Ajali ya Basi la Arusha Express na Lori yaua watano Dodoma

Poleni wasafiri kwa mkasa ulio wakuta, tusli na kupiga goti kwa kuendelea kuwa hai.

ni muhimu sana madereva wa mabasi na magari yote wawe makini sana katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka.

Tunawaomba Askari wa barabarani wasimchekeee dereva yeyote atakaye vunja sheria za barabarani haswa masafa marefu ya mikoani.
 
Sasa mkuu unawahi wapi...si ungekusanya habari kamili ndipo upost...kwani wanakukimbiza ndugu yangu? Ungesaidia kuokoa majeruhi na kutoa msada stahiki then uje huku utujuze wenzio.
Hata kapicha hakuna
Kuwa wa kwanza kupost kuna raha yake
 
Ajali muda huu maeneo ya Mzakwe (Dodoma)basi la Arusha Express likitokea Arusha kueleka Dodoma.

Tusubiri mamlaka husika zitatoa taarifa za vifo na majeruhi

====

Ajali imetokea mchana huu eneo la Veyula mjini Dodoma. Basi kampuni ya ARUSHA express ikitokea Arusha kwenda Mbeya, Imegongana uso kwa uso na lori.

======

Watu hao wamepoteza maisha papo hapo huku wengine wakijeruhiwa baada ya Basi hilo kugongana uso kwa uso na Lori Novemba 13, 2022 mchana eneo la Veyul, Makutupora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibiti ajali hiyo na kusema bado wanafuatilia chanzo cha ajali na athari zaidi zilizotokana na ajali hiyo.

"Ni kweli ajali hiyo ipo, watu watano wamepoteza maisha katika eneo la ajali na wengine kujeruhiwa na wamekinbizwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa matibabu," amesema Otieno.

Basi hilo lilikuwa linatoka Arusha kwenda Mbeya liligongana uso kwa uso na lori la kampuni ya ujenzi ya China Hydropower.

View attachment 2415508View attachment 2415509View attachment 2415510
kuna shida mahala hii nchi.
 
Daah nimesikitika sana nilipopata taarifa za hiyo ajali kuwa dereva wa lori alilala likawa limehama upande wake ile dereva wa bus kustukia ikabidi ahame kumbe ndio wanafatana uso kwa uso mbaya sana aisee...
 
Dah, kibuyu kimelia nje ya barabara kabisa IMG-20221113-WA0030.jpg
IMG-20221113-WA0030.jpg
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom