Ajira kwa Wazanzibar na Wabara

Mingendeu

New Member
Aug 26, 2019
1
1
Serikali inapaswa kutafakari ni kwa namna gani wanaweka usawa kwenye hili.

Wahitimu kutoka bara wanalalamika sana. Ajira zinazotangazwa bara wanasailiwa hadi wazanzibar, lakini ajira zinazotangazwa Zanzibar, sifa moja wapo kubwa ya kusailiwa ni kuwa mzanzibar.

Mzanzibar anafaida mara 2, anaweza kupata ajira Zanzibar au Bara. Hii ipo tofauti kabisa kwa wahitimu wa bara.

Serikali wanaweza kuchukulia swala hili kama swala dogo sana, ila kiuhalisia linakuza chuki ndani ya muungano wetu. (Ajira ni moja ya changamoto kubwa tena inagusa kundi kubwa yaani vijana).

Serikali kupitia ofisi wa makamu wa Raisi, wizara ya kazi pamoja na utumishi wanatakiwa wakae na kuchukua hatua za haraka mapema. Baada ya miaka kadhaa hili swala litakuwa kubwa na halitaweza kutatulika kirahisi.
 
Kuwa tu mpole. Maana viongozi wetu wa Tanganyika, wakiwa na akili zao timamu wamekubali tuwe na Muungano wa hovyo kabisa wa changu changu, chako changu na hao Wazanzibari.
 
Back
Top Bottom