kuhakikisha kuwa NEC haishinikizwi wala kuwekewa vizingiti vya kisheria vinavyoweza kuathiri uhuru na ufanisi wa kazi yake.
Hata hivyo, utetezi huu wa kikatiba hauondoi haja ya uwajibikaji wa INEC kwa umma kwa njia ya uwazi wa mchakato, weledi, na kuzingatia haki za wapiga kura. Kwa vyovyote vile, majukumu haya yanapaswa kutekelezwa kwa lengo la kujenga imani ya umma.
3. Ukomavu wa Kisiasa na Maadili ya Kidemokrasia: “Akili Kumkichwa”
Katika mazingira haya ya kikatiba, vyama vya siasa nchini vinatakiwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kutanguliza busara, hekima, na uzalendo. Kwa mfano, ni vyema vyama vikajizuia kutoa matamko ya kichochezi dhidi ya INEC au kutaka matakwa yao yatimizwe nje ya mifumo ya kisheria. Badala yake, hoja zao ziwasilishwe kupitia majukwaa rasmi ya kidemokrasia kama vile Bunge, na mijadala ya kitaifa.
Methali ya Kiswahili isemayo “Akili kumkichwa” ni wito wa kufikiri kwa kina kabla ya kutenda. Katika hali ya sasa, ni muhimu kwa vyama vya siasa kutafakari kama wanachokiomba kinatokana na maslahi ya taifa au ni mihemko ya kisiasa inayolenga manufaa ya muda mfupi.
Aidha, pale ambapo vyama vinaona mapungufu katika sheria au Katiba, yafaa watumie mifumo rasmi ya mapitio ya kisheria na kikatiba badala ya kutarajia mabadiliko kupitia mashinikizo au lawama zisizo na tija. Maboresho ya sheria au Katiba ni mchakato unaohitaji hoja madhubuti na maridhiano ya kitaifa, kwa kutambua ukweli mchungu kwamba Katiba sio mali ya vyama bali ni ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wito wa Kitaifa
Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapaswa kuchukua jukumu la msingi la kuhakikisha uchaguzi huru, wa haki, na wa kuaminika. Vyama vya siasa kwa upande wao vinapaswa kuwa washirika wa kweli wa demokrasia kwa kujenga imani kwa wananchi pasipo porojo. Pia ni muhimu
kuheshimu uhuru wa INEC si tu ni suala la kikatiba, bali pia ni kiashiria cha ukomavu wa kisiasa wa taifa letu.
Mwisho kabisa, demokrasia si mashindano ya kutafuta madaraka pekee, bali ni uwezo wa kushirikiana katika kuijenga Tanzania iliyo bora kwa wote.