Habibu B. Anga
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 6,557
- 25,748
- Thread starter
- #301
Daahh!! Sijui nisemeje.. Hii ndio type ya expertise tunayotaka, madini!!Mosi, hakuna suala la kutoka nje ya mada! Pili, bora umesema wazi kwamba "nyinyi mnaaamini kwamba video inatokana na maudhui....!" Sasa unless kama unataka na mimi niseme kama "mnavyoamini nyinyi!"
Sasa nirudi kwenye mada.
Jukwaa hili hili December 27, 2014 kuhusu video ya Mwana ya Ali Kiba nilisema:
December 27, 2014 hadi leo zaidi ya mwaka mmoja umepita na kuhusu video ya Diamond nimesema:Msisitizo kwenye RED & BLUE!!! Kwahiyo hapo utaona nilichosema dhidi ya video ya Diamond leo ndicho hicho hicho nilikisema dhidi ya Kiba zaidi ya mwaka mmoja uliopita kwahiyo hapo hakuna suala la u-Team!
Sasa tatizo lako wewe na wengine, unataka mtu akiimba "nikinywa maji nakuona kwenye glass" ndo basi tena unataka ionekane glass yenye picha ya mtu ndani yake. Sasa hiyo itakuwa ni kuzigeuza lyrics kuwa movie/video script!!! Naweka kumbukumbu sawa; hakuna dhambi kutengeneza story line lakini vile vile hakuna dhambi kutokuwa na story line basing on lyrics. Video script writer anaweza tu kuusikiliza wimbo mwanzo mpaka mwisho mara nyingi awezavyo kisha ana-develop theme! Story line atakayotengeneza itatokana na hii theme ambayo amei-develop na sio kugeuza mashairi kuwa ndio story line yeneyewe! Sasa ukiangalia Make Me Sing mwandishi alichoangalia ni kwamba wimbo unamzungumzia "my everything" wa mtu! Aka-develop maudhui ya namna gani mwanaume anakuwa tayari kwa lolote kwa "my everything" wake. Hapo akatumia robbery kuwasilisha message ya vile mtu alivyo tayari kwa lolote! Hata hivyo, kv ni sanaa mwandishi aka-conclude nini mwisho wa yote hayo! Umefanya tukio wajomba wakakuotea "my everything" wako mwenyewe ukamwacha!!!
Lakini kwa upande mwingine suala la story line works better kutegemeana na mashairi wa wimbo wenyewe! Kama umeisikiliza Utanipenda, just kwa mashairi yake tu unaweza kumsimulia mtu na akakuelewa! Yaani mashairi peke yake yanasimama kama hadithi na unaweza kutengenezea hata movie (sio video). Mfano mwingine ni Starehe. So, kwa mashairi kama hayo ndipo idea ya story line inayoendana na mashairi ya wimbo ina-work better!!
Salute mkuu..