Mkuu umegusa mahali sensitive sana.
Kuna watu hawaitambui nguvu ya watumishi kwa sababu ya viburi vya Madaraka,hawafanyi maamuzi kulingana na miongozo iliyopo bali kwa utashi wao kupitia kauli zao wazitoazo.
Hili ni time bomb,watumishi anaowadharu atake asitake ndio watekelezaji wa Ilani ya chama chake na ndio watekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali yake.
Haboreshi hali ya utendaji kazi zao,haboreshi maslahi yao halafu anawaamuru tena kwa ubabe wafanye kazi kwa bidii,hii si uongozi bora,anapaswa ajitafakari ingelikuwa ni yeye angekuwa na morali ya kufanya kazi kwa bidii?
Morali ya utendaji kazi ya watumishi wengi sana hasa wa ngazi za kawaida wasiokuwa wakuu wa idara au vitengo ambao ndio wengi serikalini imeshuka sana ktk kipindi hiki cha uongozi cha awamu ya 5,hii kikubwa ni sababu wamejikatia tamaa kwa kudhulumiwa haki zao kwa hoja zisizo na mashiko.
Kama serikali inawaona ni mzigo na wage bill ni mzigo mzito kwake,ifanye rentranchment kubwa,iwape chao,iache watumishi wachache walioboreshewa maslahi yao kuliko kung'ang'ania halafu unashindwa kuwatumia.