Ajitokeza kumfufua NYERERE

Ajitokeza kumfufua NYERERE

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,579
Reaction score
161,430
944738_554285484630700_523909365_n.jpg



MAAJABU YA MBEYA HEBU SOMA HII KWA MAKINI KABISA.

Huyu mzee alifika katika studio za Kyela FM,

anasema yeye anahitaji Msaada anataka kwenda kumfufua Mwl. Julius Kambarage Nyerere baba wa Taifa aliyefariki Miaka 15 iliyopita,

Na huo ufunguo ameushika mkononi ndiyo wa kumfufulia!

Madai yake mzee huyu anasema anaenda kumfufua na Mwalim ndiye atakuja kusimamia uchaguzi wa mwaka 2015.

Na pia anaibashiria CCM kuwa mshindi atatoka katika chama cha CCM.
 
Mmmmhh huyu babu naye ni njaa tu jamani, ila hapo mwisho sijaelewa, unasema anaibashiria CCM kushindwa au kushinda?

Mpwa Elli ujana wa Profesa wa matunguli Maji Marefu na Nchemba uzeeni ndo wanakuja kuwa wachawi kama huyu babu..
 
Last edited by a moderator:
Anataka kuyafanya hayo kwa Mamlaka ya nani?

Kashindwa kufufua wazazi na ndugu zake halafu kirahisi tu anataka kufanya hayo anayoyaota...
 
Mh nani atasimama na kumsikiliza mzimu nyerere. anataka kututishia watu tusilale .lol
 
Wanyakyusa Wajanja sana kwa kusaka hela na hasa vibabu. Ila wote tunajua General Mboma ndiyo alikomba za kutosha na kwenda kuzificha Kyela. Yaani haka kawilaya kadogo ila kameshatoa Wakuu wawili wa JWTZ, Msemaji wa Polisi, Mkuu wa Upepelezi Tanzania, Mbunge aliyesababisha Waziri Mkuu ajiuzulu, Mwanakijiji, Mtanzania, Babu wa Loliondo .......

Sasa hebu Mtanzania atupe habari zaidi, kwa nini Babu kaanzia kwenye Radio yake ya Kyela FM? Au wewe kijana na wewe umeanza Ujasilimali wa Babu wa Loliondo? Hahahaaaaaa, Wanyakyusa mpo juu sana. Kuna haja ya sisi jirani zenu wa Sikonge tujifunze mengi sana kutoka huko kwenu.
 
Kweli tutafika ?
Kama mtu anafika Studio ya Redio na kukaribishwa na kuuanza kumwaga pumba kama hizi alafu mtangazaji naye anaruhusu Ujinga kama huu sijui huko mbele ya safari Mungu atuongoze!
 
ndiyo maana kila kukicha namuomba Mungu asinichukue mapema nizidi kushuhudia maajabu ya walimwengu na vituko vya karne ya 21.........................
 
Na Masapila Loliondo alianza hivi hivi hawa watu wa mbeya sijui wana nn?
 
Mmmmhh huyu babu naye ni njaa tu jamani, ila hapo mwisho sijaelewa, unasema anaibashiria CCM kushindwa au kushinda?
hili lichama linaamini sana mambo ya ushirikina na endapo wataidandia hii theory ya huyu mzee majibu yako wazi, akimfufua wanashinda akishindwa kumfufua vis-vesa
 
Sim'bishii huyo babu anasema kweli kabisa, hivi hamjui kwamba hii nchi inaongozwa na mizimu? 75% ya viongoz wa CCM na serikali yao wote ni mizimu tu, wenyewe walishakufa muda mrefu sana na hii iliyopo sasa ni mizimu yao!
 
Back
Top Bottom