Air Tanzania’s Airbus A220 suffers engine failure

Air Tanzania’s Airbus A220 suffers engine failure

soma mstari wa mwisho nielewe...
kwa kujadili ujinga wa kiwango hiki ccm itatawala milele..

tukijadili vya msingi kama tume huru na katiba tunaweza kutegemea kuitpa ccm..

pamoja?
Ccm haina uwezo wa kutawala milele kama chama cha siasa, bali ccm nguvu za dola ndio itaweza kutawala, tena sio kwa ridhaa ya wananchi, bali kupitia kubaka box la kura.
 
Tunahoji mkataba maana ndege sio bajaji. Ww kahoji mikataba ya bajaji, ni suala la kugawana maeneo tu ya kuhoji.
Ndiyo maana anakuambiaje! Hilo la mkataba wala usihoji kwani ni too advanced wako... Hata ukionyeshwa hakuna utakachoelewa. Waachie wataalam wewe endelea na shughuli nyingine zilizo kwenye uwezo wako.
 
soma mstari wa mwisho nielewe...
kwa kujadili ujinga wa kiwango hiki ccm itatawala milele..

tukijadili vya msingi kama tume huru na katiba tunaweza kutegemea kuitpa ccm..

pamoja?

Nani kakuzuia ww kujadili tume huru na katiba mpya?
 
Me nafikiri vifaa maalum vya ulinzi wa Rais ndio vimesababisha engine failure, waviondoe haraka.
 
Ndiyo maana anakuambiaje! Hilo la mkataba wala usihoji kwani ni too advanced wako... Hata ukionyeshwa hakuna utakachoelewa. Waachie wataalam wewe endelea na shughuli nyingine zilizo kwenye uwezo wako.

Kwakuwa ww uko hapa jukwaani una uelewa mdogo, basi unaamini kila aliye hapa ni kama ww au chini yako. Kwa taarifa yako kuna watu kibao wako serekalini tulikuwa tunawaburuza tu darasani, na tunajua uwezo wao na hata wakituona wanajua uwezo wetu. Hivyo kama ww huelewi shikilia hapo hapo, usitutujumuishe na sisi.
 
Una uhakika kuwa ndege ni zetu sote? Ulisikia maneno ya viongozi wa chama tawala waliyokuwa wakiyatoa pale uwanjani siku ya mapokezi ya ndege hizo? Zile ni mali za ccm mkuu,hivi unaweza kusema viwanja vya michezo ni mali ya nchi? Japo vilijengwa kwa nguvu za wananchi wote? Acha tu wengine waviombee mabaya maana vinatumika kama fimbo ya kuwaadhibu,hukumbuki Zitto kabwe alipopanda hiyo ndege watu walifanya kama headline kwenye magazeti yote ya ccm na vibaraka wao kina msiba?maana alionekana kama nguruwe aliyeingia msikitini!! Ya nini sasa?kwanza asilimia tisini+ ya watanzania Wazalendo wa kweli hawana hata mategemeo ya kuja kuweza kulipa nauli ya ndege,kwa hiyo kwao yawepo au yasiwepo kwao ni sawa tu! Tunayashangiliaga tu kwa kuwa wakubwa wanaolindwa na polisi,jeshi,migambo na mabunduki mengi wametulazimisha kushangilia,ila kiukweli hayana maana yoyote kwa mkulima wa mihogo na mtama huko namtumbo,kilimo chenyewe cha hand to mouth,nauli itoke wapi?
Tuache kurushiana maneno yasiyo na tija hapa, tuelekeze nguvu na akili zetu katika kumshukuru Mungu failure ya engine haikusababisha maafa, pengine tutoe ushauri wa nini kifanyike badala ya kukejeli as if ATCL haituhusu, ndege ni zetu sote, zinapotokea changamoto sote tuguswe sawia, kejeli, vijembe na kukatishana tamaa hakutuweki pamoja.
 
Hivi kipao mbele cha watanzania ilikuwa ni ndege hayo madenge ni hasara tu.bora tungewekeze kwenye maji.afya .elimu na mengineyo.kenya kila siku wanalia hasara
 
Will do that for sure....
Nyinyi endeleeni kunadilisha ndege imepata pancha na haikustahili kuharibika

My bad boss kuingilia uhuru wa wajinga

Sorry

Weka uzi uliowahi kuanzisha ukijadili habari za katiba mpya au tume huru ya uchaguzi, sana sana na ww huwa unachangia tu hizi hizi hoja za kina Lisu na kina Makonda wakitafuta baba waliokimbia watoto.
 
unataka kila ndege ya ATCL ikipatwa na hitirafu unataka Waziri Kamwele aite press

Hitilafu, sio HITIRAFU!

Tunaanza-anzaje kujadili usalama na ubora wa injini za ndege kama hata kuandika Kiswahili hujui ???

Watawala wanategemea sana watu kama wewe kuendelea kuwepo madarakani japo wameshindwa kazi...
 
Thx God, ndege imetua salama, na huo ndio ujasili wa rubani, kimsingi rubani kiongozi na wasaidizi wake wanapaswa kupewa pongezi nyingi, ktk biashara hayo mambo yapo sana, tatitzo wengine hata kuuza pipi tu hawajawahi kuuza, kwa hyo ukiwaeleza kuhusu changamoto za kibiashara wao hawajui,

Biashara inastaji nne mhimu
1) loose, loose, loose
2) loose, gain, loloos
3) gain, gain, loose
4), gain, gain, gain

Sasa kila stage inachangamoto zake, stage iliyongum sana ni ya kwanza, maana, inahusisha mtaji, bila faida, kwa mazingra yake biashara nying huwa zinakufa ktk kipind cha mwanzo wa biashara au kat..

Kwa airtz, wanapitia kwenye changamoto nying lkn naamin watavuka tu wakiwa na nia...
 
Binadamu wa kitanzania ni kichekesho sana, anashangaa ndege kupata matatizo wakati yeye kuna wakati mwili wake unalazwa mwezi mzima pale TMJ au Muhimbili.

Wewe mtengenezaji wa ndege unahitaji matengenezo ya mwili wako kwa mikono ya madaktari, unashangaa vipi unachokitengeneza kutengenezwa!!.
 
Haiwezi kuwa vita ya Mashirika ya ndege bali watengeneza Engine ambao ni GE,RR,PW
Hakika, nakubaliana na wewe kuhusu hilo, maana ukitoa oda ya kutengenezewa ndege, una nafasi ya kuchagua aina ya injini ambazo ni kati ya hizo ulizozitaja.
 
Ndege zilizonunuliwa hadi zikacost damu ya watu hazina baraka, watabaki kusema kuharibuka ni jambo la.kawaida.
Wakuu,

Ile Ndege yetu aina ya Airbus A220-300 iliyokuwa imeshikiliwa Afrika kusini katika uwanja wa Oliver Tambo jijini Johannesburg, jana imeendelea kupatwa na Majanga baada ya kudaiwa kwamba injini yake kupata matatizo wakati ikiwa angani ikitokea Mwanza kwenda Dar.

Imedaiwa rubani wa ndege hiyo aliamua kuirudisha Mwanza na kutua salama japo Injini itahitajika kubadilishwa ili iweze kupaa. Alikuwa kapaa angani urefu wa futi 7,500.

Matatizo kwenye ndege ni jambo la kawaida, tatizo ni kwanini tunafichwa habari? Kwa usiri huu napata wasiwasi kama ATCL inafanya kazi kwa viwango vya kimataifa. Wasafiri walitakiwa waambiwe tatizo na kuombwa radhi.

Nashauri tuiuze na hela tuwanununulie Bima ya Afya wajane na wote wasiojiweza Tanzania.

Angalia mchoro hapa chini ya U turn ya nguvu akiwa Singida njiani kwenda Dar akaamua kurudi Mwanza. Rubani apewe tuzo au cheo Serikalini. Kaokoa roho za watu..

image

Air Tanzania’s flight TC 123 from Mwanza to Dar es Salaam yesterday suffered an engine failure not long after taking off from the lakeside city.

The aircraft had reached an altitude of just over 7.500 feet when the engine failed and the pilots decided to immediately return to their airport of origin as the nearest point of landing.

The aircraft landed safely but will have to remain on the ground for an engine change.

Meanwhile does this seem to be another case of an Airbus A220 engine failing, which prompted the FAA earlier this month to issue an Air Worthiness Directive about several similar engine failures of the Pratt and Whitney Geared Turbofan engine, which affected Air Baltic but also other airlines operating this aircraft type.

The FAA notice, which was published on September 10th, i.e just over two weeks ago, proposes the inspections of the PW1500Gs and PW1900G. It also requires that the gap between the oil supply of the engine and the fuel oil cooler must to be inspected on a more regular basis. Operators of this engine type are already exchaning the fuel oil cooler and the supply tube for new components to comply with Pratt & Whitney’s own service guidance.

The issue came to light earlier this year when P&W addressed it with its service bulletins.

Meanwhile has Swiss recently also suffered two engine failures in flight, raising additional questions about the PW engines used, more so as Airbus had similar experiences when the A320NEO family was launched, using this engine type.

These engine failures have in the past also affected Korean Air and other operators, raising serious questions about P&W’s workmanship, component reliability and generally the safety of this engine type.

Air Tanzania has two Airbus A220-300 in service and only recently ordered an additional two such aircraft for delivery in 2021.

 
Back
Top Bottom