Ajira za bara tunaomba wote, lakini za Zanzibar wanataka Wazanzibar pekee

Moussah17

New Member
Mar 21, 2024
1
0
Inapotokea tangazo la kazi/ajira Nchini kwa maana ya huku bara tunafanya application ya tangazo husika kwa kuzingatia vigezo vya umri miaka 18 hadi 45 sifa nyingine ni kuwa mtanzania kuwa na vyeti na mambo kama hayo. So kwa kawaida watanzania wote wenye sifa na vigezo kulingana na tangazo husika tunaomba nafasi hizo.

Ila kumekuwa na utofauti zanzibar
Kwa maana linapotokea tangazo lakazi kina kuwa na vigezo vya ziada kama kitambulisho cha mkazi je hapa shida inakuwa ni nini ikiwa bara zikitangazwa nafasi za kaz tunaomba wote ikiwa tu ni watanzania na je shida ikowap upande wa zanzibar waombe wenye vitambulisho vya kule tu 🤔😭
 
Zamani nliwahi omba kazi ya hotelini.nkaambiwa hutaweza wanzanzbar labda kama umejiandaa kisaikolojia na utaweza kuvumilia njoo..
Wabaguzi na watakufanyia visa eneo la kazi ndo yanayotokea huku
 
Muungano huu ni dhalimu
 
Zamani nliwahi omba kazi ya hotelini.nkaambiwa hutaweza wanzanzbar labda kama umejiandaa kisaikolojia na utaweza kuvumilia njoo..
Wabaguzi na watakufanyia visa eneo la kazi ndo yanayotokea huku
Tupe kisa kimoja cha mfano ulichofanyiwa hapo zanzibar katika kazi zako.
 
Muungano huu wanafaidika nao wanzazibari zaidi kuliko wabara ila kwa kulalamika wao utadhani ndio wananyanyasikaaaaa!
 
Tukiwa chuo fulani kule Dodoma miaka ya nyuma huko tulikuwa na Wazanzibar wanafanya kazi wizara nyeti huko kwao jamaa mmoja wa bara akawa anajaribu kutengeneza connection apate shavu kule Wazanzibar walimwambia waziwazi wewe wa Bara kule huwezi pata kazi kamwe. Hawa jamaa ni wabaguzi sana.
 
Mbona katika taasisi zinazohusu muungano wabara wapo wengi tu.
Tena ni zenye asali za nyuki wadogo kama BOT , TRA hata jeshini wapo wengi tu.

Hii wala sio ubaguzi ni ku balance tu, maana nchi ni ndogo sana so unaposema wabara wote wawe wanamiliki ardhi kule na watumishi kutoka bara waajiriwe kule kwa taasisi zisizohusu muungano kutakuwa hakuna wazanzibar tena.

Mbona mambo mengi bara wanafaidi huku tena uchumi mkubwa upo bara kuliko zanzibar.

Nikuulize unavijua viwango vya mishahara vya watumishi wa Zanzibar?

Ukiijua utaacha mdomo wazi.

Kiufupi Zanzibar hakuna uraia ni ukaazi tu wakati kabla ya Muungano Zanzibar kulikuwa na uraia wake mbona hamulitetei hilo na wakati ni nchi mbili zilizoungana?

Unapoleta mambo humu uwe unayapima kwa mizani ya uadilifu sio unaangalia upande mmoja tu.

Kwa ukweli wa mambo hata ajira zinazotoka kule sio nyingi kama za huku bara.
 
Inapotokea tangazo la kazi/ajira Nchini kwa maana ya huku bara tunafanya application ya tangazo husika kwa kuzingatia vigezo vya umri miaka 18 hadi 45 sifa nyingine ni kuwa mtanzania kuwa na vyeti na mambo kama hayo. So kwa kawaida watanzania wote wenye sifa na vigezo kulingana na tangazo husika tunaomba nafasi hizo.

Ila kumekuwa na utofauti zanzibar
Kwa maana linapotokea tangazo lakazi kina kuwa na vigezo vya ziada kama kitambulisho cha mkazi je hapa shida inakuwa ni nini ikiwa bara zikitangazwa nafasi za kaz tunaomba wote ikiwa tu ni watanzania na je shida ikowap upande wa zanzibar waombe wenye vitambulisho vya kule tu
Muungano wa hovyo kabisa huu hata ardhi wao wanahaki ya kumiliki wakati sisi hatuna mamlaka hayo kwao
Tumewalea vyakutosha
 
Back
Top Bottom