hekimanyingi
JF-Expert Member
- Jul 12, 2013
- 679
- 573
Kama kuna watumishi wa umma mil 2. Maana yake.kila.mtu kuna watu kumi nyuma yake ambao ni dependants directly or indorectly. Maana yake kuna watu 20Mil wanaoathirika na agenda hiyo. Utumishi wa umma kwa ujumla upo frustrated. Naona vyombo ya ulinzi na usalama.na wanasiasa ndo wananeemeka na nchi yetu. Hawa ambao wanaenda kutekeleza miradi ya afya, elimu, maji, umeme na vinginevyo wao hawapewi kipaombele kama miradi yenyewe. Ni rahisi sana kutibua mfumo wa itumishi wa umma ila itachukua miaka kuirejesha ikakaa vyema.
Miaka ilopita kumekukuwa na maboresho kadhaa ya kanuni za utumishi wa umma pamoja na mfumo mzima, ila miaka mitatu ilopita tangu awamu ya tano ianze, utumishi wa umma umezoroteshwa, matokeo yake yanaweza yasionekana ila najua laana kubwa itawakumba hawa wanayotekeleza haya.
Ukienda kwenye.mamlaka za serikali vyeo sasa hivi vimeanza tena kutolewa kwa upendeleo na kujuana, ikiwa ni pamoja na ukabila au ukaribu. Jambo ambalo linafanyika kwa siri.na hivyo si rahisi kuonekana kwa sasa.
Mishahara kutopanda huku vyakula na mahitaji mengine vinapanda bei ni jambo la hatari, viongozi wetu wa kitaifa hawaoni haya kwasababu wao na familia zao wanakula.na kushiba, huku wakijificha kwenye kivuli cha kutekeleza miradi ya maendeleo bia kuwafikiria wasimamiaji na watekelezaji wa miradi hiyo.
Siku watumishi wa umma wakikosa chakula, viongozi na mnaowatetea mtakuwa vyakula vyao.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake.