Ajitokeza kumfufua NYERERE

Ajitokeza kumfufua NYERERE

Hivi hata anachoongea anakijua kweli.

Jamani kwani kutoka Mbeya kwenda Butiama ni mbali kiasi gani? Ajitokeze mtu mmoja hapo Kyela ampatie Mzee nauli aende tuone atakavyomfufua huyo Nyerere kwa hiyo funguo. Kwa nini tujaze server ya JF juu ya kitu kinachoweza kuthibitishwa kuwa ni ukweli au uongo.

Tiba
 
Tiba hapo kuna mtu wa kufika huku butiama kweli
au akifika atakuwa hoi kwenda kulaza tu hosp.

Last edited by a moderator:
Kweli kila radio inatafuta umaarufu kwa habari za ajabuajabu! huyu babu kesha fufua wangapi na nyerere atakuwa wangapi?
 
Tiba hapo kuna mtu wa kufika huku butiama kweli
au akifika atakuwa hoi kwenda kulaza tu hosp.

Huwezi jua Bwana huyo Mzee hajawahi kupanda ndege na anajua ili kuwezeshwa kufika Butiama, lazima apate chance ya kukwea pipa. Wazee wengine wajanja sana. Na sijui kufufua mtu kuna uhusiano gani na ufunguo!!!!

Tiba
 
Aliyefufuni nia Yesu Kristo na Petro mtume wa Bwana Yesu,
hao wengine ni mbwembwe tu na kutiana hasira.
Huwezi jua Bwana huyo Mzee hajawahi kupanda ndege na anajua ili kuwezeshwa kufika Butiama, lazima apate chance ya kukwea pipa. Wazee wengine wajanja sana. Na sijui kufufua mtu kuna uhusiano gani na ufunguo!!!!

Tiba
 
ilisivyowezekana kumfufua nyerere ndivyo ilivyo ngumu kwa CCM kushinda uchaguzi 2015
 
babu wa loliondo+huyu wa kumfufua nyerere. Hawa watu wa mbeya wanatufanya watz mazezeta sio
 
ilisivyowezekana kumfufua nyerere ndivyo ilivyo ngumu kwa CCM kushinda uchaguzi 2015

Na kweli. hawakumwelewa babu. m nafikiri anamaanisha CCM kushinda 2015 itawezekana tu kama Mwl J K N atafufuka na awe Campain manager wa CCM. kitu ambacho hakiwezekani.
 
Sio mbaya kashauza sura na Jina kwani kuna wengine wangependa wafahamike na tanzania nzima ndani ya mda mfupi kama yeye lakini wameshindwa. Ila hizo ni ndoto za alinacha! siku zote alikuwa wapi? Au walele wanasiasa wanaoamini ushirikina wamemtuma?Alafu Sura yake yenyewe inaleta maswali mengi kuliko hata maelezo yake!!@Bujibuji
 
Tanzania the 10th wonder
Maana tuna kila aina ya maajabu na vituko
 
Hapo kwenye kumfufua nilishtuka kidogo. Halafu na babu mwenyewe anavyotisha... Ila huo ubashiri ndio nikashtuka zaidi! Chapa kule hana lolote. Kwanza ajioteshe meno mdomoni na umri huo tuone!
 
Sim'bishii huyo babu anasema kweli kabisa, hivi hamjui kwamba hii nchi inaongozwa na mizimu? 75% ya viongoz wa CCM na serikali yao wote ni mizimu tu, wenyewe walishakufa muda mrefu sana na hii iliyopo sasa ni mizimu yao!

Umenipa maono fulani..... km Azimio la Arusha halipo tena najiuliza inawezakana vipi CCM ikawepo? Kweli haya mashati ya kijani yanawakilisha mizimu tu siyo CCM ... ndiyo maana viongozi wa kweli hawapo ... wapo hawa wa "FEDHA KWANZA".
 
Hata kama ingetokea amfufue Mwl. Nyerere nahakika kabisa Mwl. angefariki tena palepale kwa presha kutoka na nchi ilivyo kwa sasa!!
 
Wangempima alcohol content kwenye damu yake. Maana huenda kachanganya viroba na ulanzi + Baridi la Mbeya!
 
944738_554285484630700_523909365_n.jpg

MAAJABU YA MBEYA HEBU SOMA HII KWA MAKINI KABISA.

Huyu mzee alifika katika studio za Kyela FM,

anasema yeye anahitaji Msaada anataka kwenda kumfufua Mwl. Julius Kambarage Nyerere baba wa Taifa aliyefariki Miaka 15 iliyopita,

Na huo ufunguo ameushika mkononi ndiyo wa kumfufulia!

Madai yake mzee huyu anasema anaenda kumfufua na Mwalim ndiye atakuja kusimamia uchaguzi wa mwaka 2015.

Na pia anaibashiria CCM kuwa mshindi atatoka katika chama cha CCM.

Mimi nitamwamini endapo atafanikiwa kufufua uchumi wake kwanza.Sura yake inaonyesha uchumi wake ulikufa zamani.Hii ni njaa na ni mchawi kama wachawi wengine,namshauri atumie ungo kama anaweza kufufua mtu, badala ya kusubiri kuwezeshwa.
 
kaangwa una bahati sana umemchana laivu, hawezi kukuroga, ila ungemsemea pembeni ingekula kwako, lazima angekuotesha kwato miguuni

Back
Top Bottom