Ajitokeza kumfufua NYERERE

Ajitokeza kumfufua NYERERE

...Kweli Radio hasa inayojiheshima inaweza kushindwa kuchuja Upumbavu usiostahili kurushwa hewani kwa Wasikilizaji wake??? Kweli Tanzania sasa ni ya Wafu wanaozika Wafu wenzao Kila uchao...:angry::angry:
 
Huyo babu ndo misukule yenyewe!ila asidharauliwe moja kwa moja,inawezekana baada wa JKN kuona ufisadi wa kutisha ndani ya chama chake anataka kurudi,hivyo kamtanguliza mjumbe.ha haa haaa!
 
Nitoke vipi hii. Mzee katamani kufanya ziara. Ile ndege ya sirikali inayoshughulikia milipuko ya malaria ingeweza kusaidia hapa fasta. Mama tibaijuka njoo.
 
Acha kusahihisha wewe, wee Mnyakyusa nini? Mwisho utasema hata Mwakyembe hatoki Kyela ingawa ni UKWELI 🙂

Ila ni SIRI yako usiwaambie watu. Sisi Wanyamwezi, watu wote wa Mbeya ni Wanyakyusa wa Kyela.
SAHIHISHO:Jenerali Mboma si mnyakyusa na wala hatokei kyela,kabla lake ni mmalila kutoka ileje,mbeya.
 
Ah!Haya bana . . . . . . . . . !!!!
 
co wote watumia user name fake.
For my side natumia my original surname na mengine yote.
 
Wanyakyusa Wajanja sana kwa kusaka hela na hasa vibabu. Ila wote tunajua General Mboma ndiyo alikomba za kutosha na kwenda kuzificha Kyela. Yaani haka kawilaya kadogo ila kameshatoa Wakuu wawili wa JWTZ, Msemaji wa Polisi, Mkuu wa Upepelezi Tanzania, Mbunge aliyesababisha Waziri Mkuu ajiuzulu, Mwanakijiji, Mtanzania, Babu wa Loliondo .......

Sasa hebu Mtanzania atupe habari zaidi, kwa nini Babu kaanzia kwenye Radio yake ya Kyela FM? Au wewe kijana na wewe umeanza Ujasilimali wa Babu wa Loliondo? Hahahaaaaaa, Wanyakyusa mpo juu sana. Kuna haja ya sisi jirani zenu wa Sikonge tujifunze mengi sana kutoka huko kwenu.

Mkuu hii wilaya ina maajabu, imetoa watu wawili wa familia moja kushika sekta nyeti nchini.
Adeni Mwamnyange
Denis Mwamnyange.!!
 
Kwa juu juu Babu anaonekana kituko lakini ukitizama kwa undani hasa hali ya sintofahamu ndani ya chama tawala usishangae babu kula shavu kwa kufuatwa awatabirie na kuwanyooshea mambo wakati wa uchaguzi. Niulize, ana tofauti gani na marehemu Sheikh wa Migomigo. Mbona alikuwa anakula shavu mpaka kwenye vituo vya luninga achilia mbali ofisi za vigogo. Nchi hii kila kitu kinawezekana ni gia yako tu. Hilo la kumfufua mchonga ni preamble ili tujue yupo lakini nionavyo hesabu zake ziko kwenye uchaguzi wa 2015. Teheee, teheee Tanzania.
 
Natamani kumuita Mtela Mwampamba aje amtumie ktika kampeni zake wawe wanahutubu kwa kinyakyusa
 
Let the man rest in peace. Mwalimu akishudia kinachoendelea Tanzania lazima atapata mshituko wa moyo.
 
Redio hiyo haifai kama inatoa taarifa za kijinga kama hizo bora ifungwe na tcra.huko si kuelimisha umma wa wanakyela ni kuwapumbaza
 
Hili jambo likiwezekana naachana na taaluma yangu na kujifunza uganga wa kienyeji
 
Mboma si mtu Kyela,kwao ni wilaya ya Mbozi na wala si mnyakyusa.
 
Mkuu hii wilaya ina maajabu, imetoa watu wawili wa familia moja kushika sekta nyeti nchini.
Adeni Mwamnyange
Denis Mwamnyange.!!
Devis Mwamunyange,andika vizuri majina ya watu.
 
Atangaze msaada anaotaka. Wa hali au mali???
 
Huyo mzee katumia lugha ya picha tu kuonesha kwamba mambo yanayoendelea hapa nchini hayampendezi na anahisi wenda Mwalimu angelikuwepo haya yote yasingetokea hadi anafika mbali na kusema anatamani Mwalimu awe msimamizi wa uchaguzi 2015.
In real sense hizo zote ni lugha za picha kuuonyesha upande tawala kwamba wamekiuka misingi na taratibu za utawala alizoziacha bb wa Taifa....rushwa na matumizi ya mabavu katika vipindi vya chaguzi mbalimbali ndivyo vinavyomuumiza mzee huyo na kwa lugha ileile ya picha ndo maana akasema kama hayo mambo maovu yote yataendelea basi CCM watashinda uchaguzi 2015. hayo ndio mawazo yangu wakuu.
 
Back
Top Bottom