Ajali ya Basi la Arusha Express na Lori yaua watano Dodoma

Mzalendo39

JF-Expert Member
Apr 17, 2015
885
1,020
Ajali muda huu maeneo ya Mzakwe (Dodoma)basi la Arusha Express likitokea Arusha kueleka Dodoma.

Tusubiri mamlaka husika zitatoa taarifa za vifo na majeruhi

====

Ajali imetokea mchana huu eneo la Veyula mjini Dodoma. Basi kampuni ya ARUSHA express ikitokea Arusha kwenda Mbeya, Imegongana uso kwa uso na lori.

======

Watu hao wamepoteza maisha papo hapo huku wengine wakijeruhiwa baada ya Basi hilo kugongana uso kwa uso na Lori Novemba 13, 2022 mchana eneo la Veyul, Makutupora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibiti ajali hiyo na kusema bado wanafuatilia chanzo cha ajali na athari zaidi zilizotokana na ajali hiyo.

"Ni kweli ajali hiyo ipo, watu watano wamepoteza maisha katika eneo la ajali na wengine kujeruhiwa na wamekinbizwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa matibabu," amesema Otieno.

Basi hilo lilikuwa linatoka Arusha kwenda Mbeya liligongana uso kwa uso na lori la kampuni ya ujenzi ya China Hydropower.

20221113_152827.jpg
20221113_152829.jpg
 
Nakadori

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
8,557
19,983

SemperFI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
1,714
3,467
Watu hao wamepoteza maisha papo hapo huku wengine wakijeruhiwa baada ya Basi hilo kugongana uso kwa uso na Lori Novemba 13, 2022 mchana eneo la Veyul, Makutupora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibiti ajali hiyo na kusema bado wanafuatilia chanzo cha ajali na athari zaidi zilizotokana na ajali hiyo.

"Ni kweli ajali hiyo ipo, watu watano wamepoteza maisha katika eneo la ajali na wengine kujeruhiwa na wamekinbizwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa matibabu," amesema Otieno.

Basi hilo lilikuwa linatoka Arusha kwenda Mbeya liligongana uso kwa uso na lori la kampuni ya ujenzi ya China Hydropower.
 
4 Reactions
Reply
Top Bottom